Nawaombea France wapite leo dhidi ya Morocco kwa sababu kuu mbili:
- Morocco wanacheza mpira wa kihuni unaofanana na wa Argentina. Morali yao ni kubwa sana, tukikutana fainali itakua mechi ngumu zaidi. Ufaransa wanacheza soft ball, na tayari kwa Argentina hii soft ball imeprove failure.
Morocco wancheza sana aerial balls, na wako na average height kubwa kuwazidi Argentina. Hilo linaweza kua tatizo kwa Albiceleste. Ila wafaransa wanategemea zaidi mbio, kitu ambacho sioni kikiwasaidia kwa Argentina. Unakimbia vipi na mpira wakati kila baada ya hatua tatu, wahuni wanatandika reli?
- Sababu ya pili, ni kwaajili ya haters wa Argentina. Ufaransa ndio kichaka chao cha mwisho kilichobakia. Walijifcha kwa Australia tukawakurupusha. Wakakimbilia kwa uholanzi, tukawatimua. Wakaingia kichaka cha Croatia, tukakitia moto. Sasa wamekimbilia France. Inabidi wafuzu hao France ili tumalizie kazi yetu.
Wakifuzu Morocco alafu tukawapiga, hawa wapuuzi wa humu watasema Morocco ni wadhaifu. Acha aje huyo mbabe wao ili wakose kisingizio!
NB: kama hautaki Argentina wafunge magoli ya penati, waambie wachezaji wa team lako wacheze kwa adabu na akili. Wakitumia miguvu bila akili, sisi tutapiga tu hizo penati hata tukipewa saba kwenye mechi moja.
Na kama unadhani kufunga kwa penati ni rahisi, muulize Mbappe kilichomkuta kwenye Euros. Waulize mabishoo wako wa Brazil, na umuulize Harry Kane!