Mpaji Mungu
JF-Expert Member
- Apr 24, 2023
- 13,544
- 43,537
Gomeni mwaka mzima muone kama wasafiri tutakwama wapuuzi kabs! Walitusumbua sana kipindi hiko yaan kidala seat level 15 wao wanabeba 27, tena bajaj ziongezeke zaidi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sahihi kabisaSiasa zimerahisisha Mambo, sheria zote zinakanyangwa, Sasa tuone Serekali itasimamia wapi!? Bajaji ni on request na Sio public transport
Watu wa bajaji ilitakiwa wawe wanatoa abiria uko ndani na kuwasogeza stendi za daladala au ziwe zinapaki kwa ajili ya kukodishwa sasa kwa sasa hawa bajaji wamekuwa kama daladala, nakumbuka huko nyuma mgomo kama huu ulishawai tokea mbeya ufumbuzi wa tatizo ulipatikana nashauri watu wa arusha wajifunze huko mbeya
Sent from my vivo 2015 using JamiiForums mobile app
Wajifunze tu ya moahi ,kwa sasa amna dalala zinazoenda kcmc mambo ya bajajiKwa mara nyingine tena daladala zote zinazoenda katikati ya jiji. zimegoma kufanya biashara ikiwa ni mgomo wa pili ndani ya kipindi kisichozidi mwezi na nusu.
Mussa njuga ambae ni katibu wa daladala amesema mgomo huo hauna kikomo hadi wapate kauli kutoka kwa waziri Mkuu au Makamu wa Rais.
Sababu za mgomo huo inatajwa ni Serikali kushindwa kufikia muafaka kati yao na Bajaji kwa kuruhusu Bajaji kufanya kazi kama daladala ndani ya Jiji la Arusha
Uongozi huo umeeleza kuwa mbali na kuandika barua kwa mkuu wa mkoa kuikumbusha Serikali kutekeleza maadhimio ya vikao vya kamati ya suluhu lakini barua hiyo haikupatiwa majibu jambo ambalo limewakatisha tamaa madereva na viongozi wao.
Aidha viongozi hao wanataka kauli kutoka kwa waziri Mkuu Au makamu wa Rais kwa madai kuwa viongozi wa Arusha wameshindwa kutekeleza madai yao.
Zaidi ya Bajaji 2500 zinafanya kazi ndani ya jiji la Arusha kama daladala.
=============
LATRA YASEMA MGOMO UKIENDELEA WATAFUTA LESENI ZA DALADALA
Joseph Michael, Afisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Mkoa wa Manyara anazungumzia kinachoendelea:
Tunasikitika kitendo cha Daladala kufanya mgomo kwa kuwa tayari Serikali inafanyia kazi suala hilo chini ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye alishaunda Kamati inayohusisha watu wa Bodaboda, Daladala, Bajaj, Barabara na taasisi za Serikali zinazohusisha masuala ya Usafirishaji.
Kamati iliundwa maalum kufuatilia suala hilo na ilishamaliza kazi yake, kilichokuwa kinafuata ni kwenda kwenye hatua ya pili ya utekelezaji, kinachoshangaza wamefanya mgomo wakati wao watu wa Daladala wana wawakilishi wao kwenye Kamati.
Tunashauri warejee kutoa huduma na Kamati iendelee kutoa mchakatoa, mgomo una madhara, waliendelea hivyo Sheria inaeleza kuwa tutafuta leseni.
Nimeenda kuzungumza nao watu wa Daladala pale Kilombero Kituoni, inavyoonekana Wanachama wa Daladala hawawaheshimu viongozi wao wanaowawakilisha, kwenye umoja wao huo kuna shida.
Pia tumeruhusu Coaster za Arusha – Moshi zianze kufanya kazi wakati huu wa mgomo huku tukiwasisitiza watu wa Daladala wasitishe mgomo, wafuate Sheria na Taratibu kwa kuwa wakiendelea hivyo tutafuta leseni zao, tupo ‘serious katika hilo.
Utafikiri sio jiji bana 😅Vidaladala vyenyewe vipanya full mbanano. jirekebisheni hapo kwanza
Subutuuuuuu labda 2800 hukoooooooTuunganishie hapo na mambo ya dp world.
Wanaoteseka Wanafunzi ambao ndo wengi kuliko wazazi.Wakumbuke kuwa kabla ya daladala kulikuwepo na coaster.... coaster hazikuzuia daladala kufanya kazi , zilijiongeza na kuanza safari ndefu badala ya kuung'ang'ania kufanya safari fupi fupi hapo mjini. Kama daladala hawawezi kuwa na adabu kuruhusu biashara huria wakauze gari zao wanunue bajaji... Pumbavu kabisa.
Sent from my Infinix X6517 using JamiiForums mobile app
Msitafutane uchawi bure huo mji ni mdogo hauwezi kuhimili dalala vibajaji na pikipiki lazima mmoja atolewe knockout.Kwa mara nyingine tena daladala zote zinazoenda katikati ya jiji. zimegoma kufanya biashara ikiwa ni mgomo wa pili ndani ya kipindi kisichozidi mwezi na nusu.
Mussa njuga ambae ni katibu wa daladala amesema mgomo huo hauna kikomo hadi wapate kauli kutoka kwa waziri Mkuu au Makamu wa Rais.
Sababu za mgomo huo inatajwa ni Serikali kushindwa kufikia muafaka kati yao na Bajaji kwa kuruhusu Bajaji kufanya kazi kama daladala ndani ya Jiji la Arusha
Uongozi huo umeeleza kuwa mbali na kuandika barua kwa mkuu wa mkoa kuikumbusha Serikali kutekeleza maadhimio ya vikao vya kamati ya suluhu lakini barua hiyo haikupatiwa majibu jambo ambalo limewakatisha tamaa madereva na viongozi wao.
Aidha viongozi hao wanataka kauli kutoka kwa waziri Mkuu Au makamu wa Rais kwa madai kuwa viongozi wa Arusha wameshindwa kutekeleza madai yao.
Zaidi ya Bajaji 2500 zinafanya kazi ndani ya jiji la Arusha kama daladala.
=============
LATRA YASEMA MGOMO UKIENDELEA WATAFUTA LESENI ZA DALADALA
Joseph Michael, Afisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Mkoa wa Manyara anazungumzia kinachoendelea:
Tunasikitika kitendo cha Daladala kufanya mgomo kwa kuwa tayari Serikali inafanyia kazi suala hilo chini ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye alishaunda Kamati inayohusisha watu wa Bodaboda, Daladala, Bajaj, Barabara na taasisi za Serikali zinazohusisha masuala ya Usafirishaji.
Kamati iliundwa maalum kufuatilia suala hilo na ilishamaliza kazi yake, kilichokuwa kinafuata ni kwenda kwenye hatua ya pili ya utekelezaji, kinachoshangaza wamefanya mgomo wakati wao watu wa Daladala wana wawakilishi wao kwenye Kamati.
Tunashauri warejee kutoa huduma na Kamati iendelee kutoa mchakatoa, mgomo una madhara, waliendelea hivyo Sheria inaeleza kuwa tutafuta leseni.
Nimeenda kuzungumza nao watu wa Daladala pale Kilombero Kituoni, inavyoonekana Wanachama wa Daladala hawawaheshimu viongozi wao wanaowawakilisha, kwenye umoja wao huo kuna shida.
Pia tumeruhusu Coaster za Arusha – Moshi zianze kufanya kazi wakati huu wa mgomo huku tukiwasisitiza watu wa Daladala wasitishe mgomo, wafuate Sheria na Taratibu kwa kuwa wakiendelea hivyo tutafuta leseni zao, tupo ‘serious katika hilo.
Sasa bajaji nao wapakie wanafunzi kwa 200 sio wanaachia wanafunzi daladalaHuo ni unyimi na roho mbaya waache watu watafute pesa mbona Morogoro bajaji na daladala wanapiga ruti moja na husikii kulalamika
Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app