LGE2024 Arusha: Godbless Lema ameamua kususia na kujitenga kwenye Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa

LGE2024 Arusha: Godbless Lema ameamua kususia na kujitenga kwenye Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Mnapotezaga Muda.......hakuna uchaguzi ....wanapoteza pesa zao
 
Mbowe na wenzie wanalazimisha kushiriki uchafuzi huu ili wasizodolewe kushiriki uchaguzi wa ubunge mwaka 2025 ili wapate ruzuku.

Mbowe anajua, CHADEMA inajua na Watanzania wanajua, kuwa bila Katiba mpya na Sheria mpya ya Uchaguzi kushiriki hizi chafuzi ni Ujinga!

..haya matukio yatuongezee ari na hamasa ya kupigania Tume Huru ya Uchaguzi, na Katiba Mpya.
 
..haya matukio yatuongezee ari na hamasa ya kupigania Tume Huru ya Uchaguzi, na Katiba Mpya.
Bitter truth. Ni muhimu CHADEMA kushiriki hizi "chaguzi" ili kuthibitisha na kuweka wazi ushahidi wa maovu yanayotendwa na dola. CHADEMA wasingeshiriki mambo yangeenda shwari kabisa na kauli yoyote kuhusu kasoro za msingi ingepuuzwa kirahisi. Hata hoja za katiba mpya, tume huru na utawala bora zisingekuwa na nguvu.
 
Umechelewa sana kujua hayo yote tulisema humu.

Mwakani mmepanga tena kwenda kupoteza muda?
 
Wakuu,

Nimepokea TAARIFA kutoka sehemu zote takribani Kanda ya Kaskazini. Nimeridhika kwa kiwango cha kutosha kabisa kuwa HATUNA UCHAGUZI, nafahamu maazimio ya Kamati Kuu juu ya msimamo wetu juu ya ushiriki wa UCHAGUZI huu wa kihuni kabisa Nchini. Tatizo ni kubwa kuliko hatua tunazoweza kuchukua kwa sasa bila tathimini ya kina yenye utiyari wa kuzikana nafsi zetu.

Kwa hiyo maamuzi yoyote hata kama ni ya kujiondoa ktk hatua ya sasa yatakayofanywa na Jimbo lolote baada ya tathimini sahihi, Mimi binafsi sitakuwa na mgogoro nayo. Fanyeni Tathimini ya uhuni na uasi huu ktk maeneo yenu kisha fanyeni maamuzi ya kijasiri ktk kuamua mwelekeo wa uchaguzi huu. Mimi Godbless Lema kwa hatua ya sasa nimejitenga na UPUMBAVU, UHUNI na UASI huu. Nafikiri napaswa kuwa kwenye kikao kitakacho jadili hatua mpya za kutafuta thamani na utu wa Nchi yangu bila kuogopa mateso na mauti

Ni chapisho la Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini na Mbunge wa zamani wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema kupitia account yake ya X, leo, Jumatano Novemba 27. 2024

PIA SOMA
- LGE2024 - Godbless Lema: Viongozi wa CHADEMA Arusha wamenyimwa Viapo vya Mawakala siku moja kabla ya Uchaguzi
Canada huyo
 
Kwa hiyo maamuzi yoyote hata kama ni ya kujiondoa ktk hatua ya sasa yatakayofanywa na Jimbo lolote baada ya tathimini sahihi, Mimi binafsi sitakuwa na mgogoro nayo. Fanyeni Tathimini ya uhuni na uasi huu ktk maeneo yenu kisha fanyeni maamuzi ya kijasiri ktk kuamua mwelekeo wa uchaguzi huu. Mimi Godbless Lema kwa hatua ya sasa nimejitenga na UPUMBAVU, UHUNI na UASI huu. Nafikiri napaswa kuwa kwenye kikao kitakacho jadili hatua mpya za kutafuta thamani na utu wa Nchi yangu bila kuogopa mateso na mauti
Kuweni watulivu wakati mnafanya maamuzi yenu.
Haya yanayo fanyika, ukweli ni kwamba yalitegemewa. Sidhani kuwa kati yenu kulikuwepo na mtu mwenye mashaka ya nini kitatokea na uchafuzi huu; kwani kazi ilikwisha anza toka mwanzo.

Lililo muhimu, ni kuwa mmethibitisha wenyewe, na wananchi wameona kilicho fanyika.
Mtakuwa hamkutimiza wajibu wenu vizuri, kama mtakuwa mmeshindwa kuchukua uthibitisho kamili kila mahali palipo tokea uchafu huu.
Huu ndio ushahidi ulio wazi mtakao utumia na kuwasaidia kuamua hatua zinazo fuata baada ya hapa..

Wananchi wameona kila kitu, lakini ni wajibu wenu kuwaendea na ushahidi mlio kusanya katika zoezi hili na kufanya nao mipango ya nini kifanyike 2025.

Mkifanya pupa, kwa kuvurugwa na uchafu huu hamtaweza kufanya mipango mizuri ya kuwashirikisha wananchi. Ndiyo maana utulivu mkubwa wa akili zenu unatakiwa sana wakati huu.
 
..haya matukio yatuongezee ari na hamasa ya kupigania Tume Huru ya Uchaguzi, na Katiba Mpya.

Chafuzi wamezijua leo?

CCM inabank on kwenye kusahau kwa wabongo, fatigue ya viongozi wakuu wa upinzani na kuwanunua kwa kupenyeza rupia.

Msimamo sahihi wa CHADEMA ambao watanzania walishawaelewa ni tamko la kamati kuu ya mwaka 2020 kuwa Chama kamwe hakitoshiriki chaguzi kwa katiba hii na sheria hizi za uchaguzi. Hizi Flip flop wala hazisaidii kumake point kwa wananchi, bali zinawaonyesha Chadema kama watu wanaoyumba ktk misimamo ya msingi na hivyo kupoteza mvuto kwa kasi mbele ya umma.
 
True.....wananchi wataamua maana wameshiriki kikamilifu kukusanya Ushahidi
Wananchi wameona kila kitu, lakini ni wajibu wenu kuwaendea na ushahidi mlio kusanya katika zoezi hili na kufanya nao mipango ya nini kifanyike 2025.
 
Tunapofunga vituo vya kupiga kura kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Taifa limeendelea kushuhudia tena ubaradhuli wa wazi na wa aibu toka kwa mamlaka zote za Serikali kushirikiana kuipatia CCM na wagombea wake ushindi wa aibu hata kwa gharama za maisha ya Watanzania.

Tunalaani mauaji na kujeruhiwa kwa wagombea, viongozi na wanachama wetu mbalimbali wakiwemo:

1) Steven Chalamila wa Jimbo la Tunduma aliyevamiwa na kukatwakatwa mapanga kikatili hadi umauti kumkuta.
2) Modestus Timbisimilwa, Mgombea nafasi ya Ujumbe wa Serikali ya Mtaa wa Ulongoni A, Kata ya Gongolamboto, Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam aliyeuwawa na askari kwa kupigwa risasi wakati wa purukushani za kuzuia kura bandia na batili kuingizwa kituo cha kupiga kura.
3)George Juma Mohammed wa Kitongoji cha Stand Kata ya Mkwese Jimbo la Manyoni Mkoani Singida aliyevamiwa nyumbani kwake na watu waliofahamika kuwa askari na kumpiga risasi iliyomsababishia umauti.

Aidha, tuna taarifa kadhaa za kujeruhiwa na kukamatwa na Polisi viongozi, wagombea, wanachama na wapenzi wetu maeneo mbalimbali ya nchi walipokuwa wakijitahidi kukamata na kuzuia kuingizwa vituoni kura bandia na batili zilizopigwa tayari kuwabeba wagombea wa CCM.

Tunataka watu wetu hawa waachiwe haraka na bila masharti yeyote.

Tunaendelea kuwasiliana na Chama kitatoa tamko rasmi zoezi hili likikamilika.

Tunaamini kinachofanyika kina maagizo na baraka zote za @SuluhuSamia na Serikali yake na au nchi iko kwenye "autopilot" na yeyote katika eneo lake ana mamlaka ya kunajisi uchaguzi anavyotaka kwani tayari wamepewa kinga na Kanuni ya 49 ya Kanuni za Uchaguzi wa Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Ngazi ya Vijiji, Vitongoji na Mitaa inayosema, nanukuu:

"Msimamizi wa Uchaguzi, Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi, Msimamizi wa Kituo, Wajumbe wa Kamati ya Rufani au mtumishi yeyote wa Umma aliyehusika na usimamizi wa uchaguzi hatowajibika kwa Jinai au Madai au kuchukuliwa kwa hatua za kinidhamu au za kiutawala kwa jambo lolote alilolifanya au kuacha kulifanya kwa nia njema wakati wa kutekeleza majukumu yake chini ya Kanuni hizi". Mwisho wa kunukuu.

Hakika Taifa lina Msiba mwingine!!
 
teh teh kuna ushahidi wa CCM kuiba kura kuliko zile kura alizokamata Halima Mdee mwaka 2020 na video zimo humu JF ukizitafuta?.

Hii hoja eti Ni muhimu Chadema kushiriki chaguzi ili kuwathibitishia wananchi kuwa CCM wanaibaga kura ni hoja muflisi.

CCM siku hizi hawaibi kura tu, wanabaka mchakato mzima wa uchaguzi!.

Na njia pekee ya kukomesha hilo ni kuwashawishi wanachi wapuuzie hizi Chaguzi feki wao wadai katiba mpya tu mpaka kieleweke. Hili linaweza kuileta CCM ktk meza ya mazungumzo ikiwa serious kidogo, lakini siyo kubariki mchakato wa chaguzi za kimagumashi.
 
Chafuzi wamezijua leo?

CCM inabank on kwenye kusahau kwa wabongo, fatigue ya viongozi wakuu wa upinzani na kuwanunua kwa kupenyeza rupia.

Msimamo sahihi wa CHADEMA ambao watanzania walishawaelewa ni tamko la kamati kuu ya mwaka 2020 kuwa Chama kamwe hakitoshiriki chaguzi kwa katiba hii na sheria hizi za uchaguzi. Hizi Flip flop wala hazisaidii kumake point kwa wananchi, bali zinawaonyesha Chadema kama watu wanaoyumba ktk misimamo ya msingi na hivyo kupoteza mvuto kwa kasi mbele ya umma.

..what is the way forward kwa haya yaliyotokea?

..maana uchaguzi sio suala la Chadema peke yao.
 
Tusibaki kwenye yaliyo ita.
Ni muhimu sana kwa CHADEMA kufanyia kazi haya yaliyoo sasa.
Itasikitisha sana kama wataamua kuwa hawartashiriki mwakani kwa vile hakuna hayo yanayo takiwa.

Kutoshiriki au kutozuia uchafuzi mwakani ina maana CCM waendelee hadi 200. Hili kamwe halikubaliki.

Ni bora kabisa kuzuia asiweo na uchafuzi mwingine hao 202; kuliko kukaa embeni na kuruhusu CCM waendelee; hata kama kutakuwa kumefanyika ahadi hewa, kama ilivyo zoeleka.

Kwa hiyo; kazi ianze sasa hivi:
- kuzuia uchafuzi mwingimne 202

- kufanya miango ya kudhibiti uchafuzi wakati wa uchaguzi wa 202
 
..what is the way forward kwa haya yaliyotokea?

..maana uchaguzi sio suala la Chadema peke yao.
Kuzuia uchaguzi wa 2025 kuwepo, bila ya kuwa na Tume HURU na sheria zinazo simamia HAKI
au
Kushiriki uchaguzi huo kibabe kama wanavyo taka CCM katika mazingira yaliyopo sasa; na kuhakikisha kuwa "UHALIFU" wa CCM utakataliwa kwa njia zote. hata ikiwa kwa nguvu za wananchi. walio tayari kukataa uumbavu.

Ni hayo mawili tu.
 
Bargaining chip waliyonayo CHADEMA ni uwezo wa kuwafanya wananchi wapuuze hizi chaguzi feki. Hili linaweza kufanyika kwa consistently kuwaambia wananchi kuwa kushiriki chafuzi hizi ni kupoteza muda, pesa.

Wananchi watawaelewa sana na in exchange CHADEMA consistenly iwe na message moja tu kwa umma, kuwa bila katiba mpya nzuri, wananchi kamwe msitegemee chaguzi za maana. Na uungwaji mkono wa CHADEMA utakuwa mkubwa mno na itaheshimiwa kwa kusimamia misingi ya maana!

Umma wa kutosha utaside na CHADEMA na hilo litaweka pressure kwa CCM kufanya reforms.

One Message ya katiba mpya baasi. Mambo mengine ni distractions, na CHADEMA ikishitiki hizi distractions umma unawaona kuwa ni walewale tu, nao wanakuwa wanapoteza mvuto mbele ya umma.
 
Back
Top Bottom