Ardhi Sports Club yashiriki ufunguzi wa Michezo ya 40 ya SHIMIWI Kilimanjaro

Wizara ya Ardhi

Govt Institution
Joined
May 14, 2024
Posts
306
Reaction score
165
5b32da7a-f77c-416d-abd1-a86c47cd562d.jpeg

Timu ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi (Sports Club) imeshiriki ufunguzi rasmi wa Michezo ya 40 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) ulioambatana na maandamano ya wanamichezo wote wanaoshiriki michuano hiyo mkoani Kilimanjaro.

Maandamano ya wanamichezo yamekuwa sehemu ya shughuli za ufunguzi wa mashindano hayo, yakishirikisha watumishi kutoka Wizara na idara mbalimbali za Serikali ikiwa ni ishara ya mwanzo wa ushindani katika michezo hiyo inayolenga kuimarisha afya, umoja, mshikamano na ushirikiano miongoni mwa watumishi wa umma.

Akifungua Michezo hiyo ya 40 ya SHIMIWI leo, Septemba 26, 2026, katika Viwanja vya Chuo cha Polisi Moshi, mkoani Kilimanjaro, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda (MB), amewataka watumishi wa umma kutumia michezo hiyo kama nyenzo ya kuimarisha umoja, mshikamano na ushirikiano katika utendaji kazi.

Amesema, kuimarika kwa mahusiano na mshikamano miongoni mwa watumishi kupitia michezo kutachangia kuongeza ufanisi katika kuwahudumia wananchi kwa uadilifu.

"Serikali itaendelea kuongeza thamani katika Mashindano ya SHIMIWI kwa kuongeza ari na hamasa kwa watumishi kushiriki kikamilifu katika michezo". Amesema mhe. Makonda

Ardhi Sports Club inashiriki mashindano hayo ya SHIMIWI ikiwa na dhamira ya kuwakilisha na kuitangaza vyema Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia michezo.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala (ADA) wa Wizara ya Ardhi Bw. Deodatus Mwiliko aliyemuwakilisha Katibu Mkuu (KM) katika hafla ya ufunguzi wa mashindano ya SHIMIWI 2026 amekutana na wanamichezo wa Ardhi Sports na kuwapongeza kwa ushiriki wao mzuri na kuwataka kuendelea kujituma wakati wote wa mashindano hayo.

Amewahimiza kuongeza bidii, nidhamu na mshikamano ili kuhakikisha wanapata mafanikio na kurejea na makombe huku akisisitiza kuwa mafanikio yatawezekana endapo kila mwanamichezo atatekeleza wajibu wake kwa kujituma na kuiwakilisha vyema wizara katika mashindano.
 
Je mlipelela jezi zenu kwa Makonda ili azipime kama ni nzuri?
 
Hongereni, naona perdiem + on transit + nauli zimeingia wakuu.
 
Back
Top Bottom