katika bandiko langu nilijaribu kugusia kidogo sana juu a mambo mihimu yanayohitajika kwa watu wa aina hiyo wanaoongelewa kwenye mada....katika kuzisoma umeona kuwa kwa hali ilivyo huko Tanzania hakuna anayeweza kufaa na sababu kubw auliyoongelea ni mabadiliko ya kimaadili yanayoletwa na utandawazi kuwa yanaathiri kwa kiasi kikubwa zoezi zima la upatikanaji wa watu hawa.
yawezekana hoja yako ni ya msingi lakini nipende kukwambia kuwa huko nyumbani kuna vijana wake kwa waume wengi ambao vichwa vyao havijachafuliwa na mambo hayo lakini pia mabadiliko ya kiteknolojia sio sababu ya msingi sana maana jasusi yoyote lazima ajue matumiz ya technolojia mbali mbaliili aweze kufanya kazi zake kwa ufasaha. siku hizi haihitaji mtu kutembe na AK47 mtu anaweza kutembea na ki-USB flash disk kidogo tu ambacho kiknaweza kuwa na madhara makubwa sana katika jamii.
pengine niseme kuwa wapo watu wengi sana vichwa vyao havina uchafu mwingi na wanafiti katika eneo flani kulingana na mahitaji...huko juu kwenye bandiko langu nilisema wanahitajika watu wa aina mbali mbali kulingana na mahitaji yaliyopo...
sasa hizo ulizoita criteria naomba nikwambie kuwa kila mtu anao uwezo huo wa kila moja wapo hapo juu isipokuwa namna ya kuzitumia... uelewa wa mambo ni jambo la msingi sana...kuna wakati flani huko nikiw ahuko nyumbani nilimuuliza kijana mmoja kwamba..ili kijiji kiwe kijiji ni hatua zipi zinachukuliwa mpaka eneo flani linaitwa kijiji, na pia katika kijiji kuna safu zipi za uongozi.... kijana yule alishindwa kunijibu swali liel akabaki kurukia rukia vitu vya ajabu ...sasa swali kama hili haliihitaji eti mabadiliko ya teknolojia ...bali ni upana wa uelewa wa mambo..ni swali dogo lakini kama hujui namna ya kujibu basi huwezi
ukija kwenye swala la kumbu kumbu..kila mtu anazo kumbukumbu za kiwango flan...wapo watu wanaoweza kutaja majina ya wenzao karibu 40 waliokuwa wanasoma shule ya msingi lakini hawezi kutaja majina ya marafik zake 5 aliosoma nao sekondari...nk nk nk.... naomba nikupe changamoto ukienda kwene mishuguliko yako ya siku ..na jioni ukirudi nyumbani hebu jaribu kuandika report yako ya sku nini umefanya, umekutana na nani...alivaa nini, mliongea nini, ulipita wapi ulkaona nini....kama kuna jambo utalisahau na ulilifanya kwa siku hiyo basi jua uwezo wa kukumbuka na umakini uwapo eneo flani ni kiasi...au nenda bar hata kama hunywi pombe agiza maji kisha ukiwa mle ndani angalia kuna watu wa aina gani, umesalimiana na nani humo ndani, kuna bar-maids wangapi walivaa nini, kaunta ikoje mle ndani watu walikaa vipi,,mtu wa upande upi alikuwa anavuta sigara, uliongea na nani na mliongea nini....kumbuka iwe ni bar yenye mziki na watu wanacheza...kisha rudi nyumbani tengeneza report ya kila kitu ulichoona mle ndani....hili nalo haliihitaji mabadiliko ya tabia nchi au technolojia bali ni aili ya mtu jinsi ilivyo tulia na uwezo wake kurekodi mambo na kutunza kumbukumbu....
Niliposoma post yako nikakumbuka jambo moja miaka mingi ya nyuma siku moja mimi na mdogo wangu tulichukuliwa na baba kwenda hadi katikati ya mji na kisha baba akanionyesha dirisha moja lililokuwa wazi kwenye jengo flani la gorofa , dirisha lilikuwa kwenye gorofa ya 4.baba akaniambia unaliona dirisha lile basi nenda mpaka pale ndani ya ile ofis na fanya ufanyavyo baad aya dakika saba ningependa sana kukuona kwenye balcony ya ofis hiyo ukiwa na mtu utakayemkuta humo ndani na hakikisha mkononi umeshikilia moja ya file utakalolikuta humo na ukikosa file basi ushike hata glasi ya maji mkononi uwe unakunywa......piga picha ungekuwa ni wewe hatua zipi ungechuku na ungeanzia wapi hadi kufanikisha swala hilo ndani ya dakika saba?...mdogo wangu yeye aliambia aene mpaka mapokezi aangalie ndani ya daftari la wageni jina la mwisho la mtu aliyejiandikisha na achukue na namba za simu alipewa dakika 4.....wewe ungeanzia wapi ?..na je unadhani mabadiliko ya technolojia yanachangia lolote juu ya kufanikisha hayo mawili tuliyoambiwa na baba mimi na mdogo wangu?....
kwa hiyo napenda nikwambie kuwa mabadiliko ya globalization hayaathiri upatikanaji wa watu hawa bali kwa namna flani yanasaidia kuweza kupata vijana wanaofaa..chini ya mchango wangu pale juu nimesema wanaochaguliwa ni the right person note necessarily the best one.....
nimalize kwa kuukuuliza swali hivi unadhani kusema uongo ni dhambi?...