LGE2024 Arusha: Godbless Lema ameamua kususia na kujitenga kwenye Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Fisi hasusiwi bucha! Ufanye kitu na tapeli ndio utamjua alivyotapeli.
 
Mkuu 'Missile', mi nadhani hapa tunajihusisha na 'semantics' tu, sioni la maana tunapo pishana.

Utachukuwa "higher moral ground" na mtu/kundi linalo fanya uhalifu, tena wa maksudi kabisa kukuonyesha kwamba huna lolote unalo weza kufanya kuondokana na unyonge wako huo?

Hebu niambie, hiyo "higher moral ground" ina ushawishi gani kwa huyo anaye kudharau, na hata kwa hao wengine unao dhani unapigana kupata haki zao! Si na wao wataanza kukuona wewe kuwa huna lolote la maana kwao?

Ujinga "haupuuzwi". Njia pekee ya kuukabili ujinga ni kuuondoa, na siyo kuupuuza. Ndiyo maana katika wale maadui watatu alio wabainisha Mwalimu Nyerere, ujinga alikuwa ni mmoja wapo, na ndiyo sababu kukawa na sababu ya kumkabili; siyo "kumpuuza".
Hakuna "higher moral ground" ya kumpuuza mjinga; na wala hakuna "heshima itakayo onekana kwa wananch" kwa kufanya hivyo. Sana sana hata huo umma "utakupuuza", huku wewe ukidhani wana heshimu "high moral ground" unayo dhani wataiheshimu.
 
Mzanzibari anaibaka demokrasia. Halafu tunamwangalia tu
 
Kuna watu wanalazimisha eti kusisia uchaguzi ni kumuachia fisi butcher, lakini kinachoendelea ni wendawazimu kushiriki uhayawani wa hivi. Machafuko au mapinduzi ya kijeshi ndii habari ya mjini.
Hivyo wanashauri alternative ya kumuachia fisi bucha ni kushindana nae kula nyama na mifupa?
Huyo fisi ni wakumrushia mfupa wenye sumu ya kumuua.
Haki haipewi, huchukuliwa. Itahitajika mapinduzi ya kweli, sio ya jina, kuipata haki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…