Nawapongeza mashabiki wa argentina wote humu jamii forum
Safari ilikuwa ngumu lkn Mungu wa mbinguni alitupigania
Nimesoma comments zote nikiri wazi mashabiki wa argentina mpira wanaujua
No panic
No matusi
No hate language kwa wachezaji
Tulipofungwa mechi ya saudi arabia ndio nilifurahi sana ile ilikuwa ni wake up call kwa wachezaji walibadilika sana
Baada ya hapo mechi zote tulicheza vizuri mpaka jana
Makosa ya ottamend kusababisha tuta ndio kuliwarudisha ufaransa mchezoni
Maturity ya timu ilistahimili kipindi kigumu baada ya kusawazisha ufaransa
Mungu awabariki sana
Ningependa Christmas au new year tukutane tupate lunch km mshikamano, football huleta urafiki,undugu,upendo ujamaa
Kuna mashabiki washamba na wasio jua mpira wanamuita messi mfupi
Urefu wa messi ni 169cm na hiki ndicho kimo cha watanzania wengi tena wengi wanaishia 150cm
Ukiona shabiki anamshambulia mchezaji kwa lugha ya maumbile yake kwa chuki ujue huyo siyo mtu wa mpira ni kahaba aliyevamia mpira
Yote kwa yote football is a beautiful thing wandungu
Ile moment argentina anaongoza mbili kuna mzee alitoa ofa watu wanywe bia mbili wote
Ile bar ilikuwa na vibe
Ufaransa walipokuja kuchoka akainuka mfaransa akamlipa mzee bia zikatembea
Messi alipotuinua mzee wa argentina akatupiga round tena basi ikawa hivyo
Ni siku nyingine ambayo sitahisahau I love football