...Kiongozi Fidel80....safi kabisa kamanda, ila kwa kesi hii inavyojionyesha; Kwa namna moja au nyingine ndoa hii ilishindikana kuvunjika. Hii inawezekana mke na mume walikosa ujasiri wa kuachana. Narudia tena, Mke huyu alisha suffer abuses za kutosha na kwa kiwango cha uvumilivu wake (Ref hoja ya bht hapo juu) alimpata mfariji, kama mume naye kwa kipindi hiko alipokuwa anamnyanyasa na labda hata kumtelekeza mkewe.
....ninachotaka kuangalia kwa upeo hapa ni je? Huyo mwanamke ambaye miaka nenda miaka rudi amejiona amedhalilika kiasi cha kutosha, amenyanyaswa, amepigwa, ameumizwa, amefikia hatua ya kujiona hana thamani kwa mwanaume yeyote sababu ya matusi, kejeli na yote uyajuayo,....halafu akatokea mwanaume akamfariji, akampa matumaini, akapata amani...furaha, na matumaini angalau kwa muda mchache anaokuwa nje ya nyumba yake...
JE? Unadhani ni rahisi kwa mwanamke huyo kumsahau huyo mfariji wa maisha yake kipindi kile cha dhiki na majuto makuu? Unaukumbuka msemo, 'aliyeumwa na nyoka?....' unaamini mwanamke huyu baada ya haya yote, hana kovu moyoni mwake ambalo hapaswi kukumbukia aliyofanyiwa?....