Arsenal haijacheza na timu bora tuipime, kusema watachukua ubingwa ni matusi makubwa kwa wapenda mpira

Arsenal haijacheza na timu bora tuipime, kusema watachukua ubingwa ni matusi makubwa kwa wapenda mpira

Kuchukua ubingwa sio huruma ni uwezo
Yani sisi Arsenal kuchukua kombe mara moja kwenye miaka yote hiyo ndo mnaona kama tutafaidiika!

Mbona nyie mmechukua mara kibao, tena mlikua mnapokezana kabisa.

Chuki zitawaua nyie maibilisi wekundu!
 
Arsenal haina timu ya kubeba ubingwa wa epl
Unadhani mpira wa Ulaya kama
Bongo kwamba lazima uwe MAyele au Chama ndio ushinde
Mpira saivi ni formula tu ukiingia
Kwenye mfumo wa mtu unakaa

Hata angekuwa Beki Onyango au Kipa Ahmada Arsenal watabeba tu[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Arsenal alicheza na liverpool na chelsea zikiwa icu
Spurs huwa simuhesabu km kigogo
Msimu huu arsenal tayari kamfunga chelsea, liverpool, spurz mkubwa aliempiga arsenal ni man u tu na man city bado hajacheza nae ukiachana na hao kuna newcastle ambae safari hii anasumbusumbua hata watoto wanaosumbua vigogo wakina brighton na brentford uko gunners anawapiga kiulaini tu labda useme atakosa kombe akianza kupata majeruhi ya wachezaji muhimu maana arteta hana kikosi kipana
 
Ukweli ni kuwa arsenal anaongoza ligi kwa bahati bahati hivi ngekewa ngekewa hivi utani utani hivi.

Arsenal amecheza mechi ngumu moja tu ya manchester united hawa ndio walimpa challenge.

Kwahiyo vijana na mashabiki wa arsenal wasije weka matarajio ya ubingwa.

Bahati ya leicester city kuchukua ubingwa kibahati bahati haiwezi kujirudia.

Huwezi kuchukua ubingwa ukiwa na beki mbovu km saliba na margheles. Huwezi kuchukua ubingwa ukiwa na golikipa kimeo km yule.

Uchukue ubingwa nketia au Jesus ni forward? Huu utani wa kijinga kabisa wenzao leicester walikuwa na vardy ngolo,mahrez walikuwa wakali kuliko saka,martnel na partey.

Nakubali wachezaji km saka,partey na martinel wanauwezo wa kuridhisha ila sio hatari hawajafikia ubora wa juu.

Arsenal atafuzu UEFA ila ubingwa wa epl hawachukui.

na yule kocha wa manchester united anaweza akashinda ligi mapema kuliko kocha wa arsenal kwasababu kocha manchester united anampa wakiutu uzima zaidi km alivyo ancelot wa madrid.
Huyo wa man atafukuzwa kabla ya jua kuchwa
 
Liverpool na chelsea zilikuwa ICU wakati wanacheza na arsenal
Kwahiyo Chelsea ya kipindi kile na Chelsea ya saizi ipi ina unafuu?

Sawa Arsenal habebi ubingwa, kwahiyo bingwa ni nani?
 
Back
Top Bottom