April '09 Bomb Blasts in Dar (Mbagala) and responses

April '09 Bomb Blasts in Dar (Mbagala) and responses

Sijui walifikiria nini kuweka godawni ya mabomu karibu na makazi ya watu!
 
Hivi mbona Serikali haituelezi kinachoendelea kwa uwazi? Taarifa ya bbc inashtua sana, mbona Serikali inaficha masuala ya majanga? so sad hii inanikumbusha bus la Abood lililopata ajali na wakaamua kuzika maiti ili kuficha ukweli, Tanzania LOL!

Zaidi ya watu 300 wangine wakiwa na majeraha makubwa, wanaendelea kutibiwa, siku moja baada ya milipuko ya mabomu kutokea nje Dar es Salaam nchini Tanzania.
Maofisa wa serikali wa nchi hiyo wanasema idadi ya watu waliokufa imeongezeka na kufikia watano na huenda ikaongezeka zaidi. Wanajeshi watatu inaarifiwa hawajulikani walipo.
Uchunguzi unaendelea wa kujua chanzo cha milipuko hiyo iliyotokea kando ya kambi ya jeshi kwenye ghala la silaha nje ya jiji la Dar es Salaam.
Mamia ya watoto ambao walikimbia kwa hofu eneo la Mbagala kwenye lenye ghala hilo la kuhifadhia silaha inaarifiwa hawajulikani walipo.
Rais Jakaya kikwete ametembelea eneo lilipotokea milipuko hiyo, siku moja baada ya kadhia hiyo iliyoleta hofu miongoni mwa wananchi wa Dar es Salaam wakifikiria kumetokea shambulio jingine la kigaidi kama lililotokea katika ubalozi wa Marekani mwaka 1998 jijini Dar es Salaam.
Mwandishi wa BBC Vicky Ntetema ametembelea kambi ya muda ya shirika la msalaba mwekundu nje ya jiji la Dar es Salaam maalum ya kuwaunganisha wazazi waliopotelewa na watoto wao.
Amesema vijana 250 walikuwepo katika kambi hiyo asubuhi ya Alhamisi na wachache bado hawajulikani.
Lakini wazazi wengi waliotembelea kambi wamesema watoto wao bado wajulikani walipo na kuna ripoti kwamba watoto 750 bado hawajaonekana.
Mashuhuda wamesema watoto kadha waliokuwa wamehamanika walizama katika mto ulifurika karibu na eneo la tukio.
 
Hivi Mbagala wataipigia kura CCM kweli?

Au yote yatasahauliwa baada ya siku chache kama kawaida?
 
Unajua baada ya kutokea kwa milipuko, watu walichanganyikiwa. Sisi kama Polisi tukatumia mwanya huo kujipanga vema kukabili tukio hilo,`` akasema Kamanda Kova.

Akasema hali hiyo ilisaidia kudhibiti matukio ya wizi ambayo yangeweza kutokea katika majumba ya watu ambamo wenyewe waliyaacha na kukimbia milipuko.

``Kulikuwa na majaribio ya vibaka kutaka kuiba, lakini walidhibitiwa maana tulilijua hilo na tukajipanga mapema,`` akasema Kamanda Kova.

Hata hivyo Kamanda Kova amesema watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni vibaka walikamatwa wakiwa katika harakati zao za kupora.

Akasema kibaka mmoja alikamatwa na askari akiwa amekwapua boksi lililokuwa na shehena ya risasi na kutaka kutokomea nalo.

Akizungumzia hali ya usalama katika eneo hilo, Kamanda Kova amesema hivi sasa hali ni shwari na amewasifia askari wa JWTZ kwa kazi nzuri ya kujitahidi kudhibiti mabomu mengine yasiendelee kulipuka.
____________________________________________

Ni wangapi hawakukamatwa ambao walitoweka na silaha zikiwemo hizo risasi ?
Kamanda sijui anaongelea kitu gani hivi wakati mabomu na risasi zikirindimba na kuwaka kunaweza kutokea ushupavu wa mtu kujitolea kudhibiti.

Inasemekana hakujasogea mtu wala mdudu karibu na sehemu husika na jeshi linajipanga kuparipua tena pahali hapo ili kumaliza mabaki na sio kwenda kupitisha reki kusafisha ,ila watu wengine kwa kujisifia ndio hivyo tena ,yaani hata hapa kwenye maafa mtu anasaka cheo.
 
kilichotokea jana mbagala kinaweza kikatokea popote palipo na kambi za jeshi . Ni vema planners wetu wa miji wakubali ukweli mji si lazima nyumba ziungane kama ushanga. Maeneo hayo haykutakiwa kuwa na makazi jirani. Tamaa ndio inayotuponza, nenda mbezi beach kunaeneo ambalo jeshi linalitumia kama seehmu ya kupigia shabaha, tayari viwanja vimegawiwa kulizunguka. Nni wazi jeshi haliwezi kuhamisha kambi zake kila mara watu wanapoencroach maeneo hayo. Tubadilike mawazo la sivyo majanga haya hayepukiki.

Wala sio tamaa. Statistics zinaonyesha kwamba wakazi walioko mijini hapa Tanzania ni asilimia 33 ya population. Juzi nimeona taarifa inayosema ongezeko la watu kuhamia Dar es Salaam ni la wastani wa asilimia 7 kwa mwaka.

Kuhamisha kambi si lazima. Ila kambi zilizozungukwa na makazi ya watu kuendelea kuhifadhi silaha nzito, ni kituko cha mwaka. You simply can't get away with that stupidity.
 
The worst is still to come. Can you imagine wave ya crime inayokuja. How many guns will be unnaccounted for!!! How many of these will end up in the wrong hands. Tunauchaguzi next year isn't this a sure recipy for blood shed.
Watanzania wengi wamepumbazwa na hali ya utulivu tuliyonayo kiasi kwamba we take peace for granted. Kwasbabu peace was there without our effort, is here without our effort, it will be there without our effort.

Kuna quote ya mtu hapa inasema something like politics is to serious/important an issue to be left to the politicians. How true!
 
wakulu,
nasikia tetesi kwamba bado hawajafanikiwa kuyategua yote yaliyosalia. ukichukulia joto la dar ukachanganya na la milipuko inaweza hali ikarudi kama juzi.
je serikali ina mipango ipi kuevacuate wakazi wa mbagala au tuseme kupunguza madhara?
 
Hivi Mbagala wataipigia kura CCM kweli?

Au yote yatasahauliwa baada ya siku chache kama kawaida?

Wewe hivi unawajua watanzania au unawasikia tu? wataipigia kura za kutosha tu.

Watanzania huwa tunakaa na jambo kwa muda mfupi sana, kusahau yaliyopita ni kawaida yetu hata kama yalikuwa na madhara kiasi gani.
 
jamani, hivi tuna serikali kweli?? au ni serikali inayoendeshwa na matukio tu?? you can't believe this, eti wananchi ndio wanaopoa miili ya marehemu toka mtoni??
 
jamani, hivi tuna serikali kweli?? au ni serikali inayoendeshwa na matukio tu?? you can't believe this, eti wananchi ndio wanaopoa miili ya marehemu toka mtoni??
Serikali yetu is unprepared for this nature of disaster, we've been cought off guard, hakuna anayejua nini cha kufanya wapi na vipi, it was chaos. the death list imefikia 17 with two more kids na bado..
kwa kweli ni masikitiko makubwa...
 
Serikali imetoa mkono wa rambi rambi shs. Milioni nne kwa waanga wanne wa mambomu huko mbagala. Je, hiyo fidia inalinagana na thamani ya mtu? take into account vifo hivyo vimesababishwa na waajiriwa wa serikali.

Sijasikia mpango wa muda mrefu wa serikali katika kuzuia na kupambana na maafa. Harama za nyakati zilianza kuonekana toka enzi za Mv. Bukoba lakini hakuna kitu cha msingi kilichofanyika.

Bomb blasts: Death toll climbs to 18By Vicent Mnyanyika

Four children who died in Wednesday�s bomb explosions at a military depot in Dar es Salaam were buried yesterday, as the death toll rose to 18.

The four children, who were buried at separate funerals in the Mbagala suburb, near the military facility, some 15km from the city centre, are Kasim Kaniki, Anton Joseph, Salha Harajabu and Tumaini David.

Dar es Salaam Regional Commissioner William Lukuvi said the Government had donated Sh4 million to the families of the four children to help defray burial costs.

He told reporters that the families would also receive food and an additional Sh1.5 million on Monday, as a gesture of condolence from the Government.

"We have set up two committees, one led by the Temeke Mayor, to oversee burial arrangements and another to evaluate the extent of the damage caused,"said Mr Lukuvi.

Meanwhile, more bodies were recovered from Kizinga River at Mbagala. The victims drowned, as they fled following the explosions, which stunned the city, with the effects being felt as far as 20km away. Workers in the tall buildings in the city centre had to be evacuated, as panic spread.

Among the bomb blast casualties were eight civilians who lived near the army facility. Also killed were five members of the Tanzania People's Defence Forces (TPDF), who were at the munitions depot, when the massive explosions occurred.

Yesterday, the Government confirmed the new death toll and said search teams were still scouring the river for bodies. The Dar es Salaam Red Cross announced that over 500 children had been missing since Wednesday.

Initially, some 1,180 children had been reported missing, according to Red Cross chairperson Mayasa Mikidadi. The Government pledged assistance to the bereaved families to enable them to bury their dead.

Mr Lukuvi also announced that two of the bomb blast victims would be buried later in Singida and Musoma. "The Government will also provide transport and help meet the burial costs," he sad.

Mr Kaniki Masanja, a relative of the two victims, said the gesture was a big consolation to the bereaved families.

Various donations were received from individuals and companies, with the Quality Group Company giving five tonnes of rice, cooking oil, water, mattresses and blankets worth Sh30 million to the affected Mbagala residents.

The company's group human resources manager, Mr Amir Ali, on behalf of Quality Group managing director Yusuph Manji, handed over the donations to Mr Lukuvi. He said the company had been touched by the incident and urged other well-wishers to assist the victims.

IPP executive chairman Reginald Mengi donated Sh25 million, which he handed over to Temeke Mayor Jerome Bwanausi.

An official statement on the explosion is expected by the end of next week, and the Government has urged the residents who fled their homes to return and help ascertain the number of missing people.

Most of the people who were injured are still recuperating at Temeke Hospital, while only one, whose condition was reported to be serious, had been referred to Muhimbili National Hospital (MNH).

The chief medical officer at Temeke Hospital, Dr Asha Mahita, said 36 people were still being treated at the hospital.

Among them is a child � Anna Hamis � whose parents or relatives have not been traced. Dr Mahita urged them to turn up and collect the child, who says she lives at Mbagala Kizuiani.
Source:TheCitizen Newspaper
 
Hivi mbona Serikali haituelezi kinachoendelea kwa uwazi? Taarifa ya bbc inashtua sana, mbona Serikali inaficha masuala ya majanga? so sad hii inanikumbusha bus la Abood lililopata ajali na wakaamua kuzika maiti ili kuficha ukweli, Tanzania LOL!

Nziku..

Samahani mimevutiwa na swali lako sijafuatilia comments nyingine lkn habari iko hivi

..nina ndugu yangu ambae ni askari (ninakaa nae nyumba moja) alinidokeza kuwa kwa siku ile y apili yake tuu (baada ya mlipuko) wali kuswanya/ opoa/ okota (nisameheni kwa lugha hiyo) MAITI zaidi ya 80 na walipewa amri ya kutotangaza kiasi cha maiti walichokiona...niliumia sana
 
Hivi Mbagala wataipigia kura CCM kweli?

Au yote yatasahauliwa baada ya siku chache kama kawaida?

hahaaaaa... wakati jana kwenye taarifa ya habari mama amelala nje na mtoto wake hana pakwenda naanmwambia Jerry Moru anaishubiri serikali na CCM waje 'kuwasaidia' na anonyesha kabisha yeye anafikiri kuwa CCM pia ni serika (u know wat I mean) @$%^&*... nikasikitikia chadema ambavo hawaoni vitu kama hivi.. nikagundua sasa inabidi vyama vianze kuwa marketed kama bidhaa seriously
 
Kama hawatangazi ukweli juu ya watu waliokufa kutokana na mabomu hayo ,watawazika kimya kimya? Maana ambao mpaka sasa hawajulikani wako wapi ni zaidi ya watu 700 sasa hawa wote je?ni kweli kuwa wamepotea njia za kurudi majumbani mwao? ama wako wapi hii ni hali ya hatari sana kama tunaweza kuficha kama vile tuko vitani....
 
Je swala la mlipuko wa mabomu ndio limekuwa hadithi ama kunahatua zinazochukuliwa? Nona serikali iko kimya kabisa! Kunamaswali ambayo yaniumiza kichwa!

a) je kunataarifa za ziada zinazotelewa kuhusiana na mlipuko huo? Kwa mfano matamko ya serikali! Wachunguzi binafsi! Namaanisha serikali isimame kidede na ituambie a, b, c d.
b) Je kiwango cha maafa na uharibifu kimeshatadhiminiwa au wameanza kutadhimini? Kwa mfumo upi? Mpaka sasa Ni kiasi gani cha mali ya wananchi? Idadi maalumu ya vifo, nyumba zilizoharibika! Mpango wa fidia ukoje?
c) Je thamani ya mabomu ni kiasi gani? Yaliyolipuka yalikuwa mangapi? Ya aina gani? Kwanini yalipuke? Chanzo chake! Hata kama watagoma kutangaza kwa kudaini ni maswala ya kiusalama wa taifa! wajuie kwa hakika nini kilichoendelea!
d) Je kunampango wa kununua mabomu mapya? Maana nchi haiwezi kutokuwa na dhana za kujilinda, si ndivyo? Budget hiyo inatoka wapi? Mabomu tunanunua wapi? Lini? Baada ya uchaguzi ama kabla ya uchaguzi?
 
He heee! we Paukwa nenda pale upanga utapata majibu yote.Lakini ukiingia ndani ya geti tu, jitayarishe kwa fang-fang
 
kama kuna viongozi wasanii ni tanzania..hawaangalii sehemu ya kufanyia usnaniii..jamani nendeni mkaone watu wanavyohangaika kule...sasa hali inaelekea mbaya vyoo vibovu na vingine vimelipuliwa sijui uchafu ulielekea wapi???sasa wananchi wameanza kujisaidia hadharani ...mi sidhani tunaiajika kufikia huku....nadhani muheshimiwa rais muangalie sana hii misaada isije ikaleta maafa ,mkaanza kutafuta dhahama kumbe wachawi serikali yako.....vile vile jamani wananchi twendeni tukawape misaada hawa watu vile vitu vinavyotolewa vinaishia mifukoni..nendeni mkaone watu wanalalamika kulala na njaa mbaya zaidi hadi watoto sasa zile million 25 za MENGI na PAPA MANJI sijui zinafanya kazi gani jamani??
MUNGU ATUREHEMU
 
Back
Top Bottom