Ardhi Haikupi sio tu Mafanikio, Inaweza Kukupa Utajiri wa Ghafla

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
25,030
Reaction score
61,298
Kuna biashara ambazo zinakupa hela kidogo kidogo kila siku, lakini zipo biashara ambazo zinakaa kimya kwa muda mrefu halafu siku moja zinakushangaza kwa hela nyingi kwa mkupuo. Miongoni mwa biashara hizo ni ardhi, kilimo na madini. Unaweza ukahangaika miaka kadhaa bila kuona matokeo makubwa, lakini ikitokea umefanya dili sahihi unaweza kubadilisha maisha kwa siku moja.

Biashara ya ardhi ndiyo inayonivutia zaidi. Watu wengi wanaona udalali wa viwanja ni kazi ya kutwa nzima kupiga simu na kuzunguka bila mafanikio. Ukweli ni kwamba madalali wengi wanahangaika sana bila kupata dili kubwa. Lakini uzuri wa biashara hii ni kwamba unahitaji dili moja tu la maana. Ukakutana na mtu anauza kiwanja kizuri kwa bei nzuri, documents zikawa safi, halafu ukapata mnunuzi mwenye hela, unaweza kupiga cha juu ambacho mtu wa mshahara anaweza asikione kwa miaka kadhaa.

Ndiyo maana naona baadhi ya watu waliotoboa kwenye ardhi walikuwa na bahati ya kuifikia fursa kwa wakati sahihi. Mfano wa Scoba maarufu kama dalali mwanamke alipata mradi mkubwa Kigamboni. Alipopata fedha akaongeza uwekezaji na kuzungusha mtaji wake. Leo anaonekana kuishi maisha ya kitajiri kwa sababu aliwahi fursa ilipofika leo anatutukana anasema mwanaume hutakiwi kuendesha IST inatakiwa uendeshe discover..wengine ni dalali wa kimataifa,chief chilumba mtoto wa mjini wazee wa makumbusho mikocheni,kina Edo ana office pale palm village,wako ma madogo wanatikisa hawafahamiki dalali mzungu wa kigamboni,kuna hussein mtundu,kuna mtoto wa chief kiumbe hamadi kiumbe..hawa wote kwa sasa wako vizuri sana madili wanayoshika ni kuanzia million 50,100

Kilimo na madini hivohivo. utalima misimu mingi bila faida, halafu mwaka mmoja bei zipande au mavuno yawe bora unashika mamilioni. Vivyo hivyo kwenye madini, unaweza kutafuta kwa muda mrefu bila mafanikio makubwa, halafu ukapatikana mwamba mmoja ukabadilisha maisha.

Ndio maana naona biashara za ardhi, kilimo na madini zinafanana sehemu moja si biashara za kukupa hela kila siku, bali zina uwezo wa kukupa hela nyingi kwa mara moja. Tatizo ni kwamba wengi huona waliotoboa na kusahau maelfu waliojaribu na hawakupata hilo zali. Ndiyo maana kwenye biashara hizi bahati, muda sahihi na maamuzi sahihi vyote vina nafasi kubwa
 
Huenda kwenda ardhi ni sawa, kilimo kitoe hapo hasa cha masikini labda kilimo wanachofanya matajiri akina mo, na madini hapo ni uhakika kabisa
 
Unaweza kuwa sahihi Kwa kisasi Fulani
 
Umesema kilimo?kilimo gani?peasant Agriculture?

Mbolea bei yake ni 140,000 lakini debe la mahindi ni tsh 10,000🤔
 
Back
Top Bottom