Mbu
JF-Expert Member
- Jan 11, 2007
- 12,752
- 7,861
Mbu nimekubaliana na wewe kwenye hilo la mfariji, time is a healer...sawa na nimependa zaidi hapo uliposema kwa anayejua atahari za haya mambo hatothubutu kabisa kumnyanyasa mke wake...(hata wanawake hawatathubutu kuwanyanyasa waume zao kadhalika)
Sasa MBU kwa case hii hapa mkononi, MFARIJI naye ni mume wa mtu, huyo dada MFARIJIWA kilichomfikisha hapo ni pamoja na mume kutembea nje ya ndoa.
JE, yeye naye haoni atampa mwanamke wa MFARIJI wake mataeso endapo atajua mumewe anatembea nje ya ndoa? (nilimuuliza MJ1 kama mke wa MFARIJI naye anataarifa sikupata jibu)
AU MFARIJIWA anaona yeye anasbabu ya kumfanyia hivo mwanamke mwenzie?
La hasha,...Natamani huyo mwanadada nae aingiwe na moyo wa huruma kwa mwanamke mwenzake.
Tatizo la balaa hili, mfariji mzuri kwenye case hizi mara nyingi na kwa asilimia kubwa atakuwa mume/mke wa mtu.
Hii ni mtake msitake, na anayebisha aje atoe ushuhuda wake hapa.
Ufariji lengo lake la awali huwa ni kusikilizwa,....kueleweka, ...na mwisho kuliwazwa.
Hapa bado nazungumzia mahusiano ya mwanamke na 'mfariji' bila kuhusisha ngono, kwani tendo hilo
(la ngono) si faraja inayofuatwa nje na wanawake walio wengi walio kwenye mahusiano yenye misukosuko
ya ndoa yao (wanaohitaji faraja ya moyo)
....Sasa anadai mumewe amejirekebisha sana na amebadilika na kuwa 'mume' tatizo liko kwake amejikuta amedevelop hisia kali za mapenzi kwa 'Mshefa' kuliko kwa mumewe na kila akijaribu kumuacha huyu jamaa anashindwa maana anasindwa kujicontrol kabisa. Not only that hata 'Mshefa' huyo hana dalili za kumsaidia 'kurudi' kwa mumewe kihisia kwani kila mara anakuwa kama anamblackmail vie kuwa anampenda na eti somehow huyu mwanamke amesababisha kutokuelewana flani kati yake yeye 'Mshefa' na mkewe nyumbani kwake. So kila mdada akijaribu kumuacha 'Mshefa' mshefa anakuja juu kimapenzi yaani anachochea vile.
Mdada anasema mumewe alishagundua juu ya cheatignyake lakini akamsamehe baada ya mke kukiri na kuapa kuacha. Ila sasa ndo anashindwa kihisia yuko kwa 'Mshefa' zaidi ya mumewe. Anaomba msaada afanyeje a'rudishe' mapenzi na hisia kwa mumewe??
Amekiri kuwa alifanya kosa na anajutia kutafuta 'faraja' nje ya ndoa.
Naombeni tumsaidie .....Nitawaacknowledge msijali
...hapo penye wekundu inaitwa emotional blackmailing aka 'Msukule wa Mapenzi.'
Ni kiasi cha mwanamke kujiambia sasa basi, itakuwa!