Scientifically all people originated from Africa, ila Fijians hawatoki Tanzania. Asili ya watu haikuwa inapaa inaenda kutua ukanda fulani, hakukuwa na meli inayosafirisha wahamiaji. Kama Fijians wangekuwa na asili ya Tanzania walitakiwa waache jamii zinazowafanana kule walikopita. Wangoni walitoka South Africa kuja Tanzania, nchi za Kusini kwa Tanzania unakutana na Wangoni. Hawakufyatuka tu kutoka Afrika Kusini wakafika Tanzania.
Hakuna mtu angeweza kutoka Kigoma akasafiri kwa maji mpaka visiwa vya Fiji. Afrika hii ilikutwa na wazungu, Waafrika hawakujua kama kuna bara lina wazungu ila wazungu walilijua dark continent. Sisi sio watu wa sea voyages, ambaye angesafiri angefia safarini baada ya miaka kadhaa kama angeenda direct, na vyombo vya kubeba watu wengi pamoja na supplies zao havikuwepo, kwamba wangezaana humohumo akafa wazazi na watoto wakafika Fiji.
Endapo wangesafiri kwa kutulia sehemu wangeacha baadhi ya vizazi pale. Sasa kisiwa gani kingine wametokea Tanzania?
From Tanzania to Fiji Islands ni more than 15,000km. Hakuna uwezekano wa watu kutoka Tanganyika maelfu ya miaka iliyopita wafike Fiji bila kuacha vizazi njiani, sasa from Tz kwenda Fiji njia ya karibu unapita Southern Asian countries. Kuna weusi kule? Au kina Indonesia, Philippines, Malaysia, Brunei? Au utawasingia black Indians wale wa Kusini wanaobaguliwa.
Alternative wangepita Western, wangeingia Congo wakate bahari mpaka wafike South America. Wakate Brazil wavuke upande mwingine kina Argentina na Chile uko kisha waache bara wakate bahari waingie visiwa vya Fiji. Sasa mbona South America haikuwa na weusi mpaka pale walipopelekwa na wakoloni?
Fijians ni Melanesians, wana ufanano na majirani zao Papua New Guinea na kwa mbali Indonesia. Mtu anayesema Wafiji wametoka Tanzania namchukulia mwenye uelewa wa kawaida sana na asiyetumia common sense.
Hapa nimeeleza kwa elimu ya shule ya msingi, zaidi ya hapo kuna tens of reasons kukataa hoja yako