DOKEZO Ardhi Tabora wanapeana viwanja wao kwa wao na matajiri wanaojuana nao

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Prince05

Member
Joined
Feb 27, 2024
Posts
43
Reaction score
84
Huwezi amini wametangaza viwanja kwenye mfumo wa tausi kama kutimiza majukumu tu. Wametoa siku tano za preview. Viwanja vilitakiwa kuanza kununuliwa tarehe 5/06/2026 saa nne kamili asubuhi.

Nimekaa kwenye mfumo saa tatu na dakika 50 ili kuwahi kununua. Lakini saa 10:00 inafika papo hapo eti viwanja vyote 18 havipo viko sold ni kitu ambacho hakiwezekani. Na hii sio mara moja hata kwa mikoa mingine. Watumishi wananunua wanauza kwa bei kunwa nje ya mfumo.

Yaani sekunde 2 viwanja vimenunuliwa kwa pamoja?
IMG_6501.jpeg
 
Tabora na mapori yote hayo unalalamika viwanja vya kupima kwa miguu. je wa Dar na Arusha itakuwaje sasa

Huko ni kununua hekali na kuendelea By the way mambo ya mfumo huwezi jua viwanja 18 ni vichache sana na bei ya huko mtu mmoja anaweza chukua vitatu
 
Mapori yapo. Njoo nikupe hekari 5 za bure. Maendeleo yatafika baada ya miaka 80.
Issue ni michongo yao. Hivi ulishawi hata kununua kiwanja wewe? Ulishwahi kujua utaratibu wa tausi unavyofanya kazi? Ungekua unajua ungeelewa nachoongea ni UPIGAJI TU
 
Ulishwahi kujua utaratibu wa tausi unavyofanya kazi? Ungekua unajua ungeelewa nachoongea ni UPIGAJI TU
Kwa hio unafanyaje sasa wababe washachukua viwanja 18 wamevitia mfukoni unafanyaje au unawafanyaje? Fanya km ulibet tu mkeka umechanika soma pale wameandika "Grace Period"
 
Mapori yapo. Njoo nikupe hekari 5 za bure. Maendeleo yatafika baada ya miaka 80.
Issue ni michongo yao. Hivi ulishawi hata kununua kiwanja wewe? Ulishwahi kujua utaratibu wa tausi unavyofanya kazi? Ungekua unajua ungeelewa nachoongea ni UPIGAJI TU
Mkuu nina plot iliyopimwa Uledi karibu na walipojenga hospital ya wilaya na Stand. Ukubwa Sqm 313. Kama uko interested njoo nikuuzie, nimempa kazi dalali naona hayupo serious. Mimi siishi Tabora wala sina mpango, nilinunua bei chee kwa jamaa yangu aliyekuwa na shida ya kifedha.
 
Kias gan
 
Kufanikiwa kununua kiwanja kwa huo mfumo wa tausi ngumu mzee,hapo ni uhuni,rushwa na kujuana ndiyo kunafanya kazi,
Geita pia walitangaza viwanja eneo la buhalahala wakaweka mda wa kuanza manunuzi hiyo saa 4 asubuhi ilipofika huo mda hakuna kiwanja hata kimoja vyote vimeuzwa
 
Kiukweli sijapanga bei, nilikinunua mwaka 2021 na sijawah kukitembelea tangu kipindi hiko. Nilimtuma dalali akakiangalie alafu anifanyie tathmini ya bei, ndio nimekwama hapo, dalali na mtu anayejua kiwanja kilipo wanazumgushana tu kwenda kuoneshana huu mwezi wa saba. Mimi niliuziwa na mshikaji wangu kwa milion moja tu, biashara ya kirafiki.
 
Hapo una hati au una nn?
 
Moja Ya Idara Mbovu Kuwahi Kuwepo
Wanapeana Ujinga Tangu Viongozi Wa Juu Wajichotee Ardhi, Nyumba Imekuwa Ndiyo Sheria Yao
 
Hapo una hati au una nn?
Nina mkataba wa mauziano, ila tulivyofanya, mimi nilinunua kwa rafiki angu, yeye aliuziwa na dada mmoja wa huko Tabora bila maandishi, wakati tunasainishana mkataba viongozi wa serikali za mtaa walishauri sababu hakuna maandishi kati ya yule dada na rafiki angu basi mkataba usomeke yule dada ndio kaniuzia, tulifanya hivyo. Then nikaenda Ardhi plan ambayo ndio kampuni iliyopima na kuuza hivyo viwanja tukabadili umiliki kutoka kwa yule dada kuja kwangu. Hatua iliyobaki ilikuwa ni ya kufuatilia hati, sikufanya hivyo sababu naishi mkoa wa mbali, wala sijawahi kutembelea hilo eneo, nina jamaa yangu yupo huko ndio huwa anatembelea.
 
Kiko mtaa gani ?
 
Pole,ujumbe wameupata japo hii nchi imeoza kwa rushwa na ufisadi
 
Huwezi amini wametangaza viwanja kwenye mfumo wa tausi kama kutimiza majukumu tu. Wametoa siku tano za preview. Viwanja vilitakiwa kuanza kununuliwa tarehe 5/06/2026 saa nne kamili asubuhi.

Nimekaa kwenye mfumo saa tatu na dakika 50 ili kuwahi kununua. Lakini saa 10:00 inafika papo hapo eti viwanja vyote 18 havipo viko sold ni kitu ambacho hakiwezekani. Na hii sio mara moja hata kwa mikoa mingine. Watumishi wananunua wanauza kwa bei kunwa nje ya mfumo.

Yaani sekunde 2 viwanja vimenunuliwa kwa pamoja?
View attachment 3601487
Mwenye nguvu mwite POWER.
 
Back
Top Bottom