Arusha: Daladala zagoma tena Arusha, leo Agosti 14, 2023


Mbeya walisitisha usajili wa bajaji baada ya kuona zimekuwa kelo...., Kinachofanyika Sasa bajaji ikichoka unauza usajili.

Ilo swala Ni gumu na limekaa kimaslahi kwa Mbeya ili sumbua kwakuwa miongo mwa viongozi wa juu wa mkoa walikuwa wanamiliki/wanamiliki Hadi sasa bajaji zaidi ya 30 Kila mmoja Sasa hapo unategemia watakubali kuondoa bajaji barabarani mkuu?
 
Ndugu wana Arusha na watanzania wote kwa ujumla mkuu wa mkoa wa Arusha, mkurugenzi na mamlaka husika za usafiri walipaswa wawe waneshatumbuliwa mpaka sasa kutokana kushindwa kutatua mgomo uliopo wa magari ya usafirishaji ulioleta adha kwa wananchi mara ya pili sasa ndani ya muda mfupi.

Hali ni mbaya na hatari kwa aina ya usafiri unaotumika sasa,tena kwa watoto wadogo wa shule na wananchi kwa ujumla

Wawe wamejiuzulu mpaka sasa au mama yetu Samia wafukuzwe wahusika wote kabla siku hizi ya leo haijaisha
 
Wajifunze tu ya moahi ,kwa sasa amna dalala zinazoenda kcmc mambo ya bajaji
 
Ila nawasifia watu wa daladala wa Arusha wana msimamo siku nzima wamekaza.
Ila waache uduanzi bodaboda nao wanatafuta riziki waende kula na kuhonga wapunguze genye.
 
Hapa ndipo akili za madereva hasa wa daladala huwa nashindwa kuzielewa.Utawakataaje watu wanaotafuta riziki kama wewe tu?Hizi siyo zama za ujima kwamba usafiri uwe wa aina moja tu.Watu wana haraka zao na wanataka privacy.Daladala hujaza abiria wengi na kuwabananisha.Watu wengi hawapendi.Ni uchumi mfinyu tu.
 
Tatizo la daladala za Arusha hawaoni mbele zaidi kwamba route fupi lazima zitakufa kama ambavyo kwenye miji mingine imekuwa especially dar es salaam.

Zamani tulikuwa na route ya mwenge - africana lakini kulingana na ufupi wa hiyo route naona imekufa yenyewe automatically sababu mtu anaona heri apande bajaj ya kuchangia anafika haraka sababu route ni fupi na nauli ni kidogo anaongeza analipa 1000 tu.

Arusha mji umeanza kupanuka daladala lazima waangalie route za mbali ila hawawezi kulazimisha route fupi ambazo bajaj anaenda fasta tu kuliko kukaa stendi kusubiri gari ijae na muanze kusimama kila kituo.
 
Bajaj na bodaboda,watakua wanaombea mgomo uendelee.Watakua wamepiga hela sana leo.
 
Bahati za wenzao wasilalie mlango wazi, riziki kugawana.
 
Huo ni unyimi na roho mbaya waache watu watafute pesa mbona Morogoro bajaji na daladala wanapiga ruti moja na husikii kulalamika

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Vita Ya Viongozi Wa Serikali wamiliki wa Bajaj na Viongozi Wa Serikali wamiliki wa Daladala.
 
Wanaoteseka Wanafunzi ambao ndo wengi kuliko wazazi.
 
Msitafutane uchawi bure huo mji ni mdogo hauwezi kuhimili dalala vibajaji na pikipiki lazima mmoja atolewe knockout.

hapo..remind you daladala ni vile vipanya..
Bado bolt, farasi , uber hawajagonga hodi.

Muiheshimu dar nyie watu wa chuga

Arusha bado sana ila makelel ndio mengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…