you are right...kuna maneno mwalimu wetu aliwahi kutwambia na na aliyapenda sana alikuwa akisema hivi '' when you control your thoughts you controlyour mind, when you control your mind you control your life, once you reach a stage of being in total control of your life you become the master of your own destine...umakini katika jambo lolote ni kitu cha muhimu sana...huko mwanzo nadhan page 4 ya mada hii nilisema hakuna anayezaliwa na kufiti kweye kazi flani pasipo kupitia mafunzo yoyote....
wakati tuko vijana mzee wetu alipenda ktufindisha vitu vingi sana wakati ule tuliona kama havifai hivi....mtaa tuliokuwa tukikaa ilikuwa ni maeneo ya watu wenye nafasi zao za kutosha nk..mzee wetu alikuwa akitwambia mimi na mdogo wangu ..siku moj akasema nataka mniambie ndani a ile nyumba ya tatu kuna watu wangapi wanaishi mle na mkadirie na umri nawapa wiki nzima...sasa ndani ya wiki moja tulikuwa tuna kazi hiyo ya kujua na alitwambia sitaki mwende pale mkaonekana na mkaulize haya niliyowambia tumieni akili zenu kujua ....
basi kwa kuwa ilikuwa ni kazi ilibidi tufanye..kufanyika kwake ilikuwa ni kuangalia hasa wakati wakifua nguo wakianika...zile nguo tuliweza kuziangalia na kuelewa ni nguo za aina gani...za watoto tulizona..za watu wazima tuliziona ...za watoto wa kike au kiume tulziona na pia a watu wazima...njia hii ilitusaidia kujua nyumba ile ina watu wangapi...na wa jinsia ipi....lakini pia tulikuwa tukienda kwenye pipa la kutupia taka kabla ya wahusika hawajaja kuchukua uchafu ule...tulikuwa tuna akusanya vijikaratasi..na hapa napenda niseme wazi kabisa watu wengi hawalijui hili hata huko maofisini..unakuta mtu karatasi ina bonge la siri anachofanya ni kuifinyanga finyanga kwa kiganja kisha aantupa kwenye dustbin...sasa sisi tuliweza kutumia njia hiyo ya kwenda kwenye ma dustbin na kuangalia vikaratas karatasi, chupa, mifuko , karatasi za benk (pay slip) nk .. na hvyo tulijua mtu flani anapenda kutumia kinywaji gani, ananunua wapi, benk ya yake ni ipi, na mambo mengine kama hayo...
yote hii ni kutaka kujua watu wanaokuzunguka ni wa aina gani na hivyo uishi nao vipi...yako mazoezi mengi sana hata tulipokwenda ''shambani ''meng tulifundishwa namna ya kumjua mtu hata kama hujawahi kumuona...namna ya kuangalia hata mwandiko na aina ya uandishi wa mtu na ..mwandiko ni njia moja wapo ya kujua tabia ya mtu....humu jf kwa kuwa hatuandiki kwa wino lakini unaweza kujua character ya mtu kutokana na uandishi wake...kwa mfano
The Boss hawezi akaandika kama anavyoandika@lara 1..au anavyoandika
Pasco ana tofauti kubwa na hao wengine ukifatilia michango yao yote na aina ya andishi wao waweza kujua ni watu wa aina gani...
jambo la msingi hapa ni kuelewa na kujielewa na kuwa makini kwa kila jambo...nguvu ya umakini ni muhimu sana...ni lazima utengenezwe kuwa spy nje ya hapo ni ngumu kufanikisha kazi kujitengeneza mwenyewe ni ngumu sana..