Arusha: Ally Bananga arudi CCM kwenye mkutano wa Rais Samia Suluhu

Aliyekuwa diwanu na mjumbe wa kamati kuu ya Chadema Ally Bananga amerejea CCM leo jijini Arusha.

Bananga ameomba msamaha kwa Rais Samia na wanaccm wote kwa mambo yote ya hovyo aliyowafanyia akiwa Chadema.

Source: ITV
Mbona mke wake hajatambulishwa na yeye?
 
Kumfukuza kungewapa kiki nyie kwamba mko makini

Sasa hivi hata mkisema mlikuwa manajua mnaonekana mnatapatapa tu
 
Na alafu hiyo ya chama chako kuchukua watu toka chama usichokipenda ndio kinafanya muendelee kubaki hapo mlipo na kuishi kwa stress
 
Jamani sitaki tena kumwamini mwanasiasa yeyote! Kila mtu aamue ki-vyake! Litakuwa linanyemelea uteyuzi! Liwaache akina johnthebaptist wanang'aa sharubu tu!

Sasa ulitaka abakie chadema anafanya nn?
 
Hivi hizi siasa za kikahaba zipo bongo peke yake? maana kule majuu kusikia republican kahamia democrats au kinyume chake inaweza kutafsiriwa kama maajabu ya dunia. Yaani leo hii uwasikie Trump na Bush wamehamia democrats, au Clinton, Obama, Biden wamenunuliwa na republicans.....inavyoonekana wanasiasa kwenye nchi za mbele wanaamini sana katika itikadi za vyama vyao kinyume cha wanasiasa wa bongolala wanaoamini katika itikadi ya tumboni....
 
Kwani waliobaki wanafanya nini?

Hawana kitu wanafanya
Sasa chama hakishiriki uchaguzi chama Kipo Tu kimekaa kama sufuria jikoni

Absolutely mtu mwenye plan zake mzuri za kisiasa hawez kukaa chadema
 
Wale watu wamejengwa kwenye uzalendo na siyo njaa kama sisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…