Argentina yatwaa ubingwa Kombe la Dunia - Qatar 2022

Mimi kila nikienda kucheki mechi, naangali mpira tu. Nani anabeba ndoo ni matokeo ya mechi ya mwisho ktk mashindano haya...

Tulianza makundi, sasa tupo 16 bora. Kila aliefika hatua hii siyo bahati bali ni uwezo. Na kila timu inatamani kufika fainali, hivyo kila timu inajitoa kwa nguvu zote kupigania hiyo

Kubeza timu usiyoipenda ni haki yako kishabiki lakini kumbuka kuibeza timu hiyo haitasaidia timu yako kufika fainali au kuzuia timu unayoibeza kufika fainali. Na kinyume chake ndiyo ukweli... Kama ipo ipo tu...

Kila anaeishia hatua flani ndiyo uwezo wake umeishia hapo... anyway ngoja tuone hatua ya 16 bora inaishaje?

Ni mtazamo tu wazeia....
 
Hizi timu zilizoingia 16 Bora kwa michongo michongo ,kupitia migongo ya watu wengine sijui Korea ,Japan .....wanaenda kupigwa kipigoo cha mbwa Koko [emoji3][emoji3]
We jamaa vipi wewe! Khaaa! Korea na Japan wameingia kimchongo?! Yaan kivipi yaan... hebu tuchambulie kauli yako uliyoitoa bila kufikiri kwa shinikizo la mapenzi kwa baadhi ya mataifa au nchi(timu) na hasira za kijinga na chuki za hovyo dhidi ya mataifa(timu fulani)... je! Brazil akifungwa tena na Korea akatolewa utakuwa bado ni mchongo endelevu?! πŸ˜ƒ


Hayo mambo ya michongo na kubebana sijui kubebwa yalikuwaga zamani huenda kwa sababu teknolojia haikuwa imekuwa kama sasa. Kwa mfano:- enzi za kina Maradona kuna game ilipigwa kwenye michuano hii hii ya Kombe la dunia, Argentina walikuwa wanakipiga na England jamaa akafunga goli la mkono na england wakatoka baadae sana kwenye vyumba maalum walipokuwa wana-review au kupitia video kwa umakini wa hali ya juu na zooming za kutosha wakagundua jamaa alishika na game ilikuwa ngumu kwelikweli upande wa Argentina lakini kwa sababu ilikuwa ishapita watu wakafunika kombe mwanaharamu apite na England wakakausha. Vilevile mnamo mwaka 2010 nchini Afrika kusini ilipigwa game kati ya Germany na England, Mbugi ilikuwa sio ya kawaida... Germany akatangulia kupata bao moja, dakika chache England wakachomoa.... Germany wakaongeza, England wakapambana Frank Lampard akachomoa tena bonge la Bao nyuzi tisini... iligonga mwamba wa juu ikadundia ndani ya chaki ila kipa wa Germany akatoa nje ila ilikuwa ishaingia na Refa akasemaga sio goli ile iliwakata mood sana Waingereza na wakawa washasusa wakawa wanacheza ilimradi tu na kususa kule mwisho wa siku kukawafanya wakafa bao nne kwa moja (4-1) hatua ya 16 bora... england wakaenda kwao. Sasa yote hayo yalikuwa yakiendelea kwa sababu teknolojia ilikuwa haijaendelea kama sasa ndo mana ikaletwa "VAR"..., "AAR" n.k kwa hiyo kila kinachoendelea kwenye soka saiv hakuna Janjajanja wala michongo. Futa mawazo ya kiafrika hayo.
 
Njoo sumbawanga boss ni buku tano tu
 
Amka mkuu kumekucha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…