Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Zaidi ya watu 300 wangine wakiwa na majeraha makubwa, wanaendelea kutibiwa, siku moja baada ya milipuko ya mabomu kutokea nje Dar es Salaam nchini Tanzania.
Maofisa wa serikali wa nchi hiyo wanasema idadi ya watu waliokufa imeongezeka na kufikia watano na huenda ikaongezeka zaidi. Wanajeshi watatu inaarifiwa hawajulikani walipo.
Uchunguzi unaendelea wa kujua chanzo cha milipuko hiyo iliyotokea kando ya kambi ya jeshi kwenye ghala la silaha nje ya jiji la Dar es Salaam.
Mamia ya watoto ambao walikimbia kwa hofu eneo la Mbagala kwenye lenye ghala hilo la kuhifadhia silaha inaarifiwa hawajulikani walipo.
Rais Jakaya kikwete ametembelea eneo lilipotokea milipuko hiyo, siku moja baada ya kadhia hiyo iliyoleta hofu miongoni mwa wananchi wa Dar es Salaam wakifikiria kumetokea shambulio jingine la kigaidi kama lililotokea katika ubalozi wa Marekani mwaka 1998 jijini Dar es Salaam.
Mwandishi wa BBC Vicky Ntetema ametembelea kambi ya muda ya shirika la msalaba mwekundu nje ya jiji la Dar es Salaam maalum ya kuwaunganisha wazazi waliopotelewa na watoto wao.
Amesema vijana 250 walikuwepo katika kambi hiyo asubuhi ya Alhamisi na wachache bado hawajulikani.
Lakini wazazi wengi waliotembelea kambi wamesema watoto wao bado wajulikani walipo na kuna ripoti kwamba watoto 750 bado hawajaonekana.
Mashuhuda wamesema watoto kadha waliokuwa wamehamanika walizama katika mto ulifurika karibu na eneo la tukio.
kilichotokea jana mbagala kinaweza kikatokea popote palipo na kambi za jeshi . Ni vema planners wetu wa miji wakubali ukweli mji si lazima nyumba ziungane kama ushanga. Maeneo hayo haykutakiwa kuwa na makazi jirani. Tamaa ndio inayotuponza, nenda mbezi beach kunaeneo ambalo jeshi linalitumia kama seehmu ya kupigia shabaha, tayari viwanja vimegawiwa kulizunguka. Nni wazi jeshi haliwezi kuhamisha kambi zake kila mara watu wanapoencroach maeneo hayo. Tubadilike mawazo la sivyo majanga haya hayepukiki.
Hivi Mbagala wataipigia kura CCM kweli?
Au yote yatasahauliwa baada ya siku chache kama kawaida?
Serikali yetu is unprepared for this nature of disaster, we've been cought off guard, hakuna anayejua nini cha kufanya wapi na vipi, it was chaos. the death list imefikia 17 with two more kids na bado..jamani, hivi tuna serikali kweli?? au ni serikali inayoendeshwa na matukio tu?? you can't believe this, eti wananchi ndio wanaopoa miili ya marehemu toka mtoni??
Hivi mbona Serikali haituelezi kinachoendelea kwa uwazi? Taarifa ya bbc inashtua sana, mbona Serikali inaficha masuala ya majanga? so sad hii inanikumbusha bus la Abood lililopata ajali na wakaamua kuzika maiti ili kuficha ukweli, Tanzania LOL!
Hivi Mbagala wataipigia kura CCM kweli?
Au yote yatasahauliwa baada ya siku chache kama kawaida?
fang fang inamaanisha nini?