Argentina National Football Team (La Selección) Special Thread

Argentina National Football Team (La Selección) Special Thread

Ezekiel Lavezzi anakusudia kumburuza mahakamani radio presenter kwa kutangaza kuwa alivuta bangi muda mfupi baada ya kipindi cha mazoezi kabla ya mechi dhidi ya Colombia ambayo Argentina waliibuka na ushindi wa goli 3-0.

Leonel Messi aliongoza wenzake 25 kugoma kuongea na vyombo vya habari kufuatia kudhalilishwa kwa Lavezzi.
 
MESSI AWAONGOZA WACHEZAJI WA ARGENTINA KUGOMA KUJIBU MASWALI YA WAANDISHI WA HABARI
Lionel Messi ameowangoza wachezaji wa timu ya Argentina kususia kujibu maswali ya waandishi wa habari.

Messi amefanya hivyo baada ya kiungo wa timu hiyo, Lavezzi kutangazwa kwamba anatumia dawa za kulevya huku akijua ameitwa kwa ajili ya majukumu ya timu ya taifa.

Argentina iliitwanga Colombia kwa mabao 3-0 katika mechi ya kuwania kucheza Kombe la Dunia na kuamsha matumaini.

Messi alisema wachezaji wote wanaungana na hawatajibu swali lolote la waandishi wa habari huku akisisitiza wanataka kupewa heshima yao.
3A6FF16000000578-3941082-image-a-62_1479293815598.jpg
 
Argentina________Chile

02:30, Mar 24 2017
Tournament
World Cup Qualification CONMEBOL 1st round
Match Date
Fri, Mar 24, 02:30

U'r welcome Again!
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Chile lazma wafe

Tena kifo cha mbwa, na atakiona cha moto huku la pulga, huku the bruno Dybala...huyu fundi natamani aje Barca nitafurahi aisee.
Ref hawa jamaa wanawasumbua sana Argentina kila wakikutana. Hii game itakuwa 50/50.

Uzuri ni kuwa yule kocha George Sampaoli aliyekuwa akiwasumbua sana kwa sasa hayupo. Anaifundisha sevilla kwa sasa.
 
Tim limejaa mastaa wakutosha na wengine wanakosa hadi nafasi...lakini sijui tunakosea wapi jamani.hii inashangaza sana. Lakini All in All dakika 90 zitaamua hiyo cku..
 
Full Time:

Argentain 1 - 0 Chile...Messi 1

Next match na Bolivia,

Itapigwa 29 March, 23:00 kwa saa za bongo
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Back
Top Bottom