Arusha Jiji Serikali yaachia TZS 5.2B kwaajili ya Vijana 4% Walemavu 2% na wanawake 4%

Arusha Jiji Serikali yaachia TZS 5.2B kwaajili ya Vijana 4% Walemavu 2% na wanawake 4%

Jesusie

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2021
Posts
1,466
Reaction score
766
===
Chini ya Sheria ya fedha ya Serikali za mitaa sura namba 290 kifungu cha 37 ya mwaka 2019 kila halmashauri inatakiwa kutenga 10% ya mapato yake kwa mwaka kwaajili ya maendeleo ya watu wa halmashauri husika kwa mchanganuo ufuatao, 4% kwaajili ya wanawake, 4% kwaajili ya Vijana na 2% kwaajili ya walemavu bila kujali dini, rangi,kabila au itikadi za siasa,
===
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dk John Marco Pima alimfurahisha sana Rais Samia Suluhu Hassan baada ya kutoa TZS1.37BL kwaajili ya kutekeleza sheria hiyo ya fedha kwa robo ya kwanza ( 1Q ) ya mwaka.

===
Nakwamantiki hiyo kama robo ya mwaka ni TZS 1.37BL kwa mwaka mzima Dk Pima kwa niaba ya Rais Samia atatoa Jumla ya Tshs 5.2BL yaani Vijana watapata Tshs 2.08BL,Wanawake Tshs 2.08BL na Walemavu Tshs 1.04BL hii ni zaidi ya Commercial Bank,
===
Arusha changamkieni fursa hii achaneni na mambo ya Ukamanda tumieni hizi fedha ili mjenge familia zenu najua ninyi kamwe hamuwezi kukimbilia Kanada mmecheleweshwa sana Arusha,
===
Angalia hii,Kama kila kikundi cha watu watano kitapewa Tshs 10M tu Rais Samia kupitia Arusha Jiji atasaidia Jumla ya vikundi 520 kwa mwaka na tutakuwa na Loan Portifolio ya watu|wateja zaidi ya 2,600 ambao kila mmoja atapewa mtaji wa kuanzia wa mil 2

===
Na hii ndio utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2020|25 iliyoahidi ajira 8M kila mwenye macho na aone sasa Juhudi kubwa na nzuri za Rais Samia Suluhu Hassan Mkt wa ccm-tanzania.
===
Tanzania tuna Jumla ya halmashauri 184 kama kila Halmashauri itakuwa na Loan Portfolio ya wateja 1,000 tu nchi nzima kwa mwaka mmoja tutakuwa na Loan Portfolio ya watu 184,000 hapa Umasikini tutausikia tu redioni,

===
Wakurugenzi wengine mnayohaja ya kuiga mfano huu mzuri wa Dk John Marco Pima mkurugenzi wa Jiji la Arusha na natamani matumizi ya 10% yawe ndio kigezo cha Ubora wa Mkurugenzi kwani wanachi lazima waone umuhimu wa kuendelea kuichagua CCM-Tanzania.

VIVA SAMIA VIVA || VIVA TANZANIA VIVA
 
Tunaongelea nadharia nyiingiiii wakati mambo straight forward kama tu mhitimu kupata mkopo wa kwenda chuo (zingatia huu ni mkopo na amefaulu) unakuwa tatizo..., alafu tunaleta siasa na propaganda
 
Tunaongelea nadharia nyiingiiii wakati mambo straight forward kama tu mhitimu kupata mkopo wa kwenda chuo (zingatia huu ni mkopo na amefaulu) unakuwa tatizo..., alafu tunaleta siasa na propaganda
Hujaona watu wakipokea mkopo?

Jaribu kuomba acha nadharia
 
Mleta Uzi umeandika Jambo ambalo kiuhalisia utekelezaji wake hakuna ,Kwa yan mwaka mmoja bl 5 point something .kama ni kweli hongera yake lakini mm najua haiwezekani na hawatapata
 
Mleta Uzi umeandika Jambo ambalo kiuhalisia utekelezaji wake hakuna ,Kwa yan mwaka mmoja bl 5 point something .kama ni kweli hongera yake lakini mm najua haiwezekani na hawatapata
Unataka kusema walimdanganya Rais?
 
Chini ya Sheria ya fedha ya Serikali za mitaa sura namba 290 kifungu cha 37 ya mwaka 2019 kila halmashauri inatakiwa kutenga 10% ya mapato yake kwa mwaka kwaajili ya maendeleo ya watu wa halmashauri husika kwa mchanganuo ufuatao, 4% kwaajili ya wanawake, 4% kwaajili ya Vijana na 2% kwaajili ya walemavu bila kujali dini, rangi,kabila au itikadi za siasa,

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dk John Marco Pima aliukuna sana mtima wa Rais Samia Suluhu Hassan baada ya kutoa tshs 1.37BL kwaajili ya kutekeleza sheria hiyo ya fedha kwa robo ya kwanza ( 1Q ) ya mwaka,Nakwamantiki hiyo kwa mwaka mzima Dk Pima kwa niaba ya Rais Samia atatoa jumla ya Tshs 5.2BL yaani Vijana watapata Tshs 2.08BL,Wanawake Tshs 2.08BL na Walemavu Tshs 1.04BL hii ni zaidi ya Commercial Bank,Arusha changamkieni fursa hii achaneni na mambo ya Ukamanda tumieni hizi fedha ili mjenge familia zenu najua ninyi kamwe hamuwezi kukimbilia Kanada mmecheleweshwa sana Arusha,

Angalia hii,Kama kila kikundi cha watu watano kitapewa Tshs 10M tu Rais Samia kupitia Arusha Jiji atasaidia Jumla ya vikundi 520 kwa mwaka na tutakuwa na Loan Portifolio ya watu|wateja zaidi ya 2,600 ambao kila mmoja atapewa mtaji wa kuanzia wa mil 2,Na hii ndio utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2020|25 iliyoahidi ajira 8M kila mwenye macho na aone sasa Juhudi kubwa na nzuri za Rais Samia Suluhu Hassan Mkt wa ccm-tanzania.

Tanzania tuna Jumla ya halmashauri 184 kama kila Halmashauri itakuwa na Loan Portfolio ya wateja 1,000 tu nchi nzima kwa mwaka mmoja tutakuwa na Loan Portfolio ya watu 184,000 hapa Umasikini tutausikia tu redioni, Wakurugenzi wengine mnayohaja ya kuiga mfano huu mzuri wa Dk John Marco Pima mkurugenzi wa Jiji la Arusha na natamani matumizi ya 10% yawe ndio kigezo cha Ubora wa Mkurugenzi kwani wanachi lazima waone umuhimu wa kuendelea kuichagua CCM-Tanzania.

Ujinga ni kipaji; ukiwa na haya mawazo utakuja kufa maskini
 
Mkurugenzi huyu yupo makini Sana, na amefanya mambo Mengi sana Arusha. Tunaomba Sasa afikirie kupaboresha stendi ndogo na kuhakikisha serkali inakusanya mapato ya kutosha na kuondosha madalali wanaonyanyasa wananchi na KUKUSANYA pesa nyingi kuliko serikali
 
Nimeshaona wanawake wengi tu wanaoipata hii mikopo kila awamu ingawaje sijawah kutana na wakiume na mara zote inatolewa kwa kikund kuanzia watu watano
 
Nimeshaona wanawake wengi tu wanaoipata hii mikopo kila awamu ingawaje sijawah kutana na wakiume na mara zote inatolewa kwa kikund kuanzia watu watano
Mikopo inatoka sana, tatizo letu sisi wanaume hawana imani kwamba tutapata
 
Back
Top Bottom