Arudisheje hisia kwa mumewe? ...Msaada tafadhali

Arudisheje hisia kwa mumewe? ...Msaada tafadhali

Inaonyesha mshefa anazo sana na anamaliza kila kitu kwa huyo mama.
MJ1 mwambie aombe talaka kwa mmewe kama hawezi kumwacha mshefa ili ale kwa uhuru.

anazo hela? sijaona pahala hela imezungumzwa humu....labda tuseme penzi lenyewe tu limemnogea! mapenzi sio pesa Fidel, watu wanaacha waume zao ndani na mapesa yao wanahangaika huko na wauza mkaa....shauri yako
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
moyo wa mwanamke ni kama bahari
kuna mengi mno yaliyojificha.....

ukitaka kumaanisha nini hasa? nyie mioyo yenu haifichi mapapa na manyangumi? dont you guys lie and act as well?
 
Nakupa pole sana kwa kazi ngumu uliyobeba kwani kuna wakati mtu unakuwa concerned na mabo ya watu tena watu wazima kuliko mambo yako mwenyewe.kwani hao wanandoa dini gani?wanaenda msikitini au kanisani?wanasali kweli?kwa akili yao ya kibinadamu wamechokana waachane kama huyo mwanamama anasali,mwambie asikuulize tena wewe akae aongee na mungu wake atapata jibu
 
dc1e7bb70513761a7c33db0c772850bd.jpg
...nadhani kuna haja ya kuangalia kipimo cha ustahmilivu ambacho MKE anakubalika awe nacho. Wengi wape, lakini kumhukumu huyu mwanamke ambaye tayari alisha suffer physical na emotional abuses za kumtosha maishani mwake, kiasi cha kujiona hana thamani, nuru na dira kwenye ndoa yake,mnh...bado naiangalia kesi hii kwa pande mbili;
domestic-violence-physical-abuse-450a102908.jpg
...wanawake ndio silent sufferers. Tuangalie wanawake hawa ambao wananyanyasika kijinsia na kiakili ilhali jamii inayowazunguka (ndugu jamaa na marafiki na hata viongozi wa dini na mabaraza ya wazee) kwenye kesi hizo humlazimisha Mwanamke awe mvumilivu....amrudie Mumewe....
physical-abuse.jpg

Je, ni kiwango gani Mwanamke anastahiki kustahmili. Hivi, mfano wewe mwanaume upo kwa shemeji yako na dada'ko. Kisha usiku wa manane Mumewe anarudi....baada ya muda ukamsikia dada'ko anapigwa makofi, ngumi na mateke chumbani kwao,...na unamsikia dada'ko analia kwa uchungu akiomba mumewe asimuumize, ....utakwenda kumsaidia, au utajisemea hilo ni tatizo lao...watalimaliza wenyewe? Mpaka ni wapi?...
2x07-abused-woman-2.jpg
,......wapi ni mwisho wa uvumilivu?
Mwanamke huyu ambaye kakosa msaada toka kwa ndugu, jamaa, marafiki, kanisa, na hata wazee wa ukoo...
akibahatika kupata mtu atayemfariji kipindi cha misukosuko hiyo,...nani alaumiwe?
 
ukitaka kumaanisha nini hasa? nyie mioyo yenu haifichi mapapa na manyangumi? dont you guys lie and act as well?

bht wewe mwenyewe umesema kuwa wanaume kuna mambo tumejipa kuwa na haki yetu
including cheating.....
utaona kuwa wanaume hatuhangaiki saaana kufanya mambo kwa siri
not that natetea au kuwa proud na hiko but inatufanya tuwe wa wazi kiaina......

sasa nikisema moyo wa mwanamke ni kama bahari....hapa nazungumzia uwezo wa wanawake
kuficha jambo moyoni mwake......mfano kanogewa nje...lakini mume unaweza kabisa usijue
 
Good one Mbu

Let me tell you some... Sijawahi kusikia mahusiano yasiyokua na abuse, adn you know why?? because we have different thresholds and kibaya zaidi malezi tofauti and definition ya abuse ni very wide

Hakuna mwanaume ambaye hajawahi kuwa abused kwenye relationship vivyo hivyo wanawake...the only challenge we have ni how we communicate these abuse to societies around us

Pili, hakuna anayeamua ku-cheat akashindwa, and 99% huchukulia abuse kama sababu... hint, sikiliza wanaume wanaocheat wanavyoongelea mahusiano yao na hao "lovers wa nje"

Once you start cheating, there is no way you will be able to stop completely in a lifetime, because utakua umeprove kwamba IT IS DOABLE!!

LASTLY, in a country like Tanzania, with all these hard knock life na makundi yetu ya kudanganyana... cheating could be as high as 90% kwa walio kwenye mahusiano

MUACHE HUYO DADA ALE MAISHA, NATURAL COURSE ITAKUJA ILI YAISHE
 
Mbu, kila kitu kina ukomo, hata huo uvumilivu wenyewe! kiwango cha ukomo wa uvumilivu kitatofautiana baina mtu na mtu, mwingine akitukanwa ndo mwisho, mwingine akitolewa hata manundu yumo tu...

utakapofikia ukomo wa uvumilivu basi utajiondokea mwenyewe bila hata katekista wala mzazi kushauri (ushauri si lazima ufuatwe). na unapofikia huu ukomo sasa nadhani lawama zimwendee tu aliyesababisha haya yote.
 
Umeongea point haswaaaa.

MJ1 mwambie huyo mama amjaribu huyo mshefa kama kweli anampenda na yupo tayari kubeba majukumu aombe awe bi mdogo na aachane na mmewe hapo ndipo utakapo jua akili ya mwanaume.
 
kwa hiyo mnafanyaga tu carelessly, tukiwakamata poa mkivuka salama poa tu....

twendeni pole pole tutafika....tulianza enzi za mwanamke 'vumilia tu huyo ni mumewo' sasa naona tupo au karibu tunafika 'do me I do you' (kwa kificho na ujanja mkubwa) lakini baadaye tutahamia kwenye kufanya bila kificho saaana!

naona hiyo ndo trend!!
 
Mbu, kila kitu kina ukomo, hata huo uvumilivu wenyewe! kiwango cha ukomo wa uvumilivu kitatofautiana baina mtu na mtu, mwingine akitukanwa ndo mwisho, mwingine akitolewa hata manundu yumo tu...

utakapofikia ukomo wa uvumilivu basi utajiondokea mwenyewe bila hata katekista wala mzazi kushauri (ushauri si lazima ufuatwe). na unapofikia huu ukomo sasa nadhani lawama zimwendee tu aliyesababisha haya yote.

Umeongea point haswaaaa.
MJ1 mwambie huyo mama amjaribu huyo mshefa kama kweli anampenda na yupo tayari kubeba majukumu aombe awe bi mdogo na aachane na mmewe hapo ndipo utakapo jua akili ya mwanaume.

....Kamanda mtm umezungumzia kila relationship ina some elements za abuses, nakubaliana nawe kwa hilo,....ni jinsi kila mtu anavyoweza tolerate mambo. Wengine huona ni abuse, wengine huona mwenziwe mahaba yamemkolea ndio maana anateswa, naye haki yake ateseke.

...Kiongozi Fidel80....safi kabisa kamanda, ila kwa kesi hii inavyojionyesha; Kwa namna moja au nyingine ndoa hii ilishindikana kuvunjika. Hii inawezekana mke na mume walikosa ujasiri wa kuachana. Narudia tena, Mke huyu alisha suffer abuses za kutosha na kwa kiwango cha uvumilivu wake (Ref hoja ya bht hapo juu) alimpata mfariji, kama mume naye kwa kipindi hiko alipokuwa anamnyanyasa na labda hata kumtelekeza mkewe.

....ninachotaka kuangalia kwa upeo hapa ni je? Huyo mwanamke ambaye miaka nenda miaka rudi amejiona amedhalilika kiasi cha kutosha, amenyanyaswa, amepigwa, ameumizwa, amefikia hatua ya kujiona hana thamani kwa mwanaume yeyote sababu ya matusi, kejeli na yote uyajuayo,....halafu akatokea mwanaume akamfariji, akampa matumaini, akapata amani...furaha, na matumaini angalau kwa muda mchache anaokuwa nje ya nyumba yake...

JE? Unadhani ni rahisi kwa mwanamke huyo kumsahau huyo mfariji wa maisha yake kipindi kile cha dhiki na majuto makuu? Unaukumbuka msemo, 'aliyeumwa na nyoka?....' unaamini mwanamke huyu baada ya haya yote, hana kovu moyoni mwake ambalo hapaswi kukumbukia aliyofanyiwa?...

Mimi nadhani time is a healer. Suluhisho pekee ni mwanamke ajipe muda,
Mume mtu naye awe muelewa kwa kiasi gani alichangia kuharibu 'Upendo' wa mkewe,
na kujua consequences zake kama hizi. Kwa wanaojua athari ya haya mambo, hutothubutu
kumnyanyasa mkeo mpaka afikie hatua ya kwenda tafuta maliwazo nje na hapa sizungumzii [ngono!,]
bali ile haki ya kuheshimiwa, kuthaminiwa, kupendwa, kusaidiwa, kuhurumiwa, kusikilizwa, kushauriwa bila
kejeli nk nk....
 
anazo hela? sijaona pahala hela imezungumzwa humu....labda tuseme penzi lenyewe tu limemnogea! mapenzi sio pesa Fidel, watu wanaacha waume zao ndani na mapesa yao wanahangaika huko na wauza mkaa....shauri yako

...nami nilihisi kutumika neno 'mshefa' limeondoa uzito wa sakata hili.
 
Mbu nimekubaliana na wewe kwenye hilo la mfariji, time is a healer...sawa na nimependa zaidi hapo uliposema kwa anayejua atahari za haya mambo hatothubutu kabisa kumnyanyasa mke wake...(hata wanawake hawatathubutu kuwanyanyasa waume zao kadhalika)

Sasa MBU kwa case hii hapa mkononi, MFARIJI naye ni mume wa mtu, huyo dada MFARIJIWA kilichomfikisha hapo ni pamoja na mume kutembea nje ya ndoa.

JE, yeye naye haoni atampa mwanamke wa MFARIJI wake mataeso endapo atajua mumewe anatembea nje ya ndoa? (nilimuuliza MJ1 kama mke wa MFARIJI naye anataarifa sikupata jibu)

AU MFARIJIWA anaona yeye anasbabu ya kumfanyia hivo mwanamke mwenzie?
 
  • Thanks
Reactions: Mbu

...Kiongozi Fidel80....safi kabisa kamanda, ila kwa kesi hii inavyojionyesha; Kwa namna moja au nyingine ndoa hii ilishindikana kuvunjika. Hii inawezekana mke na mume walikosa ujasiri wa kuachana. Narudia tena, Mke huyu alisha suffer abuses za kutosha na kwa kiwango cha uvumilivu wake (Ref hoja ya bht hapo juu) alimpata mfariji, kama mume naye kwa kipindi hiko alipokuwa anamnyanyasa na labda hata kumtelekeza mkewe.

....ninachotaka kuangalia kwa upeo hapa ni je? Huyo mwanamke ambaye miaka nenda miaka rudi amejiona amedhalilika kiasi cha kutosha, amenyanyaswa, amepigwa, ameumizwa, amefikia hatua ya kujiona hana thamani kwa mwanaume yeyote sababu ya matusi, kejeli na yote uyajuayo,....halafu akatokea mwanaume akamfariji, akampa matumaini, akapata amani...furaha, na matumaini angalau kwa muda mchache anaokuwa nje ya nyumba yake...

JE? Unadhani ni rahisi kwa mwanamke huyo kumsahau huyo mfariji wa maisha yake kipindi kile cha dhiki na majuto makuu? Unaukumbuka msemo, 'aliyeumwa na nyoka?....' unaamini mwanamke huyu baada ya haya yote, hana kovu moyoni mwake ambalo hapaswi kukumbukia aliyofanyiwa?....

Mkuu Mbu hapa ndipo mimi huwa natanabaisha wazi kuwa mahawala siku zote hawaachani.
Lakini huyo mwanamke kwa vile hataki au anaona ugumu kujivua gamba kwa mshefa na huyo mshefa nae hataki kumwacha mke wa mtu huku nae akiwa na mke wake nyumbani yawezekana huyo mke wa mshefa nae ana matatizo sawa na mme wa huyo mwanamke ndugu wa MJ1. Sasa basi mimi nasemaje kwa vile hawa wanao ngonoka kwa kujificha mshefa na huyo jamaa wakae wakubaliane wawekane wazi kuliko kuharibiana ndoa. Kama wanapendana kwa dhati basi wavunje ndoa zao za awali waungane wawe kitu kimoja.
Mi naona huyo mshefa amemgeuza huyo mwanamke kama kipozeo pindi anakutwa na hamu kama kweli anampenda amwambie wazi amwache mke wake na huyu mama nae aombe talaka kwa mmewe waishi pamoja kwa raha si nyota zao zinaendana? Zaidi zaidi wanaharibiana tu.
 
kuna kitu kuhusu cheating....inayofanya iwe tamu sana...

1.kwanza ni siri
2.hupati enough kwa sababu lazima urudi kwako..
3.hakuna kuboana wala kuchungana....
4.mnapokutana wote mnakuwa na kiu...
 
Hii ndoa haipo...................wanajisumabua bure; hawatakaa warudie kwenye mstari believe me!
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Good one Mbu

Let me tell you some... Sijawahi kusikia mahusiano yasiyokua na abuse, adn you know why?? because we have different thresholds and kibaya zaidi malezi tofauti and definition ya abuse ni very wide

Hakuna mwanaume ambaye hajawahi kuwa abused kwenye relationship vivyo hivyo wanawake...the only challenge we have ni how we communicate these abuse to societies around us

Pili, hakuna anayeamua ku-cheat akashindwa, and 99% huchukulia abuse kama sababu... hint, sikiliza wanaume wanaocheat wanavyoongelea mahusiano yao na hao "lovers wa nje"

Once you start cheating, there is no way you will be able to stop completely in a lifetime, because utakua umeprove kwamba IT IS DOABLE!!

LASTLY, in a country like Tanzania, with all these hard knock life na makundi yetu ya kudanganyana... cheating could be as high as 90% kwa walio kwenye mahusiano

MUACHE HUYO DADA ALE MAISHA, NATURAL COURSE ITAKUJA ILI YAISHE

Well said....hata mshefa akichukua jumla, lazima huyu mama atafute a new version of mshefa...they do it the way we do it! and nowadays they even do it better....
 
kuna kitu kuhusu cheating....inayofanya iwe tamu sana...

1.kwanza ni siri
2.hupati enough kwa sababu lazima urudi kwako..
3.hakuna kuboana wala kuchungana....
4.mnapokutana wote mnakuwa na kiu...

siri inaongezaje utamu?
kwa nini usijilie ukasaza tu nyumbani kwako maana ni vyako kuliko kwenda kuneng'eneka milango ya wenyewe?
kuboaba na kuchungana? hizo ni spece tu za mapenzi uchungwe wee mbuzi?
hiyo kiu nyumbani huwezi kunywa maji ya kutosha ukaimaliza? tena maji chaguo lako, ukitaka ya mtungi, ya bilauri. ya ndoo, ya uhai, unajichagulia tu hadi yalowekwa water guard yapo.
 
only men can understand what i said.....
 
Back
Top Bottom