Wapendwa WanaJF.
Natumaini wote mu wazima........naombeni msaada wa namna ya kushauri.
Ni rafiki yetu kifamilia, kwa muda mrefu yeye na mumewe wamekuwa kwenye migogoro ya hapa na pale ya kindoa. Kusema ukweli mumewe amekuwa akimis-behave kwa kipindi ikiwemo kucheat, physical abuse and the like. Mke akawa anaumia, anaconfront wanagombana.. After a while mgogoro ule ukapungua (ile frequency ya wao kuja kushtaki kwetu kesi zao ukapungua na mwisho kuisha kabisa- wadau tukakaa na kumshukuru MUNGU juu ya wokovu huu maana hali ilipokuwa inaelekea ilikuwa inatishia uhai wa ndoa ile).
Juzi kanijia huyo mke ananomba ushauri kama mwanamke mwenzie. Akatoa siri ya mafanikio 'amani' ya miujiza iliyotawala kwenye ndoa yake kwa kipindi kile. Alisema alikujaamua kuwa 'mpole' asimfuatilie mumewe wala asijihangaishe naye....alitafuta 'mshefa' wa pembeni naye akawa anajilia raha kwa nafasi!!!....sikuamini lakini kutokana na matatizo aliyokuwa nayo kipindi kile nadhani nilimwelewa ingawa sikuafiki.
Sasa anadai mumewe amejirekebisha sana na amebadilika na kuwa 'mume' tatizo liko kwake amejikuta amedevelop hisia kali za mapenzi kwa 'Mshefa' kuliko kwa mumewe na kila akijaribu kumuacha huyu jamaa anashindwa maana anasindwa kujicontrol kabisa. Not only that hata 'Mshefa' huyo hana dalili za kumsaidia 'kurudi' kwa mumewe kihisia kwani kila mara anakuwa kama anamblackmail vie kuwa anampenda na eti somehow huyu mwanamke amesababisha kutokuelewana flani kati yake yeye 'Mshefa' na mkewe nyumbani kwake. So kila mdada akijaribu kumuacha 'Mshefa' mshefa anakuja juu kimapenzi yaani anachochea vile.
Mdada anasema mumewe alishagundua juu ya cheatignyake lakini akamsamehe baada ya mke kukiri na kuapa kuacha. Ila sasa ndo anashindwa kihisia yuko kwa 'Mshefa' zaidi ya mumewe. Anaomba msaada afanyeje a'rudishe' mapenzi na hisia kwa mumewe??
Amekiri kuwa alifanya kosa na anajutia kutafuta 'faraja' nje ya ndoa.
Naombeni tumsaidie .....Nitawaacknowledge msijali