April '09 Bomb Blasts in Dar (Mbagala) and responses

April '09 Bomb Blasts in Dar (Mbagala) and responses

waziri wa ulinzi amenukuliwa akiwashauri wananchi wanaokaa katika majengo marefu watoke nje
 
Ni kweli kuwa kuna tatizo la kupata simu baada ya milipuko hii?

Fundi, ni watu wanajenga karibu na kambi za jeshi au silaha zinahifadhiwa kwenye makazi ya watu?

ni watu wanajenga karibu na kambi za jeshi, coz logic ni kwamba kambi zipo kabla ya makaazi ya watu
 
Pale Dodoma kuna hospitali nzuri sana (inaitwa Mirembe) GT kama unahitaji tiba waweza kwenda pale utasaidiwa.

Jamaa hawezi kujijua kama anahitaji kupelekwa Mirembe, bali jamii iliyomzunguka ndiye yenye jukumu hiyo. bado kuna watu wanafikiri kichaa ni mpaka aokote makopo!.
 
kwani hii ya leo inatofauti na ile ya jana?

maana jana i was so uncomfortable..unajua tena you never know hawa CHADEMA hawaaminiki

Mimi nafikiri bosi wako Rostam Aziz amefanya njama silaha zilipuke ili apate tenda ya ku-supply vifaa vya jeshi ili aipe CCM pesa za kampeni kwa ajili ya uchaguzi mwakani.
 
Nimesoma mwenyewe kwenye thread ya ITV sasa hivi kuwa naibu waziri wa ulinzi Mh Emmanuel Nchimbi anaomba wakazi wa mbagala waondoke eneo hilo na wale walioko kwenye majengo marefu washuke, siyo uongo ni breaking news toka ITV

We will keep you updated
 
Hali ni shwari sasa, turudi kwa RA kule.........
Hapana...

Hali si shwari. Kuna hali ya hofu kwa wazazi wenye watoto wao maeneo yale (shuleni) ambao wanatafuta kila namna ya kupata watoto wao na hawapatikani.

Red Cross ndo wanawasili sasa hivi.

Kuna bomu ambalo linaelekea kulipuka muda wowote kuanzia sasa. Moto unaendelea kuwaka tena kwa kasi kubwa zaidi.

Kama ulivyosikia Waziri akitangaza, mlio kwenye majengo marefu Dar mkae mkao wa kukimbizana likilipuka lile linalohofiwa.
 
nilikuwa maeneo ya Ubungo, nikadhani ni miungurumo ya radi......do we possess defective and worn out armaments or???
 
Ghala la silaha limeshika moto. Inasemekana kuna tatizo la kiufundi.Barabara ya kilwa kuelekea mbagala imefungwa. Wanene wote wa jeshi la ulinzi wako eneo la tukio
 
Nimeambiwa hivyo pia tena inasemekana mpaka sasa kuna tatizo la mawasiliano via landline, ati hata mobile communications zilikata! Hii inatokana na hii issue au ni michemsho ya TCRA?

Sasa hivi kuna mtu kaniambia kuwa watu kama 60 hivi inasemekana kupoteza maisha this is uncofirm news....
na ni za sms.....pls kama kuna mtu ana zaidi tufamishe
 
Vijana wawili wamekamatwa wakiwa wameiba mabaki ya mabomu na risasi za kutungulia ndege. Hii biashara ya vyuma chakavu itatutoa roho. Jamani walioko maeneo ya Mlimani tupeni habari hali ikoje huko? mitikisiko ni mikubwa?
 
Hapana...

Hali si shwari. Kuna hali ya hofu kwa wazazi wenye watoto wao maeneo yale (shuleni) ambao wanatafuta kila namna ya kupata watoto wao na hawapatikani.

Red Cross ndo wanawasili sasa hivi.

Kuna bomu ambalo linaelekea kulipuka muda wowote kuanzia sasa. Moto unaendelea kuwaka tena kwa kasi kubwa zaidi.

Kama ulivyosikia Waziri akitangaza, mlio kwenye majengo marefu Dar mkae mkao wa kukimbizana likilipuka lile linalohofiwa.

Invisible;

Hii ndo naita bla blah blah balaaaaaahhhh kutoka kwa waziri.

Inatakiwa huyo waziri aachane na politiki, awaachie wataalamu waseme hilo bomu la hatari linaloSUBIRIWA kulipuka likilipuka litafikia umbali wa KM ngapi?

Kwahiyo mtu anayeishi Tegeta kwenye ghorofa pia ashuke? au mwisho ni Chalinze?!?

Mie sishuki wanasiasa waongo.
 
Vijana wawili wamekamatwa wakiwa wameiba mabaki ya mabomu na risasi za kutungulia ndege. Hii biashara ya vyuma chakavu itatutoa roho. Jamani walioko maeneo ya Mlimani tupeni habari hali ikoje huko? mitikisiko ni mikubwa?

jamani binadamu wengine ni waajabu sana, wanaambiwa wasisogelee eneo la tukio wao ndio kwanzaa...khaa
 
Invisible;

Hii ndo naita bla blah blah balaaaaaahhhh kutoka kwa waziri.

Inatakiwa huyo waziri aachane na politiki, awaachie wataalamu waseme hilo bomu la hatari linaloSUBIRIWA kulipuka likilipuka litafikia umbali wa KM ngapi?

Kwahiyo mtu anayeishi Tegeta kwenye ghorofa pia ashuke? au mwisho ni Chalinze?!?

Mie sishuki wanasiasa waongo.

FP mswalie mtume,...roho tamu, teremka baba!
 
Back
Top Bottom