Arusha: Afariki baada ya kuingia kwenye kisima chenye mita 60 kumtoa mbuzi

Arusha: Afariki baada ya kuingia kwenye kisima chenye mita 60 kumtoa mbuzi

Elimu Elimu Elimu muhimu yani nikiwaza metre moja ni kama futi tatu na cm 10 halafu mtu aniambie nidumbukie kwenye shimo la mita 60 kisa sh. Elfu 40 nachoka mimi 🤣🤣🤣!!!

Yani 200Feet deep down kwa 40k kuokoa maisha ya mbuzi... likely huyo mzee aliekubali offer ni type ya wale waokota makopo wanywaji wa visungura 24/7.
 
Umaskini mbaya nyie, hapo alipiga hesabu ya 40k yake akifanikisha imsaidie matumizi😪

Huyo mwenye mbuzi pia amekosea kwa huo umbali angempotezea tu huyo mbuzi, asingeruhusu watu waingie kumtoa,ila basi ajali kazini🤔
Hahahahah wanasema kisima kina majini🤣 ndo maana jamaa kafeli kutoka kaliwa na jini😂
 
Umekunywa shimha na jobo mixer kisungura afu umeshushia na ugoro afu unataka uzame kwenye kina kirefu cha maji!! NOTE: Kazi ilikuwa inafanywa na watu watano kwa malipo ya tsh 40 elfu hivyo kila mmoja angepata elfu 8 kwa kazi hatari kama hiyo.Umaskini mbaya sana
 
Mtu mmoja anayefahamika kwa jina Mbaruku mussa anayekadiriwa kuwa na miaka 47 makazi wa mtaa wa olmoti kata ya olimoti mkoani Arusha anahofiwa kufariki baada ya kudaiwa kupewa Dau la fedha shilingi elfu arobaini (40) kuingia katika kisima cha maji chenye mita zaidi ya 60 kwenda kumtoa mbuzi aliyedumbukia humo.

Viongozi pamoja na wananchi wanadia kuwa wameweka kambi kwa siku ya tatu hadi hii leo wakiwa na askari wa jeshi la zimamoto na uokoaji kwa ajili ya kuokoa lakini hadi hii leo imeshindikana

“Walikuja vijana watano ambao walizama kwenye shimo kwa shilingi elfu arobaini lakini baadaye ilitokea kishindo katika kisima yule bwana kuchungulia tukakuta ameshadumbukia kwenye kisima nikawaambia wavute kamba ikarudi yenyewe,walikubaliana watamtoa huyo mbuzi kwa elfu 40 ndio wakazama kwenye kisima,baada ya tukio wengine wakakimbia”Chacha Joseph -Shuhuda

Kwa upande wa jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Arusha wamefika eneo la tukio na kuendelea na jitihada za uokozi lakini hadi Ayo Tv inaondoka eneo la tukio hawakuweza kufanikiwa

View attachment 3203798
Mtumbukizeni ndani ya kisima askari wa uokoaji ili akaandae kwanza mikakati ya kumuokoa mbuzi.
 
Duuuuu
 
“Walikuja vijana watano ambao walizama kwenye shimo kwa shilingi elfu arobaini lakini baadaye ilitokea kishindo katika kisima yule bwana kuchungulia tukakuta ameshadumbukia kwenye kisima "SIJAELEWA HAPA"
Mkuu
Unaifahamu tume ya mipango veve?
Hizi issue zinaandaliwaga kitaalam kututoa mchezoni
 
Wanawake tukumbuke kuwaombea waume zetu wanapotoka,na pia tujifunze kuwashukuru kwa wanacholeta.

Pole kwa familia na ndugu.
Mwanaume ukiwa huna hela mwanamke anakuona tàkataka tuu.
 
Back
Top Bottom