Venus Star
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 26,519
- 78,311
Utangulizi
Za leo wana JF.Kama kawaida yangu katika kuelisha watanzania ili waweze kuijua kweli.
Matishio haya na uvumbuzi wa hizi silaha za maangamizi hayana nia njema katika dunia yetu hii.
Leo nitaongelea kuhusu Mabomu ya nuclear na matokeo ya Neclear Winter na mwisho wa binadamu kuishi duniani.
Armageddon ni concept iliyo andikwa kwenye biblia katika kitabu cha ufunuo 16:16. Ukitaka kuelewa zaidi kuhusu concept hii unatakiwa uisome sura yote ya 16. Kwa ufupi ni kwamba sehemu hiyo watakutana wafalme wa dunia na vita kuu ya dunia itapigwa. Siku hiyo inaitwa Siku ya Mungu (Day of God). Na itakuwa ndio mwisho wa dunia, maana watu wengi sana watakufa.
Concept hiyo ninaiweka sasa katika hali hii ya sasa dunia ikishuhudia nchi kumiliki silaha za maangamizi zaidi ya mabomu 13,000. Huku vita vya kuchokozana hapa na pale zikiendelea bila sababu kubwa za msingi. Wakubwa kutishiana na kuonesha ubabe wao wa silaha za maangamizi. Je, tunaelekewa wapi? hatuwezi kuifanya dunia yetu ikawa ya amani?
Mathara ya Mlipuko wa Mabomu ya Nuclear
Dunia tunayoishi kwa sasa imeshuhudia mambo mawili ya Nuclear yaliyoangushwa huko JapanHiroshima liliangushwa bomu lenye uwezo wa 15 kilotons of TNT
Nagasaki liliangushwa lenye uwezo wa 20 kilotons of TNT
Haya kwa pamoja yapo na 35 kilotons of TNT yanauwezo wa kuzalisha nishati 1.5 x 10^14 joules
Kutokana na kuendelea kwa teknolojia nchi zinamilki mabom ya nuclear yenye uwezo kuanzia 100 kilotons of TNT na zaidi.
Uchambuzi wa kisomi unaeleza kuwa inahitajika mabomu ya nuclear yenye uwezo wa 10,000 kilotons kwa pamoja kuleta maangamizi ya dunia na kusababisha nuclear winter
Kwa mujibu wa hali ya sasa ni mambomu 100 tu yenye uwezo wa 100 kilotons yanaweza kuzalisha 10,000 kilotons
Nuclear winter ni nini?
Nuclear winter ni hali ya hewa ya kupungua kwa joto duniani inayotokana na vita vya nyuklia. Iwapo mabomu ya nyuklia mengi yatalipuliwa, hasa kwenye maeneo yenye majiji au misitu mikubwa, milipuko hiyo inatoa moshi, majivu, na vumbi nyingi sana angani. Uchafu huu ukizuia mwanga wa jua kufikia uso wa dunia kwa muda mrefu, labda kwa miezi au hata miaka kadhaa unasababisha baridi kwenye uso wa dunia.Baridi linakuwa kali, mimea inashindwa kupata mwanga wa jua, maji kukosekana, barafu kuwepo kila sehemu, hewa kuwa ya ukaa na mambo mengi kutokea. Hili jambo likitokea ndani ya mwezi mmoja biandamu wote wanaweza wasiwepo kwenye uso wa dunia.
Je, Silaha za Nuclear ni maandalizi ya maangamizi ya dunia
Mabomu ya nuclear kwa sasa ni zaidi ya 13,000 na kuweza kusababisha Nuclear Winter ni mabomu 100 tu. Mlipuko wa mabomu hauna madhara makubwa ya papo kwa hapo. Lakini baada ya hapo vumbi kubwa na moshi utakuwa angani.Switzerland ndiyo iliyojiandaa na kukabiliana na Nuclear Winter japo kwa Mwezi mmoja
Serikali ya Switzerland ilipisha utaratibu wa nchi kuchimba mahandaki ambayo yatasaidia watu kujificha humo baada ya jambo hili la vita vya nuclear kutotea.Kuna mambo ya msingi makuu manne ambayo bado kila nchi inahangaika kuyatatua ambayo yatatokea baada ya nuclear winter:
- Kujikinga na baridi kuu
- Upatikanaji wa Hewa safi
- Upatikanaji wa maji safi na salama
- Upatikanaji wa Chakula