Ili uwawin wananchi wengi wa TZ (wengi hawajasoma, maskini, na wanachohangaikia wao ni mlo tu wa siku) inabidi uwe na tabia kama zile za Magufuli, za Kuishi, kusema na kuyatenda yale kundi hilo nililolitaja linataka! Samia hana haiba ya kuyafanya hayo aliyokuwa anafanya Magufuli.
Samia ni wa kisasa zaidi, hivyo yeye kama yeye ataweza kuwawin watu wa kundi la juu na kati, may be na wanawake sababu ya jinsia yake. Inabidi apate wasaidizi wanaokubalika na hilo kundi la chini ili limuunge mkono, ambapo kwa sasa naweza kusema ana Majaliwa, Kabudi, Ummy, Aweso, may be na huyo Lukuvi. January, Riz, Nape, Mwigulu hao wote tabaka la chini linawakataa, linawaona siyo wenzao (Nadhani unajua maskini walivyo).
Kwenye siasa za chama hadi sasa anaufinyia ndani vibaya mnoo, jinsi alivyopokea nchi kutokana na kifo cha Magu, jinsi alivyodeal na suala la Mbowe, jinsi alivyodeal na wafuasi wa Magu chamani, na sasa jinsi alivyompiga matobo Job, simply the best