MwanajamiiOne
Platinum Member
- Jul 24, 2008
- 10,470
- 6,580
- Thread starter
- #81
hii kauli hapo juu imeniondoa kabisa kwenye reli kama sio kunishtua.........................
Hivi kweli ndo tumefikia hapa jamani?
Faraja siku hizi huwa inapatikana kwa the so called mshefa, na sio mume tena?.............
mungu atusamehe bure, maana nzima ya ndoa imeshachakachuliwa hapa...........lol.......
bacha nafikiri inategemea na situation maana kuna wakati mume anakuwa si mfariji tena bali anageuka kuwa mvunja amani, mvunja faraja yaani anakuwa jitu badala ya mtu. Najaribu kufikiria mume anayetelekeza familia anakimbilia kwa kimada, miezi na miaka akikumbushiwa ya familia yake ni matuc , kejeli na vipigo miaka na miaka hadi unakata tamaa ya kuwa atarejea tena,,,,,,,,,,,,,,,,,wanawake wengi ni wazito kudai talaka katika situations kama hizi wengi wetu tumekolezwa na mafundisho ya vumilia, ndoa ndivyo zilivyo na ukishindwa sana basi OKOKA na umkbidhi situation nzima MUNGU wako.
Sasa ukiangalia kizazi chetu cha sasa ambako MUNGU anawekwa mbali na maadili ya dini yanazidi kumomonyoka matokeo yake ndo haya, option ya OKOKA na umkabidhi MUNGU matatizo yako imekuwa replaced na .........TOKA NJE NAWE UFURAHIE MAISHA KATIKA MWANGA BORA! Nadhani ndicho alichokifanya dada huyu.
So pole mpenzi wangu kwa mshtuko huu.