LGE2024 Arusha: Godbless Lema ameamua kususia na kujitenga kwenye Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa

LGE2024 Arusha: Godbless Lema ameamua kususia na kujitenga kwenye Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Kura feki zinaingizwa SAA 12 asubuhi zimeshapigwa unategemea nini?
 
Waswahili wanasema hizi ni Rasharasha 2025 ndio mtawajua hao ndugu zenu CCM...si mnashirikiana kula kodi za wanyonge...mtajua hamjui....
Pambaneni na wezi wenzenu...
 
Waswahili wanasema nanukuu "Mchelea Mwana kulia hulia yeye" mwisho wa kunukuu
 
Mbowe na wenzie wanalazimisha kushiriki uchafuzi huu ili wasizodolewe kushiriki uchaguzi wa ubunge mwaka 2025 ili wapate ruzuku.

Mbowe anajua, CHADEMA inajua na Watanzania wanajua, kuwa bila Katiba mpya na Sheria mpya ya Uchaguzi kushiriki hizi chafuzi ni Ujinga!

..Chadema wangesusa tusingeweza kuyajua haya anayolalamikia Godbless Lema.

..Mimi naamini vyama vyote vya upinzani kushiriki serikali za mitaa, kumeweka wazi dhuluma ktk uchaguzi, na kumeongeza uzito wa hoja ya madai ya kuundwa kwa mfumo bora wa uchaguzi Tanzania.
 
Wewe umefanya nini ili kuhakikisha nchi inakuwa na uchaguzi huru na inapata katiba mpya?

Hiyo katiba mpya itakuja kama sahani
ya wali mezani.

Mbowe mtu mmoja afanye nini.

Wenzako leo tumepiga kura ingawa tunajua matokeo ya kura hayataheshimiwa.

Timiza wajibu wako kabla hujamlaumu mtu
 
Tulishauri sana kwenye vikao kwamba kushiriki kwenye huu uchaguzi ni kosa kubwa sana. Yule mama hana anachojua zaidi ya 4R ambazo hazitekelezeki, chadema irudi kwenye siasa za jino kwa jino.
 
Zoezi la kupiga Kura likiwa linaendelea na baadhi ya viongozi wako wameshapigiwa Kura ndio unatangaza mnajitoa

Haiko hivyo duniani kote Lema aache utoto

Ahsanteni Sana 🐼
 
..Chadema wangesusa tusingeweza kuyajua haya anayolalamikia Godbless Lema.

..Mimi naamini vyama vyote vya upinzani kushiriki serikali za mitaa, kumeweka wazi dhuluma ktk uchaguzi, na kumeongeza uzito wa hoja ya madai ya kuundwa kwa mfumo bora wa uchaguzi Tanzania.
Kwamba yameanza leo Tanzania?

Wewe na Lema wote wapuuzi
 
Itakuwa kakaribia kwenda kusalimia familia Canada
 
Kwamba yameanza leo Tanzania?

Wewe na Lema wote wapuuzi

..Mimi sio mpuuzi.

..kuna kauli za 4R, na ahadi toka kwa RAIS kwamba uchaguzi ungekuwa wa HAKI.

..sasa ni vizuri kwenda nao mpaka mwisho huku tukikusanya USHAHIDI kuonyesha kwamba mambo yamekwenda kinyume na sheria, na maagizo ya Raisi.

..naelewa frustrations ulizonazo. Nakubaliana na wewe kwamba huu sio uchaguzi wa kwanza kuharibiwa.
 
Mauaji ya wagombea na viongozi wa CHADEMA ni kila kona ya nchi na wahusika wakuu ni ccm na jeshi la police🤬🤬🤬
 
Mbowe na wenzie wanalazimisha kushiriki uchafuzi huu ili wasizodolewe kushiriki uchaguzi wa ubunge mwaka 2025 ili wapate ruzuku.

Mbowe anajua, CHADEMA inajua na Watanzania wanajua, kuwa bila Katiba mpya na Sheria mpya ya Uchaguzi kushiriki hizi chafuzi ni Ujinga!
Tuliaminishwa kuwa "Magufuli ndiye aliyeratibu na kuharibu chaguzi ila kwa kuwa katangulia mbele ya haki basi waliobaki hawana baya" haya sasa kiko wapi?
 
"Nimepokea taarifa kutoka sehemu zote takribani Kanda ya Kaskazini, nimeridhika kwa kiwango cha kutosha kabisa kuwa hatuna uchaguzi, nafahamu maazimio ya Kamati Kuu juu ya msimamo wetu juu ya ushiriki wa uchaguzi huu, tatizo ni kubwa kuliko hatua tunazoweza kuchukua kwa sasa bila tathimini ya kina yenye utayari wa kuzikana nafsi zetu" -Lema

"Kwa hiyo maamuzi yoyote hata kama ni ya kujiondoa katika hatua ya sasa yatakayofanywa na jimbo lolote baada ya tathimini sahihi, mimi binafsi sitakuwa na mgogoro nayo, fanyeni tathimini katika maeneo yenu kisha fanyeni maamuzi ya kijasiri katika kuamua mwelekeo wa uchaguzi huu, mimi Godbless Lema kwa hatua ya sasa nimejitenga na nafikiri napaswa kuwa kwenye kikao kitakachojadili hatua mpya za kutafuta thamani na utu wa nchi yangu bila kuogopa mateso na mauti" -Lema

Ni chapisho la Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini na Mbunge wa zamani wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema kupitia mtandao wake binafsi wa X, chapisho aliloweka leo, Jumatano Novemba 27.2024

PIA SOMA
- LGE2024 - Godbless Lema: Viongozi wa CHADEMA Arusha wamenyimwa Viapo vya Mawakala siku moja kabla ya Uchaguzi
Chadema Kanda ya Kaskazini Imemshinda Nabii Mnyang'anyi wa Malori,

Vijana machachari wa Arusha, wenye mawazo mapya na fikra mbadala wamestaafisha mnyang'anyi bila kupenda, dah :pedroP:
 
Back
Top Bottom