Argentina yaanza mchakato kuvidai tena visiwa vya Falklands kutoka Uiengereza

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Waziri wa mambo ya nje wa Argentina Santiago Cafiero amesema tayari ameshamjulisha mwenzake wa Uiengereza James Cleverly nia ya nchi yake kujitoa kwenye mkataba wa mashirikiano uliosainiwa mwaka 2016.

Wakati wa utawala wa Margret Thatcher nchi hizo mbili ziliwahi kupigana mwaka 1982 kuhusiana na visiwa hivyo ambavyo viko masafa ya meli 300 kutoka Amerika ya kusini.

Jumla ya watu 3500 wanaishi kwenye visiwa hivyo. Katika madai yake makongwe Argentina inasema visiwa hivyo vilichukuliwa na Uiengereza visivyo halali mnamo mwaka 1833

f7f99af037f54fb2b78ddc636c530b4f
 
UK ni wasikivu na wapenda amani wakitumia njia za kidiplomasia vzr watarejeshewa visiwa hivyo bila shida
 
Raia wa folks wanajiona waingereza zaidi kuliko waagentina hapo ndio mtihani
Ndivyo wallivyo watu wote waliowahi kutawaliwa na wakoloni wa Ulaya.Hata Mayote pia wanasema ni wafaransa.Hilo wakoloni wanalijua ndio maana ukianza kuzozana nao wanakwambia itisha kura ya maoni. Dawa ni kufanya kama vile alivyofanya China kwa Hong kong.
 
Na huu ndio muda sahihi wa Argentina kuvidai hivyo visiwa iwapo wana maslahi navyo kwani Uiengereza yenyewe iko hoi haiwezi tena kupigana kama mwaka 1982,
Jichanganye, maji utayaita mma. Uingereza ilitembea zaidi ya kilomita 10,000 kwenye maji kwenda kupiga vita ndani ya miezi michache sasa unataka uilinganishe na superpower mmoja ana mwaka sasa anashindwa kupigana na jirani aliyevamia kupitia ardhini nchi mbili.

Kwanza Argentina ya miaka ile ilikuwa inaongozwa na military junta, na baada ya vita walihukumiwa na wananchi wale viongozi. Viongozi wa kijeshi hununua silaha nyingi zaidi kuliko wa kiraia, sasa hivi Argentina haina jeshi kubwa
 
Raia wa folks wanajiona waingereza zaidi kuliko waagentina hapo ndio mtihani
Falklands nadhani havikuwa na settlements kabla ya Waingereza. Sasa hata ungekuwa wewe ungechagua lipi kati ya kuwa raia wa Argentina au wa UK.
Na wanaoishi pale wengi ni asili ya Uingereza wanaleta shida, ukijichanganya ukaitisha kura ya maoni wanabaki.
UK wala haililii Falklands kama wanaoishi visiwa hivyo wanavyoililia
 
Haililii Falklands Kisha anapeleka jeshi maili 5000 kwenda kupigana!!..acha ujinga
 
Back
Top Bottom