Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,509
- 3,756
Aliyekuwa Mgombea katika nafasi ya Ujumbe wa Serikali ya Mtaa ya eneo la Mnara wa Voda, kupitia CHADEMA kabla ya Chama hicho hakijajitoa kushiriki, Sirili Homary amekutwa amefariki dunia nyumbani kwake huku akidaiwa kukatwa na kitu chenye ncha kali shingoni
Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jonathan Shana, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kifo hicho kina muda wa siku tatu tangu kimetokea.
Amesema Marehemu Homary amekutwa ndani ya nyumbani kwake katika eneo la Mnara wa Voda, huku funguo ikiwa ndani akiwa amefariki Dunia.
“Bado tunachunguza na tutatoa taarifa maana mtu amekutwa ndani na funguo ikiwa ndani inawezekana pia amejidhuru mwenyewe kutokana na labda msongo wa mawazo” amesema Shana.
Aidha amesema wako wanasiasa wanaleta uchochezi juu la kifo hicho na ameahidi wakiendelea atawachukulia hatua kwa mujibu wa sheria.
“Naomba watupe muda vyombo rasmi vya uchunguzi vifanye kazi yake, jambo kama hilo lina taratibu linapotokea tunachunguza kwa kuhusisha vyombo vinavyoaminiwa na wananchi na tutatoa taarifa kupitia Vyombo vya Habari”amesema Shana.
Naye Mbunge wa Arusha, Godibless Lema akihojiwa na Nipashe, amesema jambo hilo ni la kikatili na la kuhuzunisha na kwamba amezungumza na Kamanda wa Polisi mkoani humo ambaye amemuambia watu kadhaa wanashikiliwa kuhojiwa juu ya tukio hilo.
Amesema CHADEMA mkoani Arusha wameunda Kamati Maalum kufuatilia Mauaji hayo maana yana utata kwani Homary ni Kada Maarufu na mwaminifu wa Chama hicho.
“Sio kawaida kwa polisi kukaa kimya hapa kuna utata, RPC alipaswa aite kikao na wanahabari na waulize majibu na ajibu sasa ukimya huu unatushangaza maana jamii itapata picha gani?”amehoji Lema.