BM-40 OPERATOR
Senior Member
- Oct 13, 2012
- 153
- 55
Kuna siku moja dogo mmoja mwanafunzi wa chuo alikuwa maeneo ya mjini katika mkoa flani akiwa na mwenzake wa kiume pia ghafla akajikuka mikononi mwa askari wawili wenye sare na mmoja amevalia kiraia tu (plain clothes) na kumwambia kuwa anahitajika katika ktuo cha polisi kuna malalamiko dhidi yake na ilibidi ayatolee maelezo yeye peke yake. Kwa kuwa yule kijana hakuwa ametenda kosa lolote la kihalifu wala hakubishana nao, yeye alienda nao tu moja kwa moja mpaka kituoni kisha mahojiano yakaanza kati ya askari hao na yule kijana katika chumba kidogo kilichopo ndani ya kile kituo kwa muda kama wa masaa 2 na nusu hivi kisha akaachiwa. Baada ya kama mwezi mmoja baada ya tukio, yule kijana aliwaaga wenzake kuwa anaenda nyumbani ameitwa kuna matatizo ya kifamilia kisha atarudi ndani ya muda mfupi. Alivyoenda ndio kimoja mpaka leo wenzake hawakumuona tena mpaka leo hii na hakuna anayejua wale askari walimwambia nini kwenye yale mahojiano.
"yasiyokuhusu ni kujaacha kama yalivyo"
"yasiyokuhusu ni kujaacha kama yalivyo"