Arab Contractors wakabidhiwa Billion 688.6 kama malipo ya awali mradi wa umeme wa maporomoko ya mto Rufiji

aliombewa na kufanyiwa mabaya ghadafi aliye fanya haya huku akiwapa maish safii raia wake iwe huyu ambaye raia wanachakaa kila idara, anzia kipato, lishe na kiakili.

huyu niwa kuombea mabaya kila dk.

Dua zako hazivuki urefu wa kimo chako ndio sababu Rais anaendelea kuchapa kazi
 
Miradi hii tutakuja kuichunguza maana ripoti za CAG awamu hii zinaashiria mengi yasiyofaa.

Na huu mradi tunasubiri uhamishiwe ofisi ile ambayo matumizi yake hayakaguliwa ila hii ni kinga ya muda tu.
Nyinyi wachawi tu, ndio wale wale hazai hazai wakati tumbo mnaliona likiongezeka ukubwa kila kukicha.

Akija kujifungua mnaanza uchawi mwingine kwa kusema mtoto hataweza kukua, miaka ikizidi kwenda anakua na kumaliza masomo vizuri tu.
 
Dua zako hazivuki urefu wa kimo chako ndio sababu Rais anaendelea kuchapa kazi
zivuke mara 2, humuoni anavyo boronga anzia yeye hadi walio chini yake. uchumi chaliiii na takwimu zake za kukuta sukari 5000 akaishusha hadi 1000.

unataka dua ifanye kazi vp?
 
Mungu ambariki Rais Wetu,katika maisha yangu nimepata kusikia fedha za nchi yetu zikikwapuliwa kiujanja ujanja lakini ukifuatilia katika utawala huu maendeleo yanaenda kwa kasi sana;Nimetembea sehemu kubwa ya nchi nimeona barabara zikijegwa karibu kila mkoa,Zahanati ndo usiseme tumuunge mkono Rais wetu,nilitembea nchi flani wanamuhitaji Rais wetu japo kwa wiki moja awe Rais wao.
 
Kwa hiyo Sukari ikipanda bei kutoka 200-5000 anakomoka Rais?, uchumi ukianguka anakomoka Rais?, jifanyie tathmini huenda Dua zako zimeharibu akili zako
 
Sijui nani katuroga.
Wengine tunawaza t. 1.5 na t.4 zimetumika vipi, wengine wanasifia t. 0.688, 06?
Safari hii ni viva wajinga, mnaonekana sana kwa awamu hii. Yaani awamu hii umetufanya tuwadharau hata wenye bonge na cheti cha elimu.
We unayewaza kitu ambacho hata kwenye report ya CAG hakipo utakua mpumbavu kiwango cha SGR. Sisi tunawaza kile tunachokiona na tumeona serikali imeanza kutekeleza mradi wa rufiji. We baki na zito mnakarrshana 1.5,4 mara 8T.
 
Kwa hiyo Sukari ikipanda bei kutoka 200-5000 anakomoka Rais?, uchumi ukianguka anakomoka Rais?, jifanyie tathmini huenda Dua zako zimeharibu akili zako
wapi nimekwambia anaye komoleka ni raisi (ambaye anakula na kulala bure) nilicho kwambia kwa kifupi huyu inafaa aombewe mabaya azidi kushindwa (maana kasha shindwa mpaka sasa) ili 2020 tufanye maamuzi sahihi ya kumpiga chini.

naona unajitengenezea maswali na majibu yako ili kujifariji nawe ni GT
 
Mungu ambariki Rais Wetu,katika maisha yangu nimepata kusikia fedha za nchi yetu zikikwapuliwa kiujanja ujanja lakini ukifuatilia katika utawala huu maendeleo yanaenda kwa kasi sana;Nimetembea sehemu kubwa ya nchi nimeona barabara zikijegwa karibu kila mkoa,Zahanati ndo usiseme tumuunge mkono Rais wetu,nilitembea nchi flani wanamuhitaji Rais wetu japo kwa wiki moja awe Rais wao.
kazi ya kujenga barabara mkapa na jk. walisha maliza ilibaki mikoa michache kama tbr-ktv, kgm-ktv,tbr-kgm huyu anaweka viraka tu
 
Hundi mwisho TZS 10 million tusidanganyane. Malipo makubwa hulipwa kwa bank transfer; tuwekeeni SWIFT ADVICE kama lengo ni sisi wananchi tujue mkandarasi amelipwa
Duu kizazi cha Tomasso hichi
 
Kwakuwa hamtaki kuamini kila kitu na mioyo yenu migumu kama ya Tomaso basi tutakuwa tunaweka na ushaidi humu mpaka muelewe tu.
 
Kitendo cha shughuli zote kufanywa na hao waarabu kwa 100% bila hata kutoa "Sub-Contract" kwa local contractors kinadhihirisha wazi kuwa fedha za ujenzi zinatoka Misri ila kama ilivyo ada serikali haipendi ifahamike hivyo.
 
Serikali yakabidhi mfano wa hundi ya shilingi bilioni 688.6 kwa kampuni ya Arab Contractor kwa ajili ya kuanza ujenzi wa mradi wa umeme wa maporomoko ya maji ya mto Rufiji.

Mkandarasi ujenzi Mradi wa Maporomoko ya Mto Rufiji Kampuni ya Arab Contractors ya nchini Misri imekabidhiwa hundi ya Bilioni 688.651 kama malipo ya awali kwa ajili ya kuanza kazi za ujenzi.

Hundi hiyo imekabidhiwa leo na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto James.

Akikabidhi hundi hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango amesema kwa hivi sasa nchi inajumla ya Mw 1602, hivyo kukamilika kwa mradi wa Rufiji kutaifanya nchi kuwa na umeme mwingi na wa uhakika.

Aliongeza mradi huu unagharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia mia moja.

"Malipo haya ya awali yataenda sambamba na malipo mengine ambapo jumla yake itakuwa shillingi tilioni 1 kwa ujumla" alisema Bw. James.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Dkt. Hamisi Mwinyimvua alisema malipo hayo ya awali ni sawa na asilimia 15.

Aliongeza, malipo yamegawanyika sehemu sehemu mbili asilimia 70 ya fedha za kigeni ambazo Amelia na asilimia 30 atalipwa baada ya kukamilisha shughuli za kimkataba.

Naye Mwenyekiti wa Bodi TANESCO Dkt. Alexander Kyaruzi kwa niaba ya TANESCO ameishukuru Serikali kwa kutekeleza mradi huo.

Hafla hiyo ilihudhuliwa pia na Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadilifu Mhandisi Innocent Luoga, Mkurugenzi Mtendaji TANESCO Dkt. Tito Mwinuka, Wakandarasi na baadhi ya wasimamizi wa Mradi wa Rufiji.
View attachment 1079865
Hao wahuni hiyo hela wanaenda kuwekeza huko Uganda wanajenga kiwanda cha kutengeneza tranforma
 
Cc: chige
 
Miradi hii tutakuja kuichunguza maana ripoti za CAG awamu hii zinaashiria mengi yasiyofaa.

Na huu mradi tunasubiri uhamishiwe ofisi ile ambayo matumizi yake hayakaguliwa ila hii ni kinga ya muda tu.
Ka vipi Jinyonge ka Mkubwa
 
kama huu mradi tuna ujenga kwa pesa za ndani...hongera zimuendee mheshimiwa raisi wa jamhuri yetu pendwa
 
Back
Top Bottom