Arab contractor wanakabidhi bwawa la umeme, watu elfu 11 wameshiriki kulijenga, ndio Mradi Mkubwa wa kiuhandisi kuwahi kutokea Tanzania

Arab contractor wanakabidhi bwawa la umeme, watu elfu 11 wameshiriki kulijenga, ndio Mradi Mkubwa wa kiuhandisi kuwahi kutokea Tanzania

Sawa mkuu. Hapo nimeelewa

Sasa tuje kwenye data kwa mujibu wa taarifa za mleta mada

Watu 11,856
Person - Hours 72,000,000 ÷ Watu 11,855 = Masaa 6,072

Kwa hiyo masaa halisi ni 6,072.

Masaa 24 = Siku 1
Masaa 6,072 = Siku ngapi?
6,072 ÷24 = siku 253

Kwa hiyo kwa siku 253, ikiwa wafanyakazi 11856 walifanya kazi masaa 24 kila siku, kwa siku 253 jumla ya hizo person hours ni 71,989,682.

mkuu hesabu hazifanyikagi kwa urahisi kama ulivyofanya. ndio maana wanaofaulu hisabati ni wachache

hao watu elfu 11 hawakufanya kazi wote sawa sawa kwa pamoja, hivyo sio sahihi kugawanya moja kwa moja kama ulivyofanya.

kwenye hesabu kuna stages ndio maana mtoto wa form one afundishwi intergration,,

engineering inafanywa kwa hesabu zake yaani engineering mathematics. na ili uelewe engineering mathematics lazima kwanza uwe umeshajua Advanced mathematics.
 
mnakosea jinsi ya ku calculate hizo 72 milion hours.

Maana ya PERSON-HOUR ni kipimo cha saa moja ya kazi inayofanywa na mtu mmoja.

Person-hour Definition & Meaning

The meaning of PERSON-HOUR is a unit of one hour's work by one person.

sasa chukua hao wafanyakazi elfu 11 kisha jumlisha masaa yao yote waliyofanyia kazi kila mmoja kwa miaka ya kazi, uone total utapata masaa mangapi
Mmeamua kujadili masaa badala ya mradi!!
 
mkuu hesabu hazifanyikagi kwa urahisi kama ulivyofanya. ndio maana wanaofaulu hisabati ni wachache

hao watu elfu 11 hawakufanya kazi wote sawa sawa kwa pamoja, hivyo sio sahihi kugawanya moja kwa moja kama ulivyofanya.

kwenye hesabu kuna stages ndio maana mtoto wa form one afundishwi intergration,,

engineering inafanywa kwa hesabu zake yaani engineering mathematics. na ili uelewe engineering mathematics lazima kwanza uwe umeshajua Advanced mathematics.
Ni kweli aisee. Hesabu sio rahisi, kwa hiyo hazina namna rahisi ya kuzieleza ili wasiojua hesabu waelewe.

Mwaka 2006 wakati wa mgomo pale Njombe Secondary kuna mwalimu mmoja mgeni alipigwa mabanzi na wanafunzi wa PGM, PCM na PCB kisa tu anafundisha Physics. Jamaa wakasema inakuaje unafundisha somo gumu, ambalo tunafeli daily, wakampiga makofi.

Na mwaka huohuo, Dk. K wa mapacha akafanya verse kwenye ngoma moja, akisema ana sura ngumu mithili ya somo la physics.
 
Sina kumbukumbu vzr Ila nakumbuka N.Wazir dotto biteko kama alifungua baadhi ya mitambo lakini sio ya bwawa zima na ndomana hata thread hii imeanza kw mwandish kusema soon bwawa lotakabidhiwa Rasmi. Au sijaelewa sehem?
Kwani ndugu, kukabidhiwa ina maana kuwa ndio linaanza kazi rasmi!!???
 
Muda si mrefu kampuni ya ujenzi inakabidhi bwawa la umeme.

Ujenzi wa bwawa hilo ndio biggest engineering project kuwai kufanyika Tanzania na Africa mashariki yote.

1. idadi ya watu 11856 wamefika rufiji na kushiriki kulijenga

2. Raia wa mataifa 56 tofauti wamefika rufiji kushiriki kulijenga

3. Magari na equipment 1681 vimetumika kusaidia ujenzi

4. Masaa milioni 72 yametumika kwenye kazi ya kulijenga ( person- hours 72 milion hours)

5. Ndio mradi pekee ambao subcontractor tu, alikuwa anapewa kazi na kulipwa zaidi ya trilioni.

6. Ndio engineering project ilioleta mizigo mizito kuliko yote kuwai kufika africa mashariki. unakuta Mzigo mmoja tu una tani zaidi 200, sheria na kanuni za tanroads hawaruhusu kupitisha mizigo mizito sana barabarani ila kwenye bwawa walikaa kimyaa kama hawapo vile. Traffic wakiona gari limebeba mzigo wa bwawa tu hawaombi hata leseni ya dereva maana wanajua kibarua kitaota nyasi

7. ndio mradi pekee ulioonesha kwamba taasisi za serikali zinaweza kufanya kazi kwa spidi maana zilifanya kazi kwa spidi ya hali ya juu, bwawa lipo porini mbugani ila siku ambayo mkataba ulisainiwa, mkandarasi aliwaambia anataka akute maji safi site, umeme uwepo site, hospitali iwepo site

wizara ya maji ilitandika mabomba na kufikisha maji safi site kati kati ya pori fasta fasta wakati Dar tu kuna sehemu kibao maji safi hayajafika kwa miaka 60, tanesco nao walitandika nguzo za umeme na kufikisha umeme site fasta fasta, Tazara na yeye alifufua stesheni ya Fuga na kujenga kota za wafanyakazi wa tazara haraka haraka.

8. ndio mradi pekee ambayo serikali iliziba masikio kelele za wazungu, UN, UNESCO , WORLD BANK waliongea maneno yote ila hakuna kilichobadilika

screen shot kutoka website ya unesco 17 april 2020
View attachment 3237536
Umeme wa maji siyo wa kutegemewa mda si mrefu tutaona mgao Kwa kisingizio cha kina cha maji kimepungua,
 
Ni sababu nzuri, nakubali.

Watumiaji walioungwa kwenye mfumo walikuwa ni wengi kuliko uzalishaji, hii ndio ilikuwa hoja nambari moja.

Wakati huo miundombinu ilikuaje?
Transmission lines, una maanisha grid sio?
  • Ina maana tuliamua kujenga Power Plant ya 2.115GW tukitegemea transmission line iliyopo?
  • Msongo wa kilovolts ngapi unasafirishwa kutoka Bwawani? 400 au 220?
  • Tanesco walikuwa na mpango wa kusambaza umeme kupitia 33kV/0.4kV badala ya 11kV/0.4kV, walitekeleza hili?

Kama walifanikisha, sioni shida inatokea wapi, maana unapofanya maboresho ni lazima uzingatie future.

Hivi, substation za kupooza kutoka njia kuu, huwa zinajengwa kila mkoa au wilaya? Najua Dar zipo kadhaa, mikoani ikoje?
- Hakuna namna kukawa na substation ya mkoa, kama ni ya zamani, ikaboreshwa/upgraded kupokea umeme mkubwa na kusambaza kwingineko kwa ku-cover eneo lote la mkoa?

Kama mikoa yote haijaungwa kwenye grid, hiyo ni changamoto! Na ndio maana Grid huwa inaanguka mara kwa mara, maana grid sio ringi...mwaka jana mwishoni, imepiga chini mara kadhaa.
Kama nchi haikutumii wewe ndugu Ndalilo , tunapata hasara sana.
Ubarikiwe.
 
Sawa mkuu. Hapo nimeelewa

Sasa tuje kwenye data kwa mujibu wa taarifa za mleta mada

Watu 11,856
Person - Hours 72,000,000 ÷ Watu 11,855 = Masaa 6,072

Kwa hiyo masaa halisi ni 6,072.

Masaa 24 = Siku 1
Masaa 6,072 = Siku ngapi?
6,072 ÷24 = siku 253

Kwa hiyo kwa siku 253, ikiwa wafanyakazi 11856 walifanya kazi masaa 24 kila siku, kwa siku 253 jumla ya hizo person hours ni 71,989,682.
Kuna binadamu anaweza kufanya kazi 24hrs kwa siku 250+?
 
Likiwa full capacity ndiyo bwawa lenye kuzalisha umeme mwingi zaidi kwenye ukanda wa SADC. Litakalolipita lipo kwenye ujenzi Angola.
 
Muda si mrefu kampuni ya ujenzi inakabidhi bwawa la umeme.

Ujenzi wa bwawa hilo ndio biggest engineering project kuwai kufanyika Tanzania na Africa mashariki yote.

1. idadi ya watu 11856 wamefika rufiji na kushiriki kulijenga

2. Raia wa mataifa 56 tofauti wamefika rufiji kushiriki kulijenga

3. Magari na equipment 1681 vimetumika kusaidia ujenzi

4. Masaa milioni 72 yametumika kwenye kazi ya kulijenga ( person- hours 72 milion hours)

5. Ndio mradi pekee ambao subcontractor tu, alikuwa anapewa kazi na kulipwa zaidi ya trilioni.

6. Ndio engineering project ilioleta mizigo mizito kuliko yote kuwai kufika africa mashariki. unakuta Mzigo mmoja tu una tani zaidi 200, sheria na kanuni za tanroads hawaruhusu kupitisha mizigo mizito sana barabarani ila kwenye bwawa walikaa kimyaa kama hawapo vile. Traffic wakiona gari limebeba mzigo wa bwawa tu hawaombi hata leseni ya dereva maana wanajua kibarua kitaota nyasi

7. ndio mradi pekee ulioonesha kwamba taasisi za serikali zinaweza kufanya kazi kwa spidi maana zilifanya kazi kwa spidi ya hali ya juu, bwawa lipo porini mbugani ila siku ambayo mkataba ulisainiwa, mkandarasi aliwaambia anataka akute maji safi site, umeme uwepo site, hospitali iwepo site

wizara ya maji ilitandika mabomba na kufikisha maji safi site kati kati ya pori fasta fasta wakati Dar tu kuna sehemu kibao maji safi hayajafika kwa miaka 60, tanesco nao walitandika nguzo za umeme na kufikisha umeme site fasta fasta, Tazara na yeye alifufua stesheni ya Fuga na kujenga kota za wafanyakazi wa tazara haraka haraka.

8. ndio mradi pekee ambayo serikali iliziba masikio kelele za wazungu, UN, UNESCO , WORLD BANK waliongea maneno yote ila hakuna kilichobadilika

screen shot kutoka website ya unesco 17 april 2020
View attachment 3237536
CCM DAIMA SAMIA MITANO TENA
 
Mradi umekamilika lakini tulivyoahidiwa na magufuli wameshindwa kutimiza.kama gharama ya umeme haijapungua inakuwa hakuna faida ya huu mradi.Wananchi tulitegemea maisha yawe Mazuri Kwa kupunguza gharama za umeme lakini Hawa wachawi wa awamu ya sita ndiyo wameongeza mitozo ya kijingakijinga inayotuumiza.
 
  1. Wanakabidhi likiwa linayoa Megawatt ngapi?
  2. Je sile cracks walizosema ziliishia wapi?
  3. Je utaratibu wa kutembelea hilo bwawa ukoje?
  4. Je njia ya kufika huko inapita wapi na ni Km na masaa mangapi?
  5. Je mtu anaweza kupata accommodation akienda kutalii?
  6. Je ile mitambo ilishawashwa yote au tunatumia michache?
  7. Je sustaibability plan ipo na sheria za kulilinda bwawa zipi?
  8. Je ile gorge ilifutika au waliihifadhi kwa namna nyingine?
 
Umeme wa maji siyo wa kutegemewa mda si mrefu tutaona mgao Kwa kisingizio cha kina cha maji kimepungua,

Bei ya kuzalisha unit moja ya umeme wa maji ni nafuu sana.

Mfano gharama utakazotumia kuzalisha unit moja ya umeme wa gesi ukizitumia gharama hizo hizo kuzalisha umeme wa maji unapata unit 6 za umeme wa maji
 
Back
Top Bottom