Arusha: Barabara ya muhimu kama hii inakosaje Lami?

Kweli Kaskazin hawana shukurani!
Hv mnajua Kigoma mpaka Leo haijaungwa na mtandao wa barabara ya lami?
Mbeya kwenda Tabora na Singida kupitia Chunya hamna lami na hiyo barabara ni shortcut ya kutoka Nyanda za juu Kusini kwenda Kanda ya kati, Magharibi na Kanda ya ziwa!
Watu wanalala njiani!
Sasa hicho kiuchochoro Kuna magari yanalazimika kula njiani?
Acheni ubinafsi

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
halmashaur ya meru ndo wenye jukumu Hili apo n wananch na madiwan wake pamoja na mkuu wa wilaya
 
Siyo Lema?Bali ni magufuli??
Magufuli alisema mwenyewe wakitoa wapinzania mambo ya takuwa mazuri. Ajabu hata barabara ya mianzini aliyoahidi lami kwenye mkutano wa hadhara hadi leo hamna kitu
 
Siyo barabara hii tu, ukweli Arusha yote barabara ni za hivyo. Wanashindwa hata na Moshi. Jiji halijengi barabara kabisa. Sijui viongozi wa jiji na mkoa wanafanya kazi gani.

Barabara zote za mitaa ni vumbi/matope, ujenzi holela ndiyo usiseme. Wao wakiona unajenga wanakuja kutaka uwape hela ukiwapa hawajali kama unajenga kiholela au kwa kufuata mipango. Ilimradi hela wameshachukua.
 
Ni AIBU na Sio hiyo tu, kuna barabara ya Ilboru yaani kutoka barabara kuu ya Ars - Moshi kuna barabara inaelekea Ilboru High School, shule kongwe iliyotoa viongozi wakubwa serikalini including Mwigulu Nchemba haina lami

Na ukiangalia ni kilometer chache sana kama 2 ai 2.5 kutoka highway.

Mh. Mwigulu Nchemba, Frederick Sumaye na wengine ikumbukeni shule yenu kwa kusisitiza uwekaji barabara kwasababu hatahivyo watu wameshabomoa nyumba zao na kutenga eneo la barabara bado tu ujenzi.
 
Umenikumbusha mbali sana. Vip kijiji cha Kikwe umeme umefika?
 
Kwani Lema anasemaje ? Si alikuwa mbunge pale miaka 10
 
Huyo meya mlaumu kwa mengine lakini si hili la uongo wa majibu ya simu!

Hiki kikombe cha uongo wa kujibu simu, karibu kila mmoja wetu alishakinywea tangia teknolojia ya simu kuingia.

Tena hasa wewe mkuu, unapenda sana kuwajibu watu uongo hasa ukiwa juu ya tuta.."nipo kwenye kikao, subiri nikimaliza ntakupigia"... kumbe unafanya yako na ukimaliza haumpigii huyo mtu, mpaka akutafute tena kwa muda wake!

Tuwe wakweli watu tu waongo sana kwenye kujibu simu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi kama mdau wa Livestock Training Institute- Tengeru, sikubaliani na hiyo Barbara kuwekwa lami kwani itazuia mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa taasisi hiyo kwani hawataruhusiwa kupitisha mifugo Yao kwenye lami.
 
Mimi kama mdau wa Livestock Training Institute- Tengeru, sikubaliani na hiyo Barbara kuwekwa lami kwani itazuia mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa taasisi hiyo kwani hawataruhusiwa kupitisha mifugo Yao kwenye lami.
Nilikuwa natafuta hii comment..Nami nilisikia kwamba hiyo barabara sio official, ilikuwa kwa ajili ya kupitisha mifugo na ndio maana haiwekwi lami.
 
Mkuu wakati unapiga hizi pic nilikuona mana ulinipita pale gate la sokoni kilindi pale
 
Ina umuhimu gani hiyo barabara?

Acheni ushamba, kuna barabara muhimu kuliko hiyo lakini bado hazina lami
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…