Salam wakuu,
Nimekua nikifuatilia kwa muda mrefu sasa kuhusu swala la hili eneo la Area 51 ambalo lipo maeneo ya Nevada desert marekani. Kuna nadharia nyingi sana kuhusu eneo hili, na Kituo hicho kilichojengwa Mwaka 1955 kilikua ni cha kificho mpaka mwaka 2013 Mwezi August CIA ilivyoweka wazi existence ya kituo hiko .
Basically ni Moja ya air force base ya marekani lakini kuna usiri mkubwa sana kuhusu eneo Hilo na kinachoendelea ndani. Ni very restricted area na kuna mabango mengi ya vitisho kama "TRESPASSERS WILL BE SHOT, SURVIVORS WILL BE SHOT AGAIN" [emoji41].
Je, ni nini wamarekani wanaficha? Je, ni kweli kuna aliens waliangukaga pale?
Cha ajabu hata Rais mwenyewe kwa mwaka anaruhusiwa kutembelea eneo hilo kwa limited time pekee (sijui mara mbili).