Invisible
JF Admin
- Feb 26, 2006
- 16,286
- 8,380
- Thread starter
- #101
Kuna mdau nimemtuma aelekee eneo la tukio na anatoa ripoti hii:
Kuna maandamano ya wananchi ambao wanatembea kwa miguu na wamefunga barabara ya Kilwa wakielekea eneo la tukio, hali inavyoonyesha likitokea jambo baya basi wanaoweza kufa ni wengi... Serikali ilitakiwa kuzuia raia yeyote asiye na sababu maalum kwenda eneo hili.
Polisi wanawazuia raia kukaribia eneo hilo kwani wandai mabomu yaliyolipuka ni 'cha mtoto' (akimaanisha madogo) na kuna bomu moja kubwa sana likilipuka basi litaweza kuzua mengine.
Ataendelea kunifahamisha kinachoendelea nami nitajitahidi kuwafahamisha nini kimejiri. Wasiwasi wangu ni endapo litalipuka hilo wanalodai ni kubwa, najiuliza pia, hakuna zimamoto ya haraka hapo kambini?