Arab Contractors wakabidhiwa Billion 688.6 kama malipo ya awali mradi wa umeme wa maporomoko ya mto Rufiji

Arab Contractors wakabidhiwa Billion 688.6 kama malipo ya awali mradi wa umeme wa maporomoko ya mto Rufiji

Serikali yakabidhi mfano wa hundi ya shilingi bilioni 688.6 kwa kampuni ya Arab Contractor kwa ajili ya kuanza ujenzi wa mradi wa umeme wa maporomoko ya maji ya mto Rufiji.

Mkandarasi ujenzi Mradi wa Maporomoko ya Mto Rufiji Kampuni ya Arab Contractors ya nchini Misri imekabidhiwa hundi ya Bilioni 688.651 kama malipo ya awali kwa ajili ya kuanza kazi za ujenzi.

Hundi hiyo imekabidhiwa leo na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto James.

Akikabidhi hundi hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango amesema kwa hivi sasa nchi inajumla ya Mw 1602, hivyo kukamilika kwa mradi wa Rufiji kutaifanya nchi kuwa na umeme mwingi na wa uhakika.

Aliongeza mradi huu unagharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia mia moja.

"Malipo haya ya awali yataenda sambamba na malipo mengine ambapo jumla yake itakuwa shillingi tilioni 1 kwa ujumla" alisema Bw. James.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Dkt. Hamisi Mwinyimvua alisema malipo hayo ya awali ni sawa na asilimia 15.

Aliongeza, malipo yamegawanyika sehemu sehemu mbili asilimia 70 ya fedha za kigeni ambazo Amelia na asilimia 30 atalipwa baada ya kukamilisha shughuli za kimkataba.

Naye Mwenyekiti wa Bodi TANESCO Dkt. Alexander Kyaruzi kwa niaba ya TANESCO ameishukuru Serikali kwa kutekeleza mradi huo.

Hafla hiyo ilihudhuliwa pia na Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadilifu Mhandisi Innocent Luoga, Mkurugenzi Mtendaji TANESCO Dkt. Tito Mwinuka, Wakandarasi na baadhi ya wasimamizi wa Mradi wa Rufiji.
View attachment 1079865

Hata kama mmeamua kutafuta sifa muwe na kumbukumbu, rais wakati anamtangaza mzabuni wa huo miradi alisema huo mradi ni wa shilingi 6.5t na ni fedha za mkopo. Leo mkisema mmetoa 600b+ na ni miradi wa fedha za ndani kwa 100% ni kama mnadhani sisi ni watoto.
 
Lini tutafikiria nje ya sanduku !?
Kuharibu mazingira wakati kuna njia mbadala mf. Gas, jua,upepo n.k
Lkn jaman si tuliambiwa gas ya mtwara ndio mwisho wa matatizo yote tanzania? bidhaa viwandan itashuka, umeme utakuwa wa uhakika sasa inakuwaje tena tunavamia mradi mwingine??
 
1080381

Mkandarasi ujenzi Mradi wa Maporomoko ya Mto Rufiji Kampuni ya Arab Contractors ya nchini Misri imekabidhiwa hundi ya Bilioni 688.651 kama malipo ya awali kwa ajili ya kuanza kazi za ujenzi. Hundi hiyo imekabidhiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto James.
1080383

Akikabidhi hundi hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James amesema kwa hivi sasa nchi inajumla ya Mw 1602, hivyo kukamilika kwa mradi wa Rufiji kutaifanya nchi kuwa na umeme mwingi na wa uhakika. Aliongeza mradi huu unagharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
 
Magufuli ataacha alama ya mambo yanayoonekana japo uhuru wa watu hakuna kwa muda huu
 
Watumishi mpoo?? tujiandae kwa maumivu zaaidiiiii..........
 
mwaka jana waziri mkuu alisema wametoa 700bl ila mwaka jana awakutoa mapicha kama haya ya mwaka huu,
 
Magufuli ataacha alama ya mambo yanayoonekana japo uhuru wa watu hakuna kwa muda huu
Pierre Issa naye aliacha historia 1998 kwenye kombe la dunia kwa kufunga goli la 1600 tangu kuanzishwa kwa michuano hiyo. Lakini bahati mbaya sana, alifunga golini kwake.

Tumuombe Mungu goli unalolizungumzia hapa liwe lenye manufaa kwa timu yetu na si sifa kwa 'Pierre Issa'
 
Aisee, sisi tuna hela sana kumbe tunaweza kua Dona kantri.
 
Hongera kwa serikali ya awamu ya tano kwa kuanza mradi mkubwa wa umeme hii itakuwa ni suluhuhisho la uhaba wa nishati ya umeme nchini. VIVA MAGUFULI
 
Nimesikia malipo haya ni 70% ya malipo yote na wametakiwa kukamilisha kazi kwa wakati.
 
mkuu
Na akili yako ilivyo finyu ikabeba hiyo pumba kama ilivyo? Kuna mradi unaopingwa na hao "West" kama huu? Kivipi sasa hata serikali ifikirie kuomba mkopo {actually not donation go back to school} kutoka kwao?
mkuu umekua psychologist kupima upana na ufinyu wa akili ya mtu? anayway nilitarajia ukanushe hilo na unielemishe ila kwa sababu ya ufinyu wa akili yako ukaona unishambulie personally!! kuna tofauti ya donation na loan you better go back to school and learn that hata SGR tumekopa ndio mana deni la taifa bado linakua na Mkulu anajitetea kwamba kukopa sio dhambi!
 
Lkn jaman si tuliambiwa gas ya mtwara ndio mwisho wa matatizo yote tanzania? bidhaa viwandan itashuka, umeme utakuwa wa uhakika sasa inakuwaje tena tunavamia mradi mwingine??
Mkuu kila zama na kitabu chake, nchi imekosa consistence, Jana Hakielimu wameweka wazi utafiti wao kuwa bajeti ya elimu inashuka kwa 1% kila mwaka huku idadi ya wanafunzi ikiongezeka kila mwaka. Lazima ujue kuwa jamaa anataka kuacha tangible structures at any cost whether zitanufaisha watu au la hajali. Madeni haya tutayabeba sisi na wajukuu wetu. Tatizo ni wakati wa kampeni tulikua tukimuonesha mapicha ya huko Ethiopia na Kenya zilivyofanikiwa katika miundo mbinu. Kwahiyo anataka kuacha alama kwa jasho na damu!!
 
Miradi hii tutakuja kuichunguza maana ripoti za CAG awamu hii zinaashiria mengi yasiyofaa.

Na huu mradi tunasubiri uhamishiwe ofisi ile ambayo matumizi yake hayakaguliwa ila hii ni kinga ya muda tu.
1. Nini maana ya "hundi ya mfano" na ina umuhimu gani?
2. a. Engineering Consultant wa mradi huu ni nani?
b. Gharama zake ni kiasi gani?
3. a. Nimesikia tanroads inahusika katika usimamizi (consultant) wa mradi huu. Ni kweli?
b. Kama ni kweli nauliza ' vipi tanroads wawe consultant wa project kubwa kama hii ambayo ni ya kwanza nchini kwa scope, wana uzoefu gani na miradi ya aina hii?
4. Tarehe za kuanza na kukamilika kwa mradi ni zipi kwasababu miradi ya aina hii hukamiluka baada ya muda mrefu pengine hata miaka 10+. Na si ajabu gharama za ujenzi kuongezeka. Hasa ikiwa kuna uharaka usio wa kawaida.
 
Back
Top Bottom