Kwa wale mlio Dar,
Kutakuwa na milipuko flani mnaisikia. Ni mabomu ambayo yanalipuka eneo la kambi ya Jeshi Zakhem - Mbagala.
Hii inaweza kupelekea mitikisiko isiyotarajiwa.
Nimefahamishwa ili nitoe tahadhari hii mapema. Nini kinaenedelea? Tutafahamishana
HApa sasa tujiwekee picha kuwa tuko katika nchi ya vita. ni nafasi yetu ya kujua yale ambayo wenzetu wa mogadishu, Palestina, Irak r.t.c wanaishije kwa kihoro kama hiki, tena kwao kiukwelii na si kama hapa.
kwani hii ya leo inatofauti na ile ya jana?
maana jana i was so uncomfortable..unajua tena you never know hawa CHADEMA hawaaminiki
Tahadhari imetolewa kutoka jeshini kuwa ghala kubwa la silaha hapo mbagala base huenda likalipuka, watu wanatakiwa kuwa mbali ya radius ya kilometer 25! Tafadhali wajulisheni wengine!
Pia ninataarifa kuwa hospitali ya temeke imejaa watu waliojeruhiwa na wengi wamezimia hasa watoto wa shule.
Barabara kwenda mbagala imefungwa pia!
...Polisi wanawazuia raia kukaribia eneo hilo kwani wandai mabomu yaliyolipuka ni 'cha mtoto' (akimaanisha madogo) na kuna bomu moja kubwa sana likilipuka basi litaweza kuzua mengine.
Ataendelea kunifahamisha kinachoendelea nami nitajitahidi kuwafahamisha nini kimejiri. Wasiwasi wangu ni endapo litalipuka hilo wanalodai ni kubwa, najiuliza pia, hakuna zimamoto ya haraka hapo kambini?
...Inasemekana kuna bomu ambalo linaweza kulipuka anytime limehifadhiwa kwenye ghala hilo. Zimamoto wanajitahidi kwa kushirikiana na Knight Support na Ultimate Security...
Tatizo kubwa ni kuwa Polisi hawana vipaza sauti, wanawapiga raia kwa kuwaonea maana hawajui kinachoendelea na hawajatangaziwa. Polisi ni wengi lakini hawana vipaza sauti na kuwapiga raia ni uonevu maana hakuna mawasiliano na makelele ya wananchi yanazidi sauti ya askari bila kipaza sauti!
Tahadhari imetolewa kutoka jeshini kuwa ghala kubwa la silaha hapo mbagala base huenda likalipuka, watu wanatakiwa kuwa mbali ya radius ya kilometer 25! Tafadhali wajulisheni wengine!
Pia ninataarifa kuwa hospitali ya temeke imejaa watu waliojeruhiwa na wengi wamezimia hasa watoto wa shule.
Barabara kwenda mbagala imefungwa pia!
Kuna mdau nimemtuma aelekee eneo la tukio na anatoa ripoti hii:
Kuna maandamano ya wananchi ambao wanatembea kwa miguu na wamefunga barabara ya Kilwa wakielekea eneo la tukio, hali inavyoonyesha likitokea jambo baya basi wanaoweza kufa ni wengi... Serikali ilitakiwa kuzuia raia yeyote asiye na sababu maalum kwenda eneo hili.
Polisi wanawazuia raia kukaribia eneo hilo kwani wandai mabomu yaliyolipuka ni 'cha mtoto' (akimaanisha madogo) na kuna bomu moja kubwa sana likilipuka basi litaweza kuzua mengine.