Mkuu kwanza nikupongeze kwa thread nzuri sana ya AI japo umebase upande mmoja. Maelezo yako mengi yameegamia kwenye SIMPLE AI ambayo inakuwa controlled na mwanadamu mwenyewe. Hii kwa kiasi kikubwa upo sahihi lakini tukija upande wa pili sidhani kama upo sahihi.
Ikikupendeza zaidi soma vizuri kwanza nini maana ya neno ARTIFICIAL.
Then
1. Artificial intelligence ni nini?
2. Aina zake ni zipi? (Hapa ndipo utakuta kuna moja ambayo sometimes inaweza kujicommand yenyewe na ndiyo inaogopwa kwamba how siku ikitokea ikareact tofauti na matarajio ya mwanadamu?
3. AI future yake ni ipi? ....pointi ya 3 inakufanya usiangalie miaka ya leo au miaka 10 ijayo bali anzia miaka walau 50-100 ijayo. Kama leo watu wanaanza kutengeneza wanawake wa bandia kama yule Manuel Pellegrin.... Saudia wana Sophia then kuna ELIZA ambaye watu wa IPhone wanamuita SIRI vipi kuhusu miaka 100 ijayo?
Kuhusu biashara upo sahihi, watu wanaitumia kwenye brand zao kupiga pesa hiyo ni OPPORTUNITY COST acha wajanja wale pesa.
Ukitaka kuichimba deep msome JOHN MCCARTHY. Utaijua AI ndani nje na future yake hasa ni ipi.
Mwanafizikia mkubwa HAWKING aliwahi kusema kwamba AI inaweza kuwa ni kitu bora zaidi dunia kuwahi kukipata au kitu cha hatari zaidi kuwahi kutokea duniani hususani hizo complex AI ambazo zina uwezo wa kujicommand zenyewe. Akaandika mpaka barua ya wazi kwamba isije kutokea ikaanza kutumika kwenye vita hususani matumizi ya nyukilia kwa sababu madhara yake ni hatari mno.
Kama saivi tumeanza kuletewa neurolink, watu wanatengeneza chip ambazo zinaweza kurekodi ndoto kisha ukaja kuitazama baadae. Watu wanatengeneza chip ambazo ukiwekewa kichwani wanaweza kufuta kumbukumbu zako zote and still unahisi ni ulaghai mkuu?
Huenda tunatofautiana kwenye uelewa na mitazamo.
Naheshimu mtazamo wako na asante kwa somo zuri.
Sent from my SM-A107F using
JamiiForums mobile app