Arsenal (The Gunners) | Special Thread



WILLIAM THE CONQUER







Arsenal 1-0 Chelsea
William Gallas scores as Arsenal defeat Chelsea for the first time since February 2004 to reclaim top spot in the Premier League.

Wachezaji walioumia wamerudi (Cesc Fabregas, Alexander Hleb and Mathieu Flamini), Je moto wa Arsenal utaendelea kuwaka?
 
Huenda ukaendelea kuwaka, kwa sababu vijana wa Imarati wana ghadhabu sana mwaka huu, ingawa mara moja moja huwa wanabebwa sana!
Big up sana vijana wa Wenger, sie wa Trafford Kongwe tupo nyuma kidogo!
 
Leo mechi ilikuwa tamu sana mwishoni mwishoni.

John Terry na ubabe wake,kawekewa na Eboue imekuwa ishu. Halafu cha kushangaza, Eboue katoka uwanjani na machela.....ila hakuna habari yoyote kuhusu Eboue kuanzia BBC, hadi SkySPorts.

Ila Arsenal tunapeta. Next ni Tottenham next wknd. Defense yao mbofu mbofu.....pointi 3 zingine mfukoni.
 
Mpaka sasa hivi, Arsenal 3 - 2 Blackburn.

Arsenal wana wachezaji 10 uwanjani.
Bado tunaendelea taaaratibu........
Extratime 30 minutes. First 15 ndio zinaisha.

Eduaaaaardooooooooooo.......
 
Timu za leo

Mechi ya kwanza kwa kocha wa Spurs Juande Ramos na ushindi kwa Gunners leo utaiweka kileleni mwa Premier League hata wakti wa Xmas!

Arsenal: Almunia, Sagna, Toure, Gallas, Clichy, Eboue, Fabregas, Flamini, Rosicky, Hleb, Adebayor.
Benchi: Lehmann, Senderos, Eduardo, Gilberto, Bendtner

Tottenham: Robinson, Tainio, Chimbonda, Kaboul, Lee, Lennon, O'Hara, Boateng, Malbranque, Berbatov, Keane.
benchi: Cerny, Defoe, Taarabt, Huddlestone, Archibald-Henville.

Referee: Rob Styles (Hampshire)

Uwanja- Emirates

Interesting.
 
Baada ya kipindi cha kwanza ambapo Spurs wamecheza wakiwa watu kumi nyuma ya mpira(kujihami) Arsenal wamejaribu kutumia njia ya kati.

Goli! dakika ya 48

Fabregas anatumia njia ya midfield kumtengenezea mpira Adebayo na Adebayo anafunga goli lake la kumi kwa msimu huu wa Premier League.
 
Goli! Dakika ya 66

Wakitumia mpira wa juu unamkuta Robie Keane ambae anamdondoshea Dimitar Berbatov anaefunga goli safi.

Almuni ana maswali ya kumjibu Wenger.
 
Penalti! dakika ya 72

Arsenal wanashindwa kuokoa mpira wa adhabu na Koro Toure anamchezea vibaya Berbatov na refa Rob Styles natoa adhabu ya penalt na Almunia anaokoa Arsenal kwa kurukia upande wake wa kulia na Robie Keane anaikosesha goli Spurs.
 
Goli! Dakika ya 75

Kocha Wenger anamtuma Nicklas Bendtner kwenda kubadilisha mchezo na anachukua nafasi ya Emanuel Ebue.

Mpira wa juu unamkuta mtoto Bendtner ambae anfunga goli safi la kichwa na la kwanza kwake kwenye Premier League.

Dakika zimebakia si zaidi ya chini ya kumi plus added minutes.
 
Mabadiliko! dakika ya 82

Zikiwa zimebaki dakika 8 na zile za nyongeza ambazo si zaidi ya nne, Arsenal wanafanya mabadiliko na Alex Hleb anatoka na anaingia Giberto De Silva.

Kazi ya Silva ni kuimarisha safu ya ulinzi kwa kucheza mbele ya Galas na Toure kuzuia mashambulizi ya Keane na Berbatov
 
Dakika tisini na tatu za nyongeza zimeisha na Arsenal imeshinda kwa goli mbili kwa moja.

Arsenal itaendelea kusimama juu ya Premier League kwa kuwa na point 43 na hata wakati wa Xmas watu weeeeh!

Sasa nami naweza kupata moja moto na moja baridi kwani kuna kampeni ya kuwatoa Arsenal pale kileleni.

Weekend njema!
 
Tuendelee kukunja ngudu tu sasa Man U wabanjuliwe na Everton,lead ya 1 point sio comfortable kabisa.
 
Arsenal Wanatisha! Ni hatari tu- mwaka huu!! Sii hadithi ni ukweli tupu!!!!!!!!!!!!!!!!!
 

Despite a dubious penalty Arsenal have come on top of Tottenham Hotspurs condolences to JK and his team. Next Carling cup semi final with them, Ramos you still have work to do.
 
Nilibaki mdomo wazi pale Tottenham walipopewa penalty baada ya kumsikia mtangazaji mmoja akitamka,'Keane has never miss a penalty and this is a sure goal' nilitamani nimuulize wewe Mungu!? Na muumba akasikia sala zangu...LOL!

The good thing about Arsenal, they always find a way to win 95% of the time...🙂
 
Wakuu,
Mechi ya leo ilikuwa ngumu aisee.
Arsenal walikuwa hawajatulia kabisa. Yaani hata Fabregas alikuwa anatoa pasi mbofu mbofu. Ila goli la kwanza la Gunners lilivyochongwa, inabidi Fabregas asemehewe makosa ya leo. Maana kaondoka katika half ya Arsenal mpaka penati boxi....halafu akatoa pasi ya kisigino......You have to see the goal to appreciate it. Mzee Adebayor akamaliza taaratibu kabisa....mpira ulikuwa usawa wa milimita moja juu ya nyasi...nyavu zikatikisika, mashabiki tukakaanga chipsi!!

Halafa Niklas Brendter, eeh bana. Kaingia tu uwanjani......first touch yake...goli!! Halafu derby match!! What a day for the young striker. Ila nimefurahi zaidi jinsi alivyoruka hewani na kujikunja, akaunganisha kichwa kitamu chenye kasi ajabu....akiwaacha madefender wa Spurs na golikipa wao wakipiga lamli.

Gunners!! Nani hataki??
 
1-4. Take it, 'ave it, well 'ard, bang bang!! Nani hataki??

MaNure mpo?

Fox in the box aka Eduardo atlast he comes good twice, Adebayor, n Rosicky.....

Bado mnabisha??
 
Wenger leo ampumzisha Bacary Sagna

Justin Hoyte na Theo Walcort na Emannuel Ebue huenda wakarudi katka mechi na West Ham au "The Hummers".

Lakini Gilberto na Robin Van Persie bado ni majeruhi.

Timu ya leo:

Arsenal:

Almunia, Hoyte, Toure, Gallas, Clichy, Eboue, Flamini, Fabregas, Hleb, Rosicky, Adebayor, Lehmann, Bendtner, Diarra, Song, Diaby, Walcott, Senderos.

Habari zaidi baadae ntakapokuwa pale Emirates.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…