Arusha Jiji Serikali yaachia TZS 5.2B kwaajili ya Vijana 4% Walemavu 2% na wanawake 4%

Safi Sana
 
Nzuri sana hii,
 
Kazi iendelee
 
Mapingwa
 
Nyie zisikieni tu hizo fedha, maafisa maendeleo, wakurugenzi na madiwani watu wa hovyo kabisa hasa hasa maafisa maendeleo mimi ni muathirika.

Kwanza kabisa hizo fedha mwanzo wake ilikua maalumu kwajiri ya wanawake ili wawakamate kiurahisi kujiunga na sisiem ndo maana asilimia kubwa wanapewa wanawake.

Pili ili mpewe huo mkopo lazima muwe na kadi za sisiem, kinyume na hapo mtasubiri sana.

Tatu rushwa, amini nawaambieni asilimia kumi hadi ishirini lazima mlimwe kwanza ndio mtapata hizo fedha sasa unasemaje hizo fedha hazina riba? Na sisi vijana ndio tunafanyiwa sana hizi figisu ili tushindwe kuzichukua na mkibahatika kuzichukua hamuwezi kuzirejesha mfano mkipewa million kumi tayari mlishatoa million moja na nusu sasa kama mliazima ina maana katika hiyo kumi tayari mrudishe moja na nusu ya watu mnabaki na nane na nusu. Kwahiyo wao ndo wanatutengenezea mazingira magumu ili ionekane vijana hatuaminiki.

Na halmashauri zimejaa figisu kwa ufupi zilongwa mbali zitendwa mbali
 
Awamu ya Sita kila kitu bambam
 
Mkuu unaoushahidi wa hili?
 
Mkuu unaoushahidi wa hili?
Nimesema mimi ni muathirika ilifika hatua tulikosana kabisa na wakuu wa idara nikaamua kuachana nao maana mimi huwa sipendi ujinga na mambo ya meusi, kama 1+1=2 basi na iwe hivyo lakini usije ukanambia 1+1=11 halafu utegemee nitakufumbia macho.
 
Mkuu wewe uliomba wapi?
Hapa tunazungumzia halmashauri zetu sio benki, unanipata? Na kama umewahi kwenda kukopa lazima narudia tena lazima ulikutana na kati ya hayo niliyoyaandika kwenye huu uzi.
 
Hapa tunazungumzia halmashauri zetu sio benki, unanipata? Na kama umewahi kwenda kukopa lazima narudia tena lazima ulikutana na kati ya hayo niliyoyaandika kwenye huu uzi.
Nikweli urasimu upo ila pesa inatolewa kwa sasa, Nenda kajaribu tena
 
Nikweli urasimu upo ila pesa inatolewa kwa sasa, Nenda kajaribu tena
Mkuu soma kwa umakini post namba 69.utanielewa.

Sijasema pesa hazitolewi kabisa no ila uwe tayari kukubaliana na masharti ya hovyo wanayowekwa ambayo ni kinyume kabisa na utaratibu au mwongozo wa serikali.
 
Naona mkurugenzi wa jiji Arusha anajipigia promo mwenyewe! Ripoti ya CAG ndio itakuwa kipimo chake cha utendaji kazi! RC Mongela alionyesha wasiwasi mkubwa gharama ya ujenzi wa vizimba vya wamachinga jijini Arusha (value for money).
 
umeandika kwa hisia sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…