Arusha Jiji Serikali yaachia TZS 5.2B kwaajili ya Vijana 4% Walemavu 2% na wanawake 4%


Safi sana hii, Tanzania nakupenda sana,

Hakuna Kama Rais Samia
 
Naona mkurugenzi wa jiji Arusha anajipigia promo mwenyewe! Ripoti ya CAG ndio itakuwa kipimo chake cha utendaji kazi! RC Mongela alionyesha wasiwasi mkubwa gharama ya ujenzi wa vizimba vya wamachinga jijini Arusha (value for money)


Umemjuaje?
 
 
Una tatizo kubwa sana. Unahitaji upate counselling ya haraka sana. Hopeless kabisaaa
 
Andiko zuri, uneharibu hapo tu "kwa niaba ya Mhe. Rais." Jamani, hizi hela Halmashauri inakusanya yenyewe na kugawa yenyewe kadiri ya vigezo na miongozo ya kibajeti. Sasa hapa Mhe. Rais anaingizwa vp. Why asisifiwe huyo Mkurugenzi kwa kuhakikisha kila alichokipata ametenga badala ya kujilipa madai ya madeni na maposho? Sifa nyingine tunamuharibia Rais wetu mpendwa
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23]. Mkuu ukoo ofisi gani na mkoa upi mbona nasoma porojo zako tu hapa, kulingana na utoaji wa huu mkopo sehemu niliyopo na ulivyo viongelea ni mbingu na ardhi
Wahenga walisema ukitaka kuonja utamu ngoma ingia ucheze, sasa nikuulize wewe kama wewe umewahi kwenda kukopa hizo fedha na ukapewa bila longolongo yoyote? Usiseme nimeona wanapewa nimekuuliza wewe.
 
Habari nzuri sana hii
 
Basi mna bahati jamaa yangu, sisi huku tuliko swali la kwanza wanauliza upo upande gani kama huna chama lazima muandikishwe kuwa Wana ccm na mnapewa kadi, wakigundua mpo chama kingine aisee mtasubiri sana hata kama mradi wenu una manufaa ya moja kwa moja kwa jamii na serikali.
 
Pesa hzo zimaliwaga na wajanja hamna kitu hapo ni kupeana tu moyo na kufoji data
 
Wewe uliye andika hili bandiko uliishawahi kuupata huo mkopo unaoobgelewa apa
Mimi niko Rombo, hiyo mikopo ta Vijana, wanawaje na walemavu inatolewa kila siku.

Tatizo kubwa ni vikundi hasa vya vijana na walemavu hawarudishi pesa.

Maana watu wanajiunga kikundi ni ilimradi wapewe pesa , hawana mradi wowote wa kikundi wala vision ya pamoja.

Wengine wakishapewa pesa wantimkia Dar.

Ila pesa zipo tele tena ni mikopo isiyo na riba kabisa.

Hivi karibuni kuna vijana 12 wamekopa 30M kununua pikipiki kila mmoja kuoiga bodaboda.

Kwahiyo vijana ushirikiano ndio mafanikio.

Mkishindwa kushirikiana kujiletea maendeleo, mtashirianikishwa kumpigania mwanasiasa ajaze Tumbo lake na watoto wake na michepuko yake.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…