Tetesi: Arusha: Aliyehama Kutoka CHADEMA na Kwenda CCM Afukuzwa kwenye Nyumba na Kanisani Waumini Wamkimbia


Mkuu siku nyingine ukija Arusha tutafutane, mbali na siasa watu wa Arusha pia ni wakarimu...ila ukiingia ulingoni kwa masuala yahusuyo siasa uwe smart enough.
 
Hakuna watu wahuni kama ccm wakishamnunua mtu ....kwanza pesa wanatoa advance ya kumalizia wanaila , na baada ya hapo hawana mpango na wewe ..huyu mchungaji ," apambane na hali yake" ....mapenzi yalikuwa mazito kabla hajapanda pale jukwaani ....kwa sasa watamkimbia kama mimba !!!
Ukizingatia nao biashara haijawalipa baada ya kuliwa pesa na piki piki zao na zaidi ya vijana 500 waliowaahidi kuwa nao wangehamia ccm kwa mafuriko!!!!
 
CHADEMA bhana kwahiyo mnafurai sana ..Hivi bado mpoNairobi
 
kwani kudaiwa ni dhambi? Nchi inadaiwa itakuwa individual?? Siasa uchwara kwanini alipokuwa Chadema mbona hukuandika kuwa anadaiwa?? Deni limejulikana baada ya kuhama Chadema??!!
 
Ameanza kuisoma Namba mapema!! Kwanza Hafai kua kiongozi Hana Miiko ya Ungozi
 
Hopeless kwani kudaiwa ni dhambi? Nchi inadaiwa itakuwa individual?? Siasa uchwara kwanini alipokuwa Chadema mbona hukuandika kuwa anadaiwa?? Deni limejulikana baada ya kuhama Chadema??!!
Acheni kulialia msaidieni pa kulala
 
hivi mimi ni Chadema au Ni Mwanahabari Huru? kazi yangu ni Kuhabarisha karibu officini kwangu niko Mwembe yanga kiongozi "Mwanahabari Huru"
Wewe ni Chadema acha uongo ni mwanahabari wa Chadema wala usikatae!
 
Mkuu, usicheze na CCM. Umesahau wale madiwani wa Kilimanjaro walivyoingizwa mjini? Pesa ziliingizwa kwenye akaunti zao, wakaja Lumumba Dsm wakapokelewa na Polepole. Baada ya shughuli mmoja wao akaenda benki kuchota za kwenda kujipongeza hapa jijini akakuta zote zimetolewa. Alipouliza benki, akaambiwa benki imejulishwa kwamba pesa hizo ziliingizwa kimakosa.

Namshangaa huyo Diwani aka Mchungaji kwa kuingia mkenge huo. Wanajamvi wanahoji kwa nini asilipe pesa alizohongwa? Jibu ni kwamba CCM haitoi pesa. Ni usanii kwa kwenda mbele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…