Arab Contractors wakabidhiwa Billion 688.6 kama malipo ya awali mradi wa umeme wa maporomoko ya mto Rufiji

Lini tutafikiria nje ya sanduku !?
Kuharibu mazingira wakati kuna njia mbadala mf. Gas, jua,upepo n.k
 
Mkandarasi ujenzi Mradi wa Maporomoko ya Mto Rufiji Kampuni ya Arab Contractors ya nchini Misri imekabidhiwa hundi ya Bilioni 688.651 kama malipo ya awali kwa ajili ya kuanza kazi za ujenzi.

Hundi hiyo imekabidhiwa leo na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto James.

Akikabidhi hundi hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango amesema kwa hivi sasa nchi inajumla ya Mw 1602, hivyo kukamilika kwa mradi wa Rufiji kutaifanya nchi kuwa na umeme mwingi na wa uhakika.

Aliongeza mradi huu unagharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia mia moja.

"Malipo haya ya awali yataenda sambamba na malipo mengine ambapo jumla yake itakuwa shillingi tilioni 1 kwa ujumla" alisema Bw. James.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Dkt. Hamisi Mwinyimvua alisema malipo hayo ya awali ni sawa na asilimia 15.

Aliongeza, malipo yamegawanyika sehemu sehemu mbili asilimia 70 ya fedha za kigeni ambazo Amelia na asilimia 30 atalipwa baada ya kukamilisha shughuli za kimkataba.

Naye Mwenyekiti wa Bodi TANESCO Dkt. Alexander Kyaruzi kwa niaba ya TANESCO ameishukuru Serikali kwa kutekeleza mradi huo.

Hafla hiyo ilihudhuliwa pia na Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadilifu Mhandisi Innocent Luoga, Mkurugenzi Mtendaji TANESCO Dkt. Tito Mwinuka, Wakandarasi na baadhi ya wasimamizi wa Mradi wa Rufiji.
IMG_20190424_164341.jpeg
IMG_20190424_164325.jpeg
 
Halafu kuna watu wanamuombea Mabaya Rais wetu!

Kumchukia Magufuli ni kuchukia Taifa , ni kuchukia Maendeleo
 
aliombewa na kufanyiwa mabaya ghadafi aliye fanya haya huku akiwapa maish safii raia wake iwe huyu ambaye raia wanachakaa kila idara, anzia kipato, lishe na kiakili.

huyu niwa kuombea mabaya kila dk.
 
Trioni moja ya kitanzania? Aisee bora tungekomaa na gesi ya mtwara. That amount is very huge man.
 
Mkandarasi ujenzi Mradi wa Maporomoko ya Mto Rufiji Kampuni ya Arab Contractors ya nchini Misri imekabidhiwa hundi ya Bilioni 688.651 kama malipo ya awali kwa ajili ya kuanza kazi za ujenzi.

Hundi hiyo imekabidhiwa leo na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto James.

Akikabidhi hundi hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango amesema kwa hivi sasa nchi inajumla ya Mw 1602, hivyo kukamilika kwa mradi wa Rufiji kutaifanya nchi kuwa na umeme mwingi na wa uhakika.

Aliongeza mradi huu unagharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia mia moja.

"Malipo haya ya awali yataenda sambamba na malipo mengine ambapo jumla yake itakuwa shillingi tilioni 1 kwa ujumla" alisema Bw. James.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Dkt. Hamisi Mwinyimvua alisema malipo hayo ya awali ni sawa na asilimia 15.

Aliongeza, malipo yamegawanyika sehemu sehemu mbili asilimia 70 ya fedha za kigeni ambazo Amelia na asilimia 30 atalipwa baada ya kukamilisha shughuli za kimkataba.

Naye Mwenyekiti wa Bodi TANESCO Dkt. Alexander Kyaruzi kwa niaba ya TANESCO ameishukuru Serikali kwa kutekeleza mradi huo.

Hafla hiyo ilihudhuliwa pia na Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadilifu Mhandisi Innocent Luoga, Mkurugenzi Mtendaji TANESCO Dkt. Tito Mwinuka, Wakandarasi na baadhi ya wasimamizi wa Mradi wa Rufiji.View attachment 1079935View attachment 1079936
Hundi mwisho TZS 10 million tusidanganyane. Malipo makubwa hulipwa kwa bank transfer; tuwekeeni SWIFT ADVICE kama lengo ni sisi wananchi tujue mkandarasi amelipwa
 
Hongera wadau wote kwa hatua muhimu.Mungu baba atangulie yote.
 
Back
Top Bottom