April '09 Bomb Blasts in Dar (Mbagala) and responses

April '09 Bomb Blasts in Dar (Mbagala) and responses

jamani mimi nipo norway, kwetu ni maeneo ya buguruni, nawapigia simu nyumbani hazipatikani, kama kuna maafa nijulisheni.
 
Maeneo ya mlimani hali ilikuwa mbaya kiasi, manake wengi walifikiri ni radi, lakini majengo yametikisika na magari yenye alarm yamelipuka, mlipuko wa ving'ora.
 
ndio maana marekani wanasema kuna nchi hazitakiwi kuwa na silaha laki kwa sababu hawana uwezo wa kuzihudumia wala kuzitunza.....nafikiri jeshi letu limejisahau kazi ....wanaonesha uwezo mdogo hata wa kutunza milipuko....je tungekuwa na nuclear au atomic ..si dunia ingeteketea..thats why america hawataki silaha za hatari ziendele kusambaaa....

AU ISIJEKUWA PIA TUMEUZIWA SILAHA ZINAZOKARIBIA EXPIRED DATE BILA KUJUWA ...MAANA NJAA MBAYA SANA!!!
PM kuna kitu kinanigonga akilini kuwa hilo unalolisema sio njozi bali ndio ukweli wenyewe. Lakini hata tukiujua ukweli huo tutafanya nini? hayo yatakuwa marudio ya tabia za nchi hii.
 
jamani mimi nipo norway, kwetu ni maeneo ya buguruni, nawapigia simu nyumbani hazipatikani, kama kuna maafa nijulisheni.

Edson maafa hayajafika Buguruni ondoa shaka. Kuna tatizo pia la network ndugu yangu. Usipanick bure
 
vipi jamani hali inaendeleaje?

wengine hatupo bongo na namba za sim za watu ninaowajua bongo hazipatikani

vipi mabomu yanaendelea kulipuka?

up dates plz
 
Hivi mnategemea kitu gani hapo ? Maana ghala au godown linapowaka ujue tayari watu wameshatoweka na vitu kibao ,kwa hili la ghala la silaha si ajabu watu wameshakwiba silaha kibao tena nzito nzito ,kuna watu walikuwa wanakamatwa na mabomu ya kutupa na mkono ukifuatilia unaambiwa ,wanayatoa nchi jirani ,kuna wale waliolipukiwa wakiwa wanakusanya vyuma chakavu ,eti hawakuyajuwa ,ndio hivyo ,hapa kama hakuna kosa la uzembe basi tukae mkao wa kutoka mbio ,watu aka mafisadi wameshaiba silaha na ghala kulitia utambi.

Hapa ni wizi tu wameshaiba silaha hakuna jingine ,ushahidi umeshapotea tusubiri stori za kubuni.
 
Mkuu Invisible mbona kama post zinajirudia rudia kwenye hii thread. What has happened? au ni macho na computer yangu????

Asante sana kwa kutujuza kwenye hili kweli JF ni kiboko wa kwanza kujua.

Bomu li-papa limeshalipuka. Lile kubwa lao?
Sio kwako tu, na kwangu pia. Nikafikiria mimi ndo nimechanganyikiwa, maana hii habari inatisha na kusikitisha. Aibu nyingine ya taifa!
 
Sio kwako tu, na kwangu pia. Nikafikiria mimi ndo nimechanganyikiwa, maana hii habari inatisha na kusikitisha. Aibu nyingine ya taifa!
Ikiwa ni ajali sitokubali kuambiwa kuwa ni kosa la uzembe na hakuwezi kutikea uzembe kwenye ghala la silaha kirahisi, kumbukeni tu kuna mitambo ya Nyuklia kibao inaripuka na mengine inafanya tundu tu na kupenyesha hewa katika mazingira na kuenea ya uraiani .
 
Kova anasema kuwa hali inakuwa shwari tofauti na asubuhi na wote walio katikati ya jiji waendelee na shughuli zao. Watu wa Mbagala wameombwa waendelee kufuata maelekezo.

Majeruhi watatibiwa bure, nyumba zilizoharibiwa watafanyiwa utafiti na serikali itasaidia.
Kwenye nyumba ambazo mabomu yamedondokea wameshauriwa kureport polisi wasijaribu kuyashusha toka juu ya nyumba zao.

Pia kuna mabomu mengi yaliyofunguka bila kulipuka na inasemekana watu wameyaokota na kwenda nayo kusikojulikana na uwezekano mkuu ni kuwa yatalipuka baadae.

Mtu asijeenda nalo Kariakoo au kupanda nalo daladala
 
yasije yakaangukia mikononi mwa magaidi....
 
Habari niliyoletewa na bro ambae anaishi karibu na kambi hiyo ,anasema majeshi walitoka mkuku ,hakuamini macho yake ,kati yao alifululiza ukumbini hadi ****** na mabuti yake huku akiwa amevalia kombati,alipouulizwa kunani akawambia kuwa ghala la silaha limevamiwa na majambazi katika kubadilishana risasi ndipo zilipokosa watu na kupiga kwenye magunia ya maguruneti na makasha mengine ya silaha na hapo ndipo palipotokea pata shika ya kurushiana risasi bila mpango na huku mabumu yakianza kuripuka na moto kuenea kwenye magunia mengine ,ila jamaa alikuwa akihema ile mbaya anasema kama kengele ,ila baadae alirudisha akili yake na kuondoka lakini aliona aibu sana ,bro alipewa habari hizo na watoto wake ambao wanasoma hapo Mbagala yeye yuko mipakani akiwa katika kazi za patrol za kijeshi ya mipaka ya Tanzania somewhere Southwest of Tanzania.
 
jamani mimi niko kwenye gorofa mnanishaurije nitoke au nibaki naona wengine wote wametoka

Aaagh, Usishuke Rafiki yangu. Wewe ni mwanaume bwana,baki huko huko mkuu.waache waoga wakimbie,wewe endelea kuchungulia maendeleo ya huo msukosuko toka ghorofani tu i
 
Back
Top Bottom