Poise kutokana na kusoma kwangu google kuna haya ambayo ninafahamu na nitakujibu kwa mfumo wa questions (Q) and answers (A)
Q: 1. je usalama wa mtu ama kundi lililotoa taarifa lina hakikishwaje kuwa hawatadhurika?
A: katika hali ya kawaida kama mtu hajapitia mafunzo yoyote ya kiusalama (mtu wa kawaida sana) huwa inahitaji umakini wa hali ya juu sana katika ku-handle taarifa za siri za kiusalama na kuhakikisha zinafikishwa pahala husika laa sivyo mtu anaweza kukutwa na madhara hata kabla ya kufikisha taarifa hizo sehemu husika.
kwa hapa tanzania sijui ni wapi taarifa hizi mtu wa kawaida anapaswa kufikisha, ingawa wengi wanasema ni polisi, ila kwa nchi kama marekani kuna office maalumu ya kupokea taarifa za wananchi juu ya masuala ya matishio ya kiusalama (counterintelligence office) na hii ofisi ipo chini ya FBI na mwanajeshi ama polisi yeyote hapaswi kutoa taarifa kama hizi za kijasusi kwa mtu yeyote aliye juu ya chain of command yake.
Q: 2. Je kuna uwezekano wa watu wa intelligence system wenyewe kumpoteza aliyetoa /aliyewapatia taarifa hata kama ni kwa siri na kwa hata malipo ya fedha au kitu chochote watakachokubaliana na mtoa taarifa?
A: linapokuja suala la kupokea taarifa za kiusalama kutoka kwa mtu wa kawaida aliye nje ya system, hizo taarifa zinaweza kuwa sahihi ama si sahihi zenye lengo la kuwapoteza malengo na mikakati yenu. mtoa taarifa anaweza kutumwa hata na maadui ama mahasimu wenu ili kuwa-deflect malengo. hivyo baada ya kupokea taarifa, idara nyingi wanambinu zao za kuthibitisha kama taarifa husika zipo sahihi ama la kabla ya kufanya maamuzi.
Q: 3. Wakati uo huo kwa mfano akitoa taarifa na kundi alilotoa taarifa zao likawa linataka kumdhuru sasa hao watu wa intelligence system [hapa nazungumzia system ya nchi yoyote ile] wanamsaidiaje au kumlindaje ili asiumizwe au kupotezwa?
A: hapa sasa ndio inakuja ile issue ya elimu juu ya ku-handle taarifa na kujua ni wapi pa kuzifikisha. unaweza kupeleka taarifa polisi kumbe polisi officer uliyemfikishia hizo taarifa akawa ni sehemu ya mtandao wa huo wa kihalifu unaotaka polisi waushughulikie. endapo itajulikana kama umetoa taarifa sahihi ila kuna leakage ya aina fulani ni lazima utalindwa na huyo muhusika wa leakage kuchukulia hatua mara moja. sasa ni namna gani wanamlinda hiyo ni siri yao.
NIMEJARIBU KIASI CHANGU