Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna shule nzito sana hapa. Picked bunch of lessons. By the way, hivi intelijensia yetu ipo huru kiitikadi? Kwamba transition ya madaraka kutoka kundi la mrengo mmoja kwenda kwa jingine yaweza fanyika na loyalty ya idara isiyumbe? Najaribu kuangalia CIA kule USA (Republican vs Democrats) n.k
Mkuu wale jamaa kwa nchi za wenzetu huwa wanazaliwa wakiwa na baadhi ya attributes/tabia fulani hivi kisha wanaongezewa tradecraft/ujuzi wa kimafunzo...baada ya hapo weeee wanakuwa ni moto wa kuotea mbali...!
Hivi mishahara yao inakuaje?
Inatoka serikalini?
Wana Ac za bank?
Na huwa wanakwenda vp ofisini ili watu wengine wasiwaone?
Vipi kuhusu bodi yao, huwa wanatimiziwa kilakitu kias cha kwamba hakuna malumbano wala migomo ndani ya taasisi yao?
Na je, huwa wanaongelewa bungeni? Au matatizo yao wanayatatua kimya kimya? Mfano upungufu wa vifaa vya mawasiliano?
leo ni na ka nafasi kidogo na hivyo tunaweza kupeana mawili matatu baada ya kazi nzito ..
ndugu zangu kila mmoja amepewa karama yake na karama hizo zaweza kuwa moja au zaidi kutegemea na mtu mwenyewe anazitumia vipi karama hizo..Mungu amempa mwanadamu uwezo mkubwa sana katika ubongo na akili yake ili viwezi kumsaidia kufanya kile ambacho anaamini ...
Uchambuzi wa taarifa ni kitu ambach anakifanya kila mmoja wetu katika maisha ya kila siku ...na ni katika kuchambua taarifa hizo ndiko kunakotufanya/kufanya uwe kama ulivyo...sasa hili linakwenda sanjari na makuzi ya mtu na uwezo wake kwa ujumla...
hivyo hivyo hata katika kuchambua taarifa za kijasusi...si kila mtu anaweza kuchambua taarifa za kijasusi..hata kama yumo ndani ...
uchambuzi wa taarifa ni kitendo cha kutafsiri vipande vya taarifa zilizokusanywa katika muundo wowote na kuwa kitu kinachoweza kutumika kwa ajili y amanufaa ya jamii, jeshi, kwa kupitia kwa watunga sera (serikali)..taarifa zinapokusanywa na ''vijana'' ni lazima zipelekwe kwa wachambuzi ili kuzichambua na kuona ni namna gani ya kutatua tatizo...wachambuzi taarifa hizo ni lazima wawe wamebobea katka fani hiyo lakini pia ni lazima wasaidiwe na technolojia ili iwasaidie kufanya uchambuzi makini kwa ajili ya manufaa ya taifa zima..
Matukio mabaya yanaweza kulikumba taifa iwapo uchambuzi wa taarifa utafanywa pasipo kufata weledi wa taaluma na hvyo kuliingiza taifa kwenyr machafuko...zipo sababu zinazoeza kuliingiz taifa kwenye matatizo iwapoiwap wachambuzi hawatatumia weledi wa taaluma yao ipasavyo sababu hizo ni kama zifuatazo:
1.. kupuuzwa kwa taarifa
taarifa muhimu na zenye mashiko zinaweza kukusanywa na kuwakilishwa kwa ajili ya kufanyiwa uchambuzi lakini wachambuzi wakapuuza taarifa hizo kuzifanyia kazi na hivyo nchi ikaingia kwenye machafuka sababu kubwa ikawa ni kupuuzwa kwa taarifa muhimu
2.kukosea kucmabua taarifa na tafsiri yake (Misinterpretation)
hiyo ni sababu nyingine inayiweza kupelekea taifa kuingia kwenye machafuko..taarifa zinazokusanywa kama zizipofanyiwa uchambuzi wa kutosha na kutafsiriwa barabara basi tatizo la msingihalitatatuliwa..ili uchambuzi ufanyike sawasawa ni lazima wachambuzi watumie vifaa vya kisasa(technology) ili kurahisisha kazi..
3...kukusanya taarifa na kutoa majibu ili kukidhi haja ya watawala (subordination of intelligence to policy)
kama wachambuzi wa taarifa watafanya kazi yao na kutoa ripoti isiyoakisi ukweli ili kukidhi na kuwaridhisha wakubwa ni lazima taifa litaingia kwenye mgogoro.ni lazima wachambuz watoe majibu yanayoakisi ushaidi uliopo na sio kukidhi haja za watawala..na hili huwa ndilo kosa kubwa lilipelekea nchi nyingi kuingia kwenye machafuko
4..kukosekana kwa taarifa katika mda mwafaka na mahali sahihi..
hili nalo ni tatizo kubwa sana..taifa linaweza kuingia kwenye machafuko kwa sababutarifa sahihi hazipo zinapotakiwa kuwa kwa mda mwafaka..taarifa zinaweza kuwa kwenye moja ya idawa na idara hiyo isipeleke taarifa hizo kunakohusika..hii hutokana hasa palendnai ya idara kuna kugombania madaraka (kila idara inajiona iko juu) na hivyo idara yenye taarifa kutumia kigezo cha kuficha taarifa kama silaha juu ya idara nyingine..lakini pia inawezekana idara moja ikawa na taarifa lakini sijue wapi pa kuzipeleka yauchambuzi au idara inaweza kupuuza juu ya taarifa zilizopo..hili nalo ni tatizo maana kupuuzwa kwa taarifa hata kama ni kidogo kunaweza kuathiti uchambuzi na hivyo machafuko kutokea....
5... kufanya uchambuzi kwa kufananisha matukio( mirror-imaging)
tatizo hili ni kubwa ..kufikia hatua ya uchambua taarifa kwaa misingi ya kufannanisha matukio ni jambo baya sana..kila taarifa ina uzito wake na hivyo inastahili kuchambuliwa kwa uzito wake na kutokufananishwa na matukio yaliyopita..kwa kufnaya hivyo taarif aya mwisho itakuwa haiakisi ukwlei na uhalisia ..
kushindwa kuchambua taarifa kwa kufananishwa matukio ni sababu kubwa ya kushindwa kuchambua taarifa za kiintelinjensia...
hizo ni baadi ya sababu zinazoweza kupelekea uchambuzi wa taarifa za kijasusi kwenda mrama..nadhani nimekidhi haja ya mmoja wa wanajukwaa aliyetaka kujua jambo hili lakini pia na wengine
Bila shaka wote mu wazima wa afya. kama heading inavyojielezea hapo juu ni swali nililokuwa nikijiuliza kwa muda mrefu sasa kama uwezo wa hawa watu huwa ni wa mafunzo au wanazaliwa wakiwa tayari na hizi attributes?
Ninawasilisha.
they are made...... Kitu chochote kinatokana na nguvu ya umakini... "popote unapoelekeza umakini wako panakua"..... Ukijua jinsi akili ya mwanadamu inavyofanya kazi utagundua kuwa spies can be made... hata wewe unaweza kujitengeneza mwenyewe ukawa spy
you are right...kuna maneno mwalimu wetu aliwahi kutwambia na na aliyapenda sana alikuwa akisema hivi '' when you control your thoughts you controlyour mind, when you control your mind you control your life, once you reach a stage of being in total control of your life you become the master of your own destine...umakini katika jambo lolote ni kitu cha muhimu sana...huko mwanzo nadhan page 4 ya mada hii nilisema hakuna anayezaliwa na kufiti kweye kazi flani pasipo kupitia mafunzo yoyote....
wakati tuko vijana mzee wetu alipenda ktufindisha vitu vingi sana wakati ule tuliona kama havifai hivi....mtaa tuliokuwa tukikaa ilikuwa ni maeneo ya watu wenye nafasi zao za kutosha nk..mzee wetu alikuwa akitwambia mimi na mdogo wangu ..siku moj akasema nataka mniambie ndani a ile nyumba ya tatu kuna watu wangapi wanaishi mle na mkadirie na umri nawapa wiki nzima...sasa ndani ya wiki moja tulikuwa tuna kazi hiyo ya kujua na alitwambia sitaki mwende pale mkaonekana na mkaulize haya niliyowambia tumieni akili zenu kujua ....
basi kwa kuwa ilikuwa ni kazi ilibidi tufanye..kufanyika kwake ilikuwa ni kuangalia hasa wakati wakifua nguo wakianika...zile nguo tuliweza kuziangalia na kuelewa ni nguo za aina gani...za watoto tulizona..za watu wazima tuliziona ...za watoto wa kike au kiume tulziona na pia a watu wazima...njia hii ilitusaidia kujua nyumba ile ina watu wangapi...na wa jinsia ipi....lakini pia tulikuwa tukienda kwenye pipa la kutupia taka kabla ya wahusika hawajaja kuchukua uchafu ule...tulikuwa tuna akusanya vijikaratasi..na hapa napenda niseme wazi kabisa watu wengi hawalijui hili hata huko maofisini..unakuta mtu karatasi ina bonge la siri anachofanya ni kuifinyanga finyanga kwa kiganja kisha aantupa kwenye dustbin...sasa sisi tuliweza kutumia njia hiyo ya kwenda kwenye ma dustbin na kuangalia vikaratas karatasi, chupa, mifuko , karatasi za benk (pay slip) nk .. na hvyo tulijua mtu flani anapenda kutumia kinywaji gani, ananunua wapi, benk ya yake ni ipi, na mambo mengine kama hayo...
yote hii ni kutaka kujua watu wanaokuzunguka ni wa aina gani na hivyo uishi nao vipi...yako mazoezi mengi sana hata tulipokwenda ''shambani ''meng tulifundishwa namna ya kumjua mtu hata kama hujawahi kumuona...namna ya kuangalia hata mwandiko na aina ya uandishi wa mtu na ..mwandiko ni njia moja wapo ya kujua tabia ya mtu....humu jf kwa kuwa hatuandiki kwa wino lakini unaweza kujua character ya mtu kutokana na uandishi wake...kwa mfano The Boss hawezi akaandika kama anavyoandika@lara 1..au anavyoandika Pasco ana tofauti kubwa na hao wengine ukifatilia michango yao yote na aina ya andishi wao waweza kujua ni watu wa aina gani...
jambo la msingi hapa ni kuelewa na kujielewa na kuwa makini kwa kila jambo...nguvu ya umakini ni muhimu sana...ni lazima utengenezwe kuwa spy nje ya hapo ni ngumu kufanikisha kazi kujitengeneza mwenyewe ni ngumu sana..