Elections 2015 Apson awatumia kina Bashe kuwachafua Membe na Jack Gotham

Mtu aliyefiwa, mtanzania wa asili, anayejitangaza kuwa ni mjukuu wa mwalimu, anaweza kwenda kulala hotelini kwenye msiba wa baba yake?
Misiba ya kisasa haina haja ya kuambukizana kunguni mkuu , popote unaweza kulala cha msingi ni kufanikisha mazishi .
 
Alain Kiluvia mbona hakuna andiko ulikotajwa katajwa Jack Gotham na Membe kwanini isiwe na wewe kuwa unatumika kuwachafua hao uliowaandika hapo? Kwahiyo issues za Membe na Gotham wewe ndo msemaji wai? Ningeshaanga Kama ungekubali
 
Apson, membe, Jack ghotam, lowasa, bashe hawa ni nani kama siyo CCM? chekeni tu kufanyana hv mkidhani ni mnamkomoa mtu mmoja, ngoja mwakani tupoteze nchi ndo mtafunga midomo yenu nyie wote.
 
''Asitake tuongee ambayo yamebaki kuwa siri kwa nia ya kuepuka mivurugano ndani ya chama na serikali''
Dah hii nchi sasa.......Kuna watu wanaweza kuvuruga hadi Serikali?!!!!

2015 ipite salama maana......

Mkuu umetoa hoja nzito sana na hakika maneno kama haya yanaonyesha Tanzania kama taifa ilivyofika pabaya. Hakika aliyetufikisha hapa kuna siku historia itamhukumu. Eti kuepuka mivurugano ndani ya chama na serikali. Yaani tumefikia mahali kama taifa tunaendeshwa na mtu au watu, yaani si kwamba kuna taratibu, kanuni, miongozo na sheria. Aisee!!!!!
 
Ni kawaida MCHAWI akikaribia kukata roho,uwataja wachawi wenzie na watu aliowaua.Naona shughuli ya 'RIP' inaanza sasa
 

Utanishawishi vipi kwamba hata wewe haujaleta huu uzi kwa maslahi yako binafsi na hao unaowatetea? Yaani badala ya kuangalia maslahi ya umma unalinda uozo kwa ajili ya chama?
 

umejichanganya sana mkuu, nchi hii tunataka watu wanaoweza kusema ukweli bila ya hofu wala vitisho. Tunachotaka useme unachojua ambacho Apson amefanya, si kuleta mikwara ya kizamani kuwa ukifanya hivi mimi nitafanya vile. Hizo siasa zenu sijui nani anachafuliwa hazina tija kwa wananchi
 

Mkuu, inasikitisha maana hatima ya Taifa letu sasa ipo mikononi mwa watu kadhaa ....Kuna ombwe la kutawala, makundi yenye maslahi binafsi.

Tunakelekea kama hali itakuwa hivi ni hatari zaidi
 
Nimeshangaa sana hiyo propaganda nyepesi dhidi ya Membe kwenye sakata hili
BEN..
Hili sakata ni kama gharika. kila aliyepitiwa na mkondo lazima atasombwa. kuna kila dalili wenye nguvu wanataka kuwasukumia kwenye mkondo hata wale wasiohusika.
LET IT HAPPEN huenda kile kikundi kidogo kinachohodhi nyanja zote za maisha ya watanzania kikawa kinaenda kuteketea na hatimaye hata vyama vya siasa including CCM vitaacha kuwa maficho ya maharamia
 
Siasa za uraisi zitaivuruga tanzania na hili ni kutokana fedha nyingi zinazotumiwa na wagombea kununua vibaraka ambao bila kutazama ubora wa mgombea wao wanajali maslahi yao hivi nchi ikivurugika nyuso zenu mtaziweka wapi kwa uroho wenu wa pesa.
 
Hivi karibuni pamekuwa na taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya jamii eti mhe. waziri membe nae amepewa mgao wa fedha za escrow na kwamba atawatumia wabunge wa upinzani kuiangusha serikali.

Taarifa hizo ni za uongo.watu wanaomfahamu waziri membe watakubaliana nami kuwa waziri membe anachukia ufisadi na rushwa. Ni mmoja wa mawaziri wa serikali hii ambao wapo mstari wa mbele kupiga vita ufisadi na rushwa.

Haogopi wala kumung'unya maneno kwenye suala hilo.huenda hali hiyo ndio imepelekea mahasimu wake wa kisiasa kuanza kumzushia uongo. Lakini bahati nzuri watanzania wanamjua fisadi mkubwa wa tanzania ni nani. Pia bahati nzuri ingine ni kwamba wezi wote wa escrow watajulikana siku chache zijazo. Kwa hiyo hao wanaolipwa kufanya hivyo waache kuzusha uchafu wao.

Suala la mhe membe kushirikuana na wabunge wapinzani kuiangusha serikali linachekesha kweli. Afanye hivyo ili nini? Kwa maslahi ya nani? Yeye ni sehemu ya baraza la mawaziri sasa serikali ikivunjika atapata faida gani? Uongo mwingine jamani hauna mantiki.

Mwisho nikiwa kama mtanzania mwenye uchungu na fedha za umma naomba wote tusiyumbishwe na ujinga wa aina hii,ujinga wa kuhusisha watu wasiohusika ili kuwatoa watanzania kwenye jambo hili kubwa lenye maslahi kwa nchi yetu.

Tuungane kuhakikisha wote waluohusika na wizi wa fedha za escrow wanawajibishwa na kuchukuliwa hatua za kisheria. Mungu ibariki tanzania.
 
Membe ni mhuni amediriki kutoa siri za baraza la mawaziri, je uadilifu wake katika kula kiapo kiko wapi?......Baada ya kula mgao mdogo akaamua kuwageuka wenzake.....Ila it is true Membe kala ele na ndio zimetumika kununua helcopter ambayo Diallo anaitumia kule kanda ya ziwa
 
Membe anajulikana kuwa ni adui wa mafisadi na ufisadi. Kwa hivyo sio ajabu hao wezi wa mali ya umma wakamzushia uongo. Bahati nzuri siku chache zijazo ukweli utajulikana.
Halafu mzee apson umeliibia sana taifa la tanzania.bado hujaridhika tu...una nyumba kila kona ya dunia..dubai, afrika kusini na uingereza. Au mpaka tuanike uchafu wako ndio utatulia?
 

Wewe ni msemaji wa nani?
 
Malumbano kama haya yanadhihirisha kuwa ataechaguliwa na CCM kugombea Urais ndiye ataekuwa Rais.

Hata wapinzani jinsi wanavyochangia humu wanaamini hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…