Arusha: Barabara ya muhimu kama hii inakosaje Lami?

Arusha: Barabara ya muhimu kama hii inakosaje Lami?

Kweli Kaskazin hawana shukurani!
Hv mnajua Kigoma mpaka Leo haijaungwa na mtandao wa barabara ya lami?
Mbeya kwenda Tabora na Singida kupitia Chunya hamna lami na hiyo barabara ni shortcut ya kutoka Nyanda za juu Kusini kwenda Kanda ya kati, Magharibi na Kanda ya ziwa!
Watu wanalala njiani!
Sasa hicho kiuchochoro Kuna magari yanalazimika kula njiani?
Acheni ubinafsi

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
halmashaur ya meru ndo wenye jukumu Hili apo n wananch na madiwan wake pamoja na mkuu wa wilaya
 
Siyo Lema?Bali ni magufuli??
Magufuli alisema mwenyewe wakitoa wapinzania mambo ya takuwa mazuri. Ajabu hata barabara ya mianzini aliyoahidi lami kwenye mkutano wa hadhara hadi leo hamna kitu
 
Hii barabara ni ya vumbi Inatokea Tengeru kupitia chuo cha mifugo kuelekea mbuguni.

Barabara hii hiyo inapita katika taasisi ya Tari hot Tengeru. Na pia inapita katika chuo cha Maendeleo ya jamii (TICD) na chuo cha mifugo cha Tengeru,bila kusahau kuwa bara bara hii ndio inayopita katika chuo cha kimataifa cha Nelson Mandela,na kuelekea hadi mbuguni.

Kwa jiji kama hili ambalo limepewa hadhi ya kuwa jiji tangu miaka mingi miundombinu mingi ni bado sana maana barabara zenye Lami ni chache kulinganisha na zile ambazo hazina lami.

NawasilishaView attachment 2024645
Siyo barabara hii tu, ukweli Arusha yote barabara ni za hivyo. Wanashindwa hata na Moshi. Jiji halijengi barabara kabisa. Sijui viongozi wa jiji na mkoa wanafanya kazi gani.

Barabara zote za mitaa ni vumbi/matope, ujenzi holela ndiyo usiseme. Wao wakiona unajenga wanakuja kutaka uwape hela ukiwapa hawajali kama unajenga kiholela au kwa kufuata mipango. Ilimradi hela wameshachukua.
 
Ni AIBU na Sio hiyo tu, kuna barabara ya Ilboru yaani kutoka barabara kuu ya Ars - Moshi kuna barabara inaelekea Ilboru High School, shule kongwe iliyotoa viongozi wakubwa serikalini including Mwigulu Nchemba haina lami

Na ukiangalia ni kilometer chache sana kama 2 ai 2.5 kutoka highway.

Mh. Mwigulu Nchemba, Frederick Sumaye na wengine ikumbukeni shule yenu kwa kusisitiza uwekaji barabara kwasababu hatahivyo watu wameshabomoa nyumba zao na kutenga eneo la barabara bado tu ujenzi.
 
Ni ajabu Sana mkuu nilikuwepo pale Tengeru ,,nyuma ya kambi ya jeshi ,,,then mbele unakuta shule ya Sekondari ya Kikwe kulekea Mbuguni ..Mererani ....

Ukiambiwa hiyo road inakwenda mgodini Tena mgodi wa Taifa unaweza kushangaa....

Hawana mpango wa kuweka lami kabsa..
Umenikumbusha mbali sana. Vip kijiji cha Kikwe umeme umefika?
 
Kwani Lema anasemaje ? Si alikuwa mbunge pale miaka 10
Hii barabara ni ya vumbi Inatokea Tengeru kupitia chuo cha mifugo kuelekea mbuguni.

Barabara hii hiyo inapita katika taasisi ya Tari hot Tengeru. Na pia inapita katika chuo cha Maendeleo ya jamii (TICD) na chuo cha mifugo cha Tengeru,bila kusahau kuwa bara bara hii ndio inayopita katika chuo cha kimataifa cha Nelson Mandela,na kuelekea hadi mbuguni.

Kwa jiji kama hili ambalo limepewa hadhi ya kuwa jiji tangu miaka mingi miundombinu mingi ni bado sana maana barabara zenye Lami ni chache kulinganisha na zile ambazo hazina lami.

NawasilishaView attachment 2024645
 
Tuseme tu, kwa namna hii,haikupaswa kabisa kabisa Arusha kuitwa jiji.Barabara ya muhimu namna hii kukosa lami ni aibu.Najua pia kuna watalii wengi hupita kupata malazi serena hotel iliyopo katikati ya soko la tengeru na Chuo cha mifugo na kuona ziwa Duluti.Pia hupitisha watalii kwenda kuona makaburi ya mababu zao waliozikwa eneo hili karibu na Chuo Cha Maendeleo ya Jamii.

Lakini isitoshe, wakazi wa Mianzini Mataa kupandisha kwenda Ilboru Lodge kuna kipande kama mita 100 ambacho hakina lami.Baada ya mita kama 100 hivi kutokea Msikitini barabara ina lami km.2

Sasa hiki kipande kifupi hapa ni cha nani,Arumeru au Manispaa ya Arusha mjini.Mbona kina muda mrefu karibu mwaka wa 5 hakina lami.

Wananchi tumeshindwa kuelewa tena kwa bahati mbaya sana Meya wa jiji la Arusha ni wa eneo hilo na huwa anapita mara kwa mara.Ni mara nyingi maji yamekuwa yakifunguliwa kwenye barabara hii ambayo haina mitaro.Tumeripoti kwake kama mtendaji bila utekelezaji wowote.Nilimpigia simu siku moja kuripoti hilo,akaniambia yuko kwenye kikao Dodoma.Lakini ilinishangaza baada ya masaa machache nilimwona mjini.Labda alirudi haraka kwa ndege.

Mambo ya mabarabara haya na usanii wake yapo mengi hapa Arusha.Ila wakazi wa Mianzini nadhani wanasubiri makaratasi ya kusimama foleni hiyo sijui ndiyo 23 mtu apigwe chini kumaliza usanii.
Huyo meya mlaumu kwa mengine lakini si hili la uongo wa majibu ya simu!

Hiki kikombe cha uongo wa kujibu simu, karibu kila mmoja wetu alishakinywea tangia teknolojia ya simu kuingia.

Tena hasa wewe mkuu, unapenda sana kuwajibu watu uongo hasa ukiwa juu ya tuta.."nipo kwenye kikao, subiri nikimaliza ntakupigia"... kumbe unafanya yako na ukimaliza haumpigii huyo mtu, mpaka akutafute tena kwa muda wake!

Tuwe wakweli watu tu waongo sana kwenye kujibu simu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi kama mdau wa Livestock Training Institute- Tengeru, sikubaliani na hiyo Barbara kuwekwa lami kwani itazuia mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa taasisi hiyo kwani hawataruhusiwa kupitisha mifugo Yao kwenye lami.
 
Nilikuwa natafuta hii comment..Nami nilisikia kwamba hiyo barabara sio official, ilikuwa kwa ajili ya kupitisha mifugo na ndio maana haiwekwi lami.
 
Mkuu wakati unapiga hizi pic nilikuona mana ulinipita pale gate la sokoni kilindi pale
 
Tuseme tu, kwa namna hii,haikupaswa kabisa kabisa Arusha kuitwa jiji.Barabara ya muhimu namna hii kukosa lami ni aibu.Najua pia kuna watalii wengi hupita kupata malazi serena hotel iliyopo katikati ya soko la tengeru na Chuo cha mifugo na kuona ziwa Duluti.Pia hupitisha watalii kwenda kuona makaburi ya mababu zao waliozikwa eneo hili karibu na Chuo Cha Maendeleo ya Jamii.

Lakini isitoshe, wakazi wa Mianzini Mataa kupandisha kwenda Ilboru Lodge kuna kipande kama mita 100 ambacho hakina lami.Baada ya mita kama 100 hivi kutokea Msikitini barabara ina lami km.2

Sasa hiki kipande kifupi hapa ni cha nani,Arumeru au Manispaa ya Arusha mjini.Mbona kina muda mrefu karibu mwaka wa 5 hakina lami.

Wananchi tumeshindwa kuelewa tena kwa bahati mbaya sana Meya wa jiji la Arusha ni wa eneo hilo na huwa anapita mara kwa mara.Ni mara nyingi maji yamekuwa yakifunguliwa kwenye barabara hii ambayo haina mitaro.Tumeripoti kwake kama mtendaji bila utekelezaji wowote.Nilimpigia simu siku moja kuripoti hilo,akaniambia yuko kwenye kikao Dodoma.Lakini ilinishangaza baada ya masaa machache nilimwona mjini.Labda alirudi haraka kwa ndege.

Mambo ya mabarabara haya na usanii wake yapo mengi hapa Arusha.Ila wakazi wa Mianzini nadhani wanasubiri makaratasi ya kusimama foleni hiyo sijui ndiyo 23 mtu apigwe chini kumaliza usanii.
Ina umuhimu gani hiyo barabara?

Acheni ushamba, kuna barabara muhimu kuliko hiyo lakini bado hazina lami
 
Back
Top Bottom